Thursday 30 May 2013

Re: [wanabidii] Waarabu wa Dubai na Wachina Kujenga Kigamboni! Wananchi hawajaambiwa!

Mdugulile mimi pia naunga mkono watu kuelimishwa, nasikitishwa na kusononeshwa sana na hii tabi ya Serikali kupanga mipango isiyotimilika kwa miaka nenda rudi, mfano ni huu wa hapa au hata kule Airport kuna watu wamefanyiwa tathmini mwaka 1997 hawajalipwa mpaka leo hii...lakini pia kwanini na nyie wabunge msiibane serikali au hata makampuni binafsi mkawa mnapima haya maeneo yenu kuliko kuwa squatter?



From: Faustine Ndugulile <fndugulile@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, May 30, 2013 4:54 AM
Subject: [wanabidii] Waarabu wa Dubai na Wachina Kujenga Kigamboni! Wananchi hawajaambiwa!

Mimi ni memba wa Jukwaa kwa muda mrefu sana. Mara nyingi nimekuwa msomaji kuliko kuandika huku.
Nilitaka kutoa ushauri mdogo kuhusu suala la Mradi wa Kigamboni.
Ili kuwa na mjadala mzuri wenye tija, ni vyema wadau mkafanya utafiti mdogo kuhusu mradi huu.
Tembeleeni Kigamboni na kuongea na wananchi au kama mna ndugu wanaoishi eneo hili. Waulizeni kuhusu uelewa wao kuhusu mradi, ushirikishwaji wao na ufahamu wao kuhusu haki, stahili na hatma yao.
Mkifanya hivi mtapata ufahamu wa nini wananchi wanacholalamikia.
Wasalamu
Dkt Faustine Ndugulile
Mbunge-Kigamboni

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



0 comments:

Post a Comment