Friday 25 January 2013

[wanabidii] Mapendekezo ya Kamati ya PAC kuhusiana na ZECO

Kwa mnasaba wa maelezo ya hapo juu, Kamati inatoa mapendekezo yafuatayo kwa Barza la Wawakilishi la Zanzibar ili iiagize Serikali ya Mpainduzi ya Zanzibar, na kuitaka itekeleze mambo yafuatayo:

1. Viongozi wa Bodi ya Wakurugenzi waliomaliza muda wao 2012, msisitizo ukiwekwa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakuregenzi, Ndg Mohd Hashim Ismail, wachukuliwe hatua za kisheria kwa kuliingiza Shirika hasara zisizo za lazima, (Tsh 31,179,000/-) kwa malipo ya faini kwa Kampuni ya Kichina (China Railway Jianchang Engineering Co (T) Ltd (CRJE)), ambapo hasara hii imesababishwa na uzembe na ubinafsi wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi pamoja na wajumbe wote wa Bodi hii kwa ujumla.

2. Menejimenti ya Shirika la Umeme ichukuliwe hatua za kinidhamu, kwa uzembe wa kutosimamia ipasavyo majukumu ya Shirika, kuleta migogoro miongoni mwa wafanyakazi wake, kushindwa kulisimamia Shirika, Shirika kupoteza mapato yake, kujenga mazingira ya upendeleo  yenye kuleta ubaguzi katika kazi na kupunguza ufanisi katika utendaji wa Shirika la Umeme kwa ujumla.

3. Wafanyakazi wote wa Shirika waliotajwa kuhusika moja kwa moja ama kwa namna yoyote ile katika ripoti hii, pamoja na Watenadaji wa Shirika waliokuwa sio waajiriwa wa Shirika ikiwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Shrika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC-TV) alieruhusu Kampuni ya Zanzibar Data Com kutumia umeme kinyume na taratibu na sheria, wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria kutokana na kuhusika kwao katika kulihujumu Shirika kwa njia yoyote ile.

4. Serikali ipige marufuku na isimamie kwa udhati Kampuni zote binafsi, ikiwa ni pamoja na Kampuni ya GECCO kufutiwa vibali (ambavyo Kamati inaamini vimetoka kinyume na sheria  ama kwa namna yoyote iliyo), na badala yake kazi zinazohusiana na utoaji wa huduma ya umeme ziendelee kufanywa na Shirika la Umeme pekee, kama Sheria Nam 3 ya mwaka 2006, inavyoelekeza.

5. Watendaji wa shirika amabo pia ni wafanyakazi ama wamiliki wa Kampuni ya GECCO (pamoja na wafanyakazi wa Shirika wanaosaidia kazi za GECCO) kama walivyotajwa moja kwa moja ama kwa utaratibu wowote katika ripoti hii, wachukuliwe hatua za kinidhamu kwa kudhoofisha utendaji kazi na ufanisi wa Shirika.

6. Kwa kuwa uendeshaji wa majenereta 32 umekuwa ni mzigo mkubwa kwa Shirika, Serikali ama ichangie ruzuku katika uendeshaji wake, au kutafutwe utaalamu utakaowezesha majenereta hayo kutumia diseli ya kawaidia yenye gharama nafuu au yauzwe na badala yake yatafutwe mengine kwa mujibu wa Sheria, yatakayoweza kutumika kama inavyokusudiwa. 

7. Kwa kuwa Kamati imepata wasiwasi kwamba kuna hujuma imefanyika iliyopelekea kukosekana kwa umeme Unguja ndani ya miezi mitatu 2009/2010, Seriali, ndani ya kipindi cha miezi mitatu baada ya kuwasilishwa ripoti hii, iuende Tume iliyohuru  ya Kuchunguza chanzo na sababu zilizopelekea  kukosekana kwa umeme huo  na ripoti yake iwasilishwe na kujadiliwa katika Baraza la Wawakilishi.

8. Kwa kuzingitia matakwa ya Katiba, Serikali, kupitita Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar, ifanye ukaguzi wa fedha zilizotumika kurejesha huduma ya Umeme, Unguja baada ya kuzimika na kukosekana kwa kipindi cha miezi mitatu (Disemba 2009  hadi Machi 2010 )

9. Bila ya kuathiri masharti ya Katiba, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, ifanye ukaguzi maalum wa Hesabu za Shirika kwa kipindi cha miaka mitatu (2009 – 2012)

10. Kwa kuwa Zanzibar hakuna chombo kinachoratibu bei ya umeme, kama vile EWURA kule Tanzania Bara, na kwa kuwa ZECO hujipangia bei kwa matakwa ya EWURA, Serikali ilete Sheria ya kuanzisha chombo kitakachohusika na kudhibiti bei ya umeme Zanzibar, ambapo pamoja na majukumu yake mengine, kitashauriana kwa karibu na EWURA ili ZECO iweze kutoa huduma bora na fanisi na kupatikana kwa muafaka wa bei ya umeme Zanzibar.

11. Kwa kuwa moja kati ya dosari kubwa ya deni la umeme inalodaiwa ZECO na TANESCO inatokana na Zanzibar kukosa umeme wake, na kwa kuwa katika hili wananchi wa kawaida ndio wanaoumia na kuathirika zaidi, Serikali ihakikishe Zanzibar inazalisha umeme wake wenyewe na sio kuendelea kutegemea umeme kutoka Tanzania Bara.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment