Wednesday 29 May 2013

Re: [wanabidii] Waarabu wa Dubai na Wachina Kujenga Kigamboni! Wananchi hawajaambiwa!

Haya ngoja tumsubiri Prof alete ushahidi wa hiyo mikutano ya uwakilishi, itasaidia kuwakamata waongo. 

From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Wednesday, May 29, 2013 9:14 PM
Subject: Re: [wanabidii] Waarabu wa Dubai na Wachina Kujenga Kigamboni! Wananchi hawajaambiwa!

Hapo ujue Alexander kuwa-aidha kachoka kiakili kutokana na safari ndefu, matatizo mengi na stress ya kazi. Lakini kila kitu kumtaka Rais ajibu na hata kila sekondari iandamane kupata jibu Ikulu ina maanisha kuna tatizo la usimamizi na labda kuna vacuum kiwizara. Kama ni mimi, sitoruhusu kuwa nijibu kila kitu. Kwanza nitamwita kiongozi wa sekta husika. Ni uonevu kumtaka yeye ajibu daima. Hata kama ni Mkurugenzi atasema-subiri kwanza nitakupa jibu kesho au baadae. Kisha ataita kiongozi au viongozi husika, apate taarifa na mrejesho wake utakuwa baada ya mawasiliano nao, nao atawaita wawepo ktk kikao huenda kuna hoja nyingine unazo. Hiyo ndio participatory management.

Tunajua kijana wa watu hamumpendi na mnajaribu kufanyakila la kufanya kumuonyesha hafai daily. Ila huyo kaundwa na baba wa Taifa Mh Nyerere-akimuandaa akampika, akaiva. Amefanya mengi sana ila roho zetu tu mbaya, mbaya sana. Tumemkabidhi kwa Bwana, tumemuwekea ngao ya ulinzi. Abarikiwe na ikiwezekana aongeze miaka ifike mpaka 2017 atutoe hapa na katiba mbya na Dubai yetu kigamboni.

Wewe ulie tu Alexanda. Hata wakija kujenga hao wa Dubai-mbongo au mtanzania atachakachua tu mipango miji. Hata hiyo shea yake ya ubia ataiuza, apate hela chapuchapu akamtoe mwali, kutamba bar na viroba au kuvaa mitumba. Si nilikuambia sisi tulikuta Nyamisati, maeneo ya Rufiji kuelekea Somanga, Kilwa yamekuwa fenced yameuzwa 2008. wangapi wanajua kuwa Mafia kunajengwa International Airport na Bandari ya kisasa ya kuunganisha utalii na uchumi visiwani huko na TZ na ZNZ?  Nimekuonyesha maprofesa wanalowa maji vibaya, kutembea peku miguu chini kazi ya serikali. watu wanafukuzwa na tembo serengeti, kuibiwa pochi na baboon anafungua dirisha na kutoroka na kipochi/bag-upo kazini umetumwa kufikia wananchi uje useme wanasemaje. Kimepangwa, viongozi wao hawawezi hata kutoa taarifa za pesa za NCAA au za mwekezaji walizopewa wakafisadi-kesho wanasema wanazuia hiki au kile (wanaficha mengi). basi tu watu wananyamaza maana usisema hovyo siku yako ya kufa na kumwagiwa tindikali huijui. Hiki cha kukomoana, kuzibana midomo, visasi kitaua sana demokrasia.

Hebu angalia kiambata uone kuwa ustaarabu wetu na wastara wa Dubai na Ulaya upo tofauti. Watu wa Mtwara wana usemi usemao- 'Yonda ni Yonda tu hata umfanyeje'. Jee, unajua yonda ni nini (maanake 'Nyani').
Na kwa usemi huu, wao nao wamefanya nini hivi karibuni? Sembuse hao wa kigamboni?

Ni sawa na kuogopa ukweli halisi wa uwezo na kumkabidhi mvunja mawe kwa sepetu wa kunduchi mbuyuni Kiwanda cha Wazo Hill waSwden watakapotaka kuondoka. Ni kama hao small scale miners wa Butiama wanaodai Industrial mining complex ya Stamico/Meremeta wapewe wao. Watazalisha kwa sululu au machinery? Watazitoa wapi, machineri ambapo mining ina utata wa mauaji ya albino. Hilo likiwada hayo yatafanyakazi? Wana wasomi walioajiri? wameunda kampuni na wanahela za uendeshaji? Mengi ni usiku wa giza-jazba zitatumaliza.

Kama tumeshindwa usafi na kulinda urban plan mjini Dar-wacha tutengeneze Dubai ya pili Kigamboni.

Mbongo ana desturi anapotaka kukwepa majukumu au kuwajibishwa. Hata umuhusishe vipi bado atasema hajahusishwa. Atadhania kwa kusema hivyo atapata sifa. hajui anajiharibia.

Ni sawa vijijini ambapo mna donor, NGO au GVt funded projects. Ukifika mtu mpya wanaweza wakawaambia kuwa-hatuna funding wala msaada wowote. Tuna umasikini. Utaona mradi utauliza-watasema hii complex walijichangisha wakajenga wenyewe. Wanadhania kwa kukataa kuwataja waliotangulia kuwapa misaada watapata zaidi. Kumbe hawajui mlikwisha kupitia maofisini kwa other agents na kupata secondary sources zenye taarifa.

Safari moja tukatoa CD na kuionyesha organization husika yule nurse aliyesema haujui mradi huo. Kumbe alikuwepa ktk kikao na sherehe ambapo watu walikula mziki hapo na ngoma za asili pia akiwemo akinengua. Uso wake ulikuwa mdogo kana senti tano kwa aibu kujiona kikaoni akijadili na akicheza pia. Tulifika tumechelewa kikaoni hivyo alipata muda wa kusema uongo. Tulipoelezwa hapo hayo kuwa mbona mradi wa NGO yetu hawaujui? Nasi tulikwisha kuwapa report kibao-tukasema si una video system hapo, pembeni? Ngoja tuweke CD-ilikula kwake huyo mfanyakazi naye ni mmoja wa afisa wa idara yake attached kwetu.

Subiri mama Tibaijuka awataje, atoe na picha za vikao nao va viongozi hao na vikao na wananchi uipate mwanaharakati. Pia atoe na sahihi zao za kupokea 'Posho' ya kikao siku hiyo!! Kumbuka kuweka vidhibiti vya vikao na majadiliano-ni muhimu sana.

Hii ndio -Bongoland. Watu wanaubongo wa kukoroga mazuri kuwa mabaya daima tupo katika mzunguko usio uharaka wa maendeleo bali jazba na majungu ndio raha yetu. Hatujitambui bado. Tungekuwa m,bali sana kimaendeleo. Aje dictator itatusaidia. pokea zawadi ya kiambata.
Yule yule!!

--- On Wed, 29/5/13, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:

From: alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] Waarabu wa Dubai na Wachina Kujenga Kigamboni! Wananchi hawajaambiwa!
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, 29 May, 2013, 12:52

Kiwasila,
Kuna project na tu-project. Huwezi kutegemea project kubwa kama hii Rais asijue. Basi hata kama anajua na hataki kulizungumuzia kuna namna ya kulisemea jambo. Hivi unapomwambia mwananchi wa kawaida kua, na mimi (Rais) nimeambiwa tu ni kabariki, kama hawatawaeleza vizuri, nitakuja mwenyewe kulisemea hili jambo wakinieleze vema, watu wakueleweje?? 
Alexander

From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Wednesday, May 29, 2013 1:49 AM
Subject: Re: [wanabidii] Waarabu wa Dubai na Wachina Kujenga Kigamboni! Wananchi hawajaambiwa!

Hivi huyu Rais wa nchi anayetakiwa kujua kila cha jikoni ni kinyonga ambaye machio yake yanageuka mduara kuona pande zote au pweza mwenye mikono/mikia pande zote na macho kama kinyonga?

Nini maana ya kuwa na Waziri, wakuu wa Mikoa, Wilaya; Mbunge, Diwania na watumishi wa ugani wa sekta mbali mbali pamoja na directorate zao na wahamasishaji? Mbona wabongo twapenda lawama hatuna zaidi ya negative orientation kwa kila kitu.

Yaani kama ni mume na baba wa familia-ujue pini ya nepi ya mtoto inakaa wapi sio mama na housegirl kufahamu kiti na ujue mpaka kizoleo cha taka kwa muda huo kipo wapi.

Si la kushangaza ukafika kijijini na Diwani au mbunge ukamuona naye anauliza maswali ambayo ni wajibu wake. ila, anafanya hivyo hapo kwa kupata/ili kupata sifa na ukaona watu wanamshangilia. Mfano ni ule wa -eneo letu mkoa huu una vijito/mito 50 inayoingia baharini lakini hakuna umwagiliaji-serikali inatufanyia nini? Kuna mazao yamejazana hapa hakuna soko-serikali inatufanyia nini? Muulize kama amekwisha kufika hata kwa bwana kilimo wakakaa na kupanga jinsi ya kuhamasisha wakulipa kujiunga kukodisha gari wakapeleke kwenye soko, wapate mkopo wa lorry la kati baadae special vehicle ya kusafirisha mazao yanayoharibika kama nyanya, kabishi etc. wapo wakulima wa Lushoto wafanyao hivyo. Kuhamasisha traditional irrigation system ambayo ipo TZ toka kilimo kianze duniani hadi leo.

Hivi kweli Tibaijuka atapaka tu pekee kila kitu etc wengineo hawajui?  Basi huko UN habitati alikotoka ni shirika la ajabu duniani. lakini hapa TZ, hata yale maeneo ya World Bank funded Sites and Services; Un-habitat SUDPF approach iliyopata sifa 1990s; NHC ya Mid 1970s; Squatter upgrading ya kuongeza barabara na kuweka umeme, EPM na  ya sasa Community infrastrucural Upgrading Program (CIUP) Dar yote na Miji mingine ambayo CIUP  hela la mkopo bank ya dunia na ni participatory na wanachangia na kuweka hela bank wenyewe-bado baada ya upgrading wanajaza takataka katika mitaro hiyo waliyogharimia na viosk kukaa barabarani na kufanya kinyume na bylaws waliotunga wenyewe. Kaione hii CIUP Manzese Uwanja wa Fisi, Manzese kwa Jongo. Pia kulikuwa na Mkopo wa worl bank wa sewerage rehabilitation, kuundwa kwa DSSD na sasa mipango shirikishi ya kuzoa takataka kwa kuupa madaraka Mtaa na wakazi kuunda CBO/NGO ya kuzoa taka (kujipa ajira na kuajiri vijana) na wakazi kulipia uzoaji taka-vimeshindikana!! Baadhi ya wananchi kuamka usiku kutupa viroba vya takataka barabarani ili asilipe 500/= kwa siku kutoka biashara yake. Kutoboa choo na mtaro kumwaga kinyesi na maji machafu ili asiite private sector tankers kunyonya uchafu ili asilipie. Yakifurika-serikali haitujali. Chandarua akipewa bure asipate matende na malaria-anafunikia mchicha na kuokotea chupa barabarani anajaza ndani ya chandarua ndio kibebeo!

Ujenzi na uuzaji wa nyumba za NHC za bei nafuu mfano-Tabata, nenda kaangalie sasa uone kama ile design na makazi yapo ilivyotegemewa ili kutatua tatizo la nyumba kwa wasio uwezo. Zile nyumba za milion 3 sasa ni saluni za nywele, maduka, barabara zimezibwa wameweka vibanda yaani ni wazimu. Moto ukiwaka-hakuna pa kupita kuuzima.

Na majengo kama hayo Mbezi beach na maeneo mengine wanakojenga kukopesha watumishi na raia-sheria iwe kali kwamba kama mtu akiziba njia, kubadili design na kuweka bar badala ya makazi; kuongeza majengo mengine mpaka maghorofa kwenye plot 100% kubadili site view na kufanya overload ya utilities-apigwe fine na vibomolewe kwa gharama zake. Ama sivyo-pamoja na effort zote za toka 1970 za NHC nyumba vyumba 6 na zile ndogo; juhudi za BRU-ARDHI; Habitat na SUDPF na sasa CIUP ya City Council na Halmashauri-hiyo Satellite Cities Ideology or Plan ni escape tu kutokana na kushindwa kushughulikia matatizo yaliyokuwa toka 1970 ya kutokuwajibika kwa wananchi (hasa kwa sasa) wanaoharibu city building and service plans na mfumo husika wa usimamiaji kushindwa kufanya kazi yake katika kusimamia mipango miji.

Ni kama kukataa kufua nepi za mtoto kila wakati awekapo kinyesi na kutokumrekebisha atumie pot yake. Kwa vile anaweka kinyesi nguoni hivyo unamlala bila nguo na anashinda uchi kutwa-pamoja na risk zote unamwacha hivyo-escape usifue uchafu.

Mh Tibaijuka sasa ameacha kubomoa majengo yaliyoziba njia, kubananisha au kujazwa ktk plot kinyume na city/area plot plan; kuwaondoa wa mabondeni wanaohamia kimakusudi anauza kariakoo ya NHC ya 60,000/= in 1974 sasa ni 1 billion anahamia Jangwani-Sunna, kigogo mkwajuni na Ilala-Baghdad, Mtoni Bondeni etc. Bila ya kuushughulikia -Uswahili na Swahili mentality ya  Watanzania, hatutofika mbali. Tukitekeleza sheria-tutafika pazuri, kuogopana na visasi-tutabaki na kuwa kituko cha kucheka na hii E.A. Community ndio jamvi la wageni.

TZ ni kuhama toka plan hii haijaisha au imevurugwa na kudandia ingine re-inventing the wheel always bila kutatua shina la tatizo.

Ni mikopo na gharama kwa serikali na walipa kodi, ni mipango isiyo endelevu inaishia kati. Tutachekwa sana nchi jirani na nyinginezo, tutakuwa tukisifia miji na vijiji vya wenzetu kumbe nasi twaweza ila tu wa culture ya-haambiliki, tusiombenda ukweli. Hatuoni vibanzi vyetu machoni, hatujifunzi kutokana na makosa, daima ni kurudia makosa kutokana na mtazamo kuwa-daima mkosa si sisi ni wengineo nje ya sisi kwani sisi (wananchi) hatumo hatuhusiki.

Kwa nini nchi hii Mungu asiizamishwe kisha kila kitu kije kipya yaani iundwe upya kuje na uzao mpya sio huu?

--- On Tue, 28/5/13, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:

From: alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com>
Subject: Re: [wanabidii] Waarabu wa Dubai na Wachina Kujenga Kigamboni! Wananchi hawajaambiwa!
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, 28 May, 2013, 16:28

Hotuba ya Kikwete huko mbagala, na hoja ya mbunge wa kigamboni vinachefua hali ya hewa.

Ndugu zangu, tuihurumie nchi yetu japo kidogo. Inaonyesha serikali haijifunzi kwa machafuko yanayoendela Mwara hivi sasa. Unawezaje kutekeleza mpango mkubwa kiasi hiki wa kujenga nyumba zaidi ya 15,000 bila kuwashirikisha wananchi na hata mbunge wao? Je! mpango kama huu kikwete anadai kukwepa kuujua sawasawa na kwamba yeye amebariki mapendekezo ya manisipaa husika. 

Hili jamani ni haki kweli? Je! Rais Kikwete anataka kutuaminisha kua hajui huu mpango KAMAMBE na kwamba yeye amepewa tu mapendekezo na manispaa husika? Na kwamba akielezwa vizuri ndipo ataenda kuwaeleza wananch kama wahusika hawatafanya hivyo?? Kwamba yeye mwenyewe haujui huu mpango vizuri mpaka aelezwee?? Jamani tuache kufanyia nchi mzaha. 
Alexander

From: Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, May 28, 2013 5:44 PM
Subject: Re: [wanabidii] Waarabu wa Dubai na Wachina Kujenga Kigamboni! Wananchi hawajaambiwa!

Seleman Matthew naamini ana upeo na uelewa wa kutetea wakazi wa Kigamboni sijajua hao madiwani wenzako hali zao zikoje

2013/5/28 Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>
HII nimeiangalia na kusikitika, nimeangalia mkutano wa rais wetu kwa wananchi nikasema hivi huyu mtu anapata wapi nguvu ya kuongea vile lakini sasa najiridhisha kuwa unafiki ndio tatizo kubwa. MABADILIKO hatuna haja ya kwenda mbali, tunawabunge humu wanaoingia mjengoni na ilivyoimani ya wote bunge lina simamia serikali waache unafiki hapa wafanye ambacho mie na wewe tunakitegemea.

Satellite cities si idea mbaya nilifanya kazi kwenye hizo projects nimepata bahati ya kusoma mapendekezo ya wataalam tatizo nilionalo hapa final implementation sina uhakika kama itakwendana na kilichotarajiwa, kama kawaida the whole idea inaweza kuwa raped kama mlivyosikia mwarabu na mchina washalamba tenda masikini mtanzania haielezwi wazi atahusika hivi na ni vigezo gani vimetumika kwanza kulipitisha hilo eneo kuwa jiji na zabuni za kudaka tenda zilienda vipi haiko wazi najiridhisha kuwa the whole idea is Rapped.
Kesho tutasikia Dar ring road inajengwa bunju na pugu vibanda vinavunjwa. It is ok lakini kama rais anasema aulizwe diwani ambaye yeye kama mimi hajui na mbunge wa eneo husika hajui wao wanaambiwa tu kama wewe unavyoambiwa na kibaya zaidi tunajua uweza wa madiwani zetu si katika kuwakashifu lakini ni ukweli uweza wao wa kuchanganua mambo mdogo sijui tunakwenda wapi.
Ingependeza hili suala lisiwe la kisiasa watu wasitupwe nje kama enzi za mkoloni anachukua aridhi afrika kusini niliyoyasoma kwenye vitabu vya historia yatajirudia.

2013/5/28 Wanakijiji Kimbiji <wanakijijikimbiji@yahoo.com>

   MJI MPYA WA KIGAMBONI ! SASA WANANCHI TUPO NJIA PANDA !
   Kauli ya waziri wa Ardhi Bunge inawapa mashaka wakazi wa Kigamboni,

   Mpango wa siri ya kuwafukuza wenyeji wa Dar na kuwaweka wageni ndio
   Agenda ya Wizara ya Ardhi,
   
   Watanzania sasa tuna miaka 51 ya Uhuru,lakini tupoangalia tutajikuta 
   tunaingia katika migogoro ya Ardhi na uvunjivu wa amani utakaosababishwa
   na Ardhi.
   Ni mda mchache tu huko bungeni Dodoma waziri wa ardhi Mhe.Bi Anna
  Tibaijuka ameliezea bunge kuwa nyumba takribani elfu 30 zitajengwa na 
   makampuni ya Dubai na Wachina, na wakazi wa Kigamboni watakuwa na hisa !
   Kauli hiyo ya waziri Anna Tibaijuka inawatia wasi wasi wananchi na kujiuliza
   maswali mengi kama vile kuwa na hisa katika biashara hipi? nani mmiliki wa
   Ardhi? mbona wananchi wa Kigamboni hawajapewa taarifa yoyote!
   hakuna kikako chochote kile kilicho washirikisha wananchi na kujua
   hatima yao ! mbuge wa Kigamboni Mhe.Ndugulile naye kashangazwa na

   TATIZO LA KUWAMILIKISHA ARDHI WAWEKEZAJI LITALETA UTATA,
   Wenyeji wa asili ya mikoa ya Dar-es-salaam na Pwani, wamejawa na unyonge
   na kujiona wapo katika kilio cha kusaga meno kwa kuondolewa katika sehemu
   zao za asili na kutojua wapi watapelekwa,
   Tabia za baadhi ya wajanja kumiliki mashamba makubwa nalo limekuwa ugonjwa
   ulijitokeza katika kumiliki Ardhi.
   
   UVUNJWAJI WA SHERIA ZA ARDHI
   Migogoro mingi ya Ardhi inatokana na uvunjwaji wa sheria zilizopo
   na wizara inahusika kwa namna moja au ingine katika kuvunja sheria hizo,
   Kuna Ardhi zinazomilikiwa kimila,pia na manispaa, lakini Wizara ya ardhi
   imekuwa ikiwanyang'anya wazawa na kuwapa wawekezaji wa kigeni ardhi
   hizo bila ya kuwashirikisha wahusika,wananchi,serikali za mitaa na manispaa.
   Ni juzi tu wakazi wa eneo la Tuangoma, njia panda ya Amani beach huko
   Kimbiji walijikuta wanabobolewa majumba na kulazimishwa kulipwa
  fidia la Sh.700,000 kwa heka ! na muwekezaji wa Kichina ndio kaanza
   kazi? Wanajeshi nao wanajaribu kuwatishia maisha wanye mashamba 
   ili wapate mashamba ya bure.
   Serikali ilitupia jicho tatizo la Ardhi tusije tukawa watumwa katika nchi yetu.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
Bariki G. Mwasaga,
P.O. Box 3021,
Dar es Salaam, Tanzania
+255 754 812 387

0 comments:

Post a Comment