Friday 25 January 2013

[wanabidii] Kamati ya Baraza la Wawakilishi – Uchunguzi wa ZECO

Ufuatao ni muhtasari wa kamati ya Baraza la wawakilishi inayowakilishwa na kamati ya PAC ikiwasilishwa na mwenyekiti Mh Omar Ali Shehe juu ya uchunguzi wa ZECOm (Zanzibar Electricity Coop)

Hii ni ripoti ya tatu kwa Baraza hili ikitanguliwa na zile ripoti za mambo mbalimbali na ripoti kuhusiana na Baraza la Manispaa.

- Shirika la umeme lina dhima kubwa juu yetu.

- Suala la huduma ya umeme lina umuhimu mkubwa nchini mwetu. azma ya serikali ni nzuri kwa kuamini ni lazima kila mwananchi anafaidika nayo.

- Huduma hii imesambaa maeneo mengi ya mjini na vijijini Unguja na Pemba

- ZECO kama shirika lina wajibu wa kuingiza mapato ya kujihudumia wenyewe na kuongeza mapato kwa serikali

- Kamati ilifanya majadiliano na ZECO na kupanga maeneo ya kutembelea pale itakapoona ipo haja ya kufanya hivyo

- Kamati lianza kwa kukutana na wafanyakazi na uongozi wa shirika.

- Kikao cha wafanyakazi wa Pemba yalikuwa kama hivi: kuna upendeleo wa nafasi za kusoma, kunaupendeleo wa ajira, kuna ubadhirifu wa mali ya umma, khofu ya wafanyakazi kufuatia kususua kwa shirika.

Kwa upande wa unguja walikuwa na wasiwasi na baadhi na wafanyakazi wenzeo kama vile: kunga umeme kwa mahoteli kinyume cha shirika, kuunga umeme kinyume cha shirika, kuna upendeleo wa nafasi za masomo, uhamisho usiofuata utarartibu, ajira hawapewi, hawatumii rasilimali upasavyo, wafanyakazi kutoridhika na uongozi, kuweko na makundi, shirika linatumia fedha nyingi, viwango vya mishahara, ununuzi wa vifaa.

 1&2. Upotevu wa fedha na sababu za usumbufu wanazopata wananchi

Hili lina fanywa na wafanyakazi wasio waaminifu. Kumekuwa na tofauti ya viwango vya ulipaji umeme. Wateja wamegawika makundi makuu mawili; wateja wakubwa na wateja wadogo taratibu zake za kupata umeme zinalingana. Kamati imechaguwa baadhi ya wateja na kuwatembelea ili kujiridhisha UNguja na Pemba.

Shirika lina baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu wakishirikiana na wateja. Kuna tofauti ya malipo kati yakazi zinazofanana. malipo yaliyopo kwenye risiti yanatofautiana na malipo halisi. malipo yanayolipwa bila ya kupewa risiti. Wateja kutumia umeme bure bila yakuwemo kwenye orodha ya shirika.

Nyumba ya Bw Mohd Dadi ameunganishiwa umeme akiwa amelipa 442, 000 wakati bi Zuhura ametozwa 1,200,000. Bwana Ussi ameunganishwa 194,000 wakati Hamadi Abdalla 597,000.

Mohd Sleiman amelipa 8,000,000 wakati kwenye risiti ni 190,000.  Amani Makungu amuenguwa 3phase amelipa 2,500,000 yeye amekiri amelipa 37,000,000. Amekiri kwamba fedha hizo amelipa kwenye account binafsi.

NMB Bank ameungiwa 3,718,000 lakini vifaa ni vingi sana baadae form yake imeonekana ni 14,000,000.

Minara ya simu: shughuli hii imepewa kampuni binafsi kuunga umeme. shirika limepoteza jumla ya …….  kwa gharama ya imnara 43. wafanya kazi wa kampuni hii ya ZAGECO ni wafanyakazi walewale wa ZECO. Hamidu Saidani ni mfanyakazi wa ZECO.

Baadhi ya wateja hawamo kwenye orodha ya shirika. Wateja 23 wanatumia bila ya kulipa hawamo kwenye orodha.

Kwa upande wa UNGUJA

Wateja 160 wakubwa na wadogo walitembelewa. Waliotembelewa ni wateja 21.

SEEROCK hoteli hii imeungwa umeme bila ya utaratibu. Umeme wa kampuni hii umeungwa na kampuni kutoka Tanzania Bara, bila ya kuhakikiwa na shirika. Shirika limeeleza kwamba lilimpiga fine mteja huyu. Fedha ya 12,132,000 ndio zilizoingia kwenye shirika.

Raskichangani imeunga umeme kwamba umeme umeungwa tokea 2002, lakini hakuna form zinazothibitisha. Shirika linapoteza kumbukumbu

Hautham Sunset beach mteja huyu hayumo katika mteja wao. nguzo 30 feki zimetumika kusambaza umeme, wameshindwa kuthibitisha namna alivyopata umeme.

The residenc kampuni ya hoteli imeungiwa umeme 2,100,000 huku nguzo 46 zimetumika.

Kendwa beach resort, hakuna barua bali form imeonekana bila yakuwa na sign wala hakuna uthibitisho wa malipo ya mteja huyu.

Shumbana Amani Karume; ilikubalika kamati haikupata uthibitisho kwamba amenunua kwa fedha zake, mteja ametumia nguzo 36 bila ya uthibitisho kuwa nguzo hizo zimeuzwa na shirika, bila ya uthibitisho wa shirika.

Leisure hoteli hakuna utaratibu wa uthibitisho wa kuungiwa mteja huyu.

Mafile ya wateja wakubwa yamekosekana, wateja 147 yamekosekana kwa vile mafile yao yamerowa kwa mvua katika ofisi kongwe, kwa vile bati ya ofisi hiyo ilikuwa inavuja.

Kampuni ya Zanzibar Data Com imekodishwa mnara na kupewa umeme bure. haijawahi kulipa tangu ilipokodishwa kwake kodi ya mnara. mbali na mnara wa mtoni pia imekodi mnara wa masingini kampuni hii hailipi umeme, lakini kampuni hii imeomba kuungiwa, la kushangaza shirika hili linatumia umeme kutoka mnara wa TVZ. kamati imeamuru kukatwa waya wake huo, baada ya siku mbili tu uliungwa tena.

Kampuni za simu; kila mnara unatakiwa ujitegee kwa huduma ya umeme. Kituo cha Zantel matemwe, hakuna maombi yoyote yaliyofanywa na zantel kupata umeme kwenye kituo hichi, bado mteja huyu maweze kulipia 28,00000 kwa kufungiwa transformer ya 3 phase.

Account za shirika Pemba: 2010 ilikuwa inaingiziwa 1,000,000 kwa siku. hakuna auditing, shirkia lina mtu mmoja wa auditing kwa unguja na pemba.

Mohd Khamis Juma (Kilindi) alilishauri shirika kuwa na udhibiti matumizi yake kwa Pemba. Menega mkuu alichoamuwa ni kumleta unguja bila ya kumpangia kazi yoyote . 

Hakuna mkataba baina ya shirika na kampuni ya ulinzi wa kituo cha umeme Tanga.

 3. Uajiri wa upendeleo

kuanzia 2008 hadi 2012: suala la uajiri linaratibiwa na wizara husika. shrika limeajiri bila ya kutowa matangazo kupitia vyombo vya habari. maombi yote kwa upande wa pemba yaliwasilishwa kwa menager pemba badala ya meneger mkuu. kukosekana mikataba. Mikataba haiko kihalali na kisheria. probation period. udanganyifu wa vyeti. kuvuka umri wa mwombaji. kuajiriwa watu wasio na sifa na kuachwa walio na sifa. Muajiriwa Tawhida ni shemegi wa manager utawala Unguja, wakati Mohd H Mohd ni mjomba wa meneger pemba. Mohd Khamis Juma alikatiliwa kusoma chuo kikuu Dodoma. Fadhila alikosa ruhusa ya kwenda kusoma degree ya kwanza.

4. mali ya shirika kuuzwa kwa kufuata taratibu

shirika linaweza kuuza mali zake kwa njia ya mnada wa hadhara au mapatano ya mojakwamoja katika soko lililowazi. kamati imebaini kwamba kuna vifaa vimeruhusiwa kuuzwa kinyume ya taratibu na sheria. jumla ya transforma 6 badala ya 1 iliyoruhusiwa. bodi ya zabuni haikushirikishwa katika mauzo haya. transformer 1 imepotea katika mazingira ya kutatanisha.

shirika linauza mali zake bila ya kutumia taratibu na sheria.

5. majenerator 32 yaliyopo mtoni

haja na sababu ya kununua majenerator imekuwa na utata. kuna hoja kwamba majenerator hayo yamenunuliwa kwa fedha za msamaha wa deni. ni tofauti na sababu za awali kwamba fedha zilizotumiwa ni kwa sababu ya kukosa umeme wa muda miezi 3.  kuna swala Vipi kumekosekana umeme Unguja?. kamati imekosa maibu kuhusiana na swala hili hadi pale itakapoundwa tume huru ya kuchunguza hili. kuna kauli kuwa ni ufadhili wa norway na sweeden ndio imetowa majenerator.

kampuni iliyioleta magenerator imesema kwa kawaida wao hawatengenezi hadi wapate order maalum. hivyo kuna shaka kubwa kwamba kukosekana umeme unguja ni hujuma maalum.

hakukuwa na mpango wowote wa kununuliwa magenerator hayo kabla. hakukuwa na bodi ya zabuni iliyokaa kuidhinnisha magenerator hayo. kazi zote badala ya kusimamiwa na shirika zimefanywa na mshauri kutoka norway.

ununuzi ulistahiki kwa njia ya zabuni. utaratibu uliotumika kikao cha maafa cha makatibu wakuu na kutafuta suluhisho. hatuo iliyofuata kutafuta wafadhili hao, manager hafahamu chochote kilichohusika kupeleka maombi kwa wafadhali. manager kampuni ya mantak waliwahi kueleza shughuli zao kwa shirika  kabla ya kutokea tatizo la umeme. bank ya PBZ $ 1,800,000 ililipa deni hilo. Shrika la umeme limehusika moja kwa moja kupatikana kwa magenerator hayo. shirika lilipa $20,700 sawa 32,000,000 kwa kampuni ya kichina kwa ulafi na uzembe wa shirika la umeme.

magenerator yote yanafanya kazi. kuyaendesha magenerator ni gharama kubwa na kulitia hasara shirika. mafuta ya kuendeshea ni tofauti na mafuta ya kawaida yanayotumika kuendesha magenerator mengine.

6. kiwango cha deni la TANESCO

historia la deni 2008  lilikuwa 1,871, 545,000 hadi kufikia 22,700,000,000. sehemu ya kwanza ni deni ambalo halina ubishi, na sehemu yapili lile lenye ubishi. 2011 asilimia baada ya kupandishwa umeme kwa asilimia 18 deni la umeme limeongezeka 22.8 bilioni. sasa hivi EWURA umepandisha gharama kwa asilimia 3.

ZECO inauwezo wa kulipia 1.6 billion uwezo wa ZECO kulipa ni 3 bilion huku makusanyo ni 3 billion kwa mwezi. kupungua uwezo kulipa ni kutokana na kupandishwa bei na EWURA.

Deni halisi la ZECO ni 62.37 bilioni, mungano italipa 39 , lililobakia lilipwe na ZECO.

HITIMISHO

1. viongozi wa bodi waliomaliza muda wao (mohd hashim) wachukuliwe hatua za kisheria kwa kuliingiza shirika

2. management ya shirika wachukuliuwe hatua za kinidhamu

3. wafanyakazi wote wa shirika waliotajwa moja kwa moja pamoja  watendaji wengine wachukuliwe hatua za kisheria

4. serikali ipige marufuku kampuni zote binafsi zinazofanya kazi za umeme

5. wafanya kazi wa kampuni wanaofanya

6. kwa kuwa magenerator imekuwa mzigo, itafutwe mbadala wake

7. kwa vile kuna dhana kumetokea hujma za kukosekana umeme unguja, serikali iunde kamati ya uchunguzi katika kipindi cha miezi 3

8.

9.

10. serikali ianzshe chombo kitakachopanga bei ya umeme Zanzibar

11. deni la tanesco ni kwa zeco ndio iliyosababisha, Zanzibar izalishe umeme wake na sio kutegemea umeme kutoka Bara

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment