Wednesday 29 May 2013

[wanabidii] Re: KILICHOMUUA NGWEAR NI MADAWA YA KULEVYA

bado sijakupata where you got the full info kwamba ni madawa ya kulevya ndugu let me know tu maana watu wanasema tu juuu juu maana hata watu ambao wako huko south africa hawasemi hivyo

On Wednesday, May 29, 2013 12:51:05 PM UTC+4, Abdalah Hamis wrote:
Taarifa ambazo Lenzi ya Michezo imezipata kutoka Afrika ya Kusini kwa HusseinOriginal ambaye yupo Pretoria, amesema Ngwear amefariki leo asubuhi kwenye gheto ambalo alikuwepo pia msanii M to The P ambaye yeye amelazwa hospitali akiwa mahtuti. 

"Tulivyokwenda kuwagongea asubuhi tuliwakuta Ngwear amefariki na M To The P akiwa amepoteza Fahamu Kabisa"

Baada ya kuwapeleka hospitali Daktari alitibitisha amekufa na ameshatoa taarifa kwa watu wa Karibu wa Ngwear huko Afrika nya Kusini.

Ngwea akiwa na msanii M to the P walitakiwa kurudi Dar leo lakini waliwakuta wamezimia kwenye chumba wote wawili baada ya kuzidisha (overdose) madawa ya kulevya na M to the P.

Hata hivyo mama yake Ngwear ambaye yupo nyumbani kwao Morogoro amethibitisha kupokea taarifa ya kifo cha mwanae na kusema kuwa taarifa za kuwa za kuwa alikuwa Afika ya Kusini alikuwa hana kwani mara ya mwisho kuongea naye zimepita wiki mbili sasa.

Pia amesema taratibu za maandalizi ya mazishi yatakavyokuwa yataanza baada ya kufika baba yake mdogo Ngwear ambaye yupo mkoani Ruvuma kwani anatarajiwa kuwasili kesho Morogoro.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment