Thursday 31 January 2013

[wanabidii] Neno Fupi La Usiku Huu; Hakuna Siri...!

Ndugu zangu,

Wanadamu tunahangaika sana kutaka kutunza siri. Niwaambie, katika maisha hakuna siri. Na kama zipo, ni chache sana.

Inasemwa, kuwa siri ni ya mmoja. Lakini ona, hata mmoja huyo anaweza kuweweseka na siri ya moyoni mwake. Na mara ile atakapomnon'oneza mwenzake, basi, kuna unafuu atauona.

Ukweli ni huu, kuwa kwenye maisha haya tunayoishi, siri ni chache sana. Ndio, ni wanadamu wachache sana wenye siri na wakazitunza. Hivyo, wanadamu tunapoteza muda na nguvu zetu nyingi sana katika kujifanya tunatunza siri. Ni kazi bure.

Duniani kuna wenye kusema wasiyomaanisha, na kuna wasiomaanisha wanayosema. Haya ni mawili tofauti. Na wenye kuyatenda wanadhani kuna wanachoficha. Kuwa wana siri. Hapana, wanajidanganya. Hivyo, ni waongo tu.

Mara nyingi nakutana na watu wenye kutamka; " E bwana ee, jambo nililokueleza ni siri, usimwambie mtu!" Na jambo hilo hilo unaweza kuambiwa na mwingine, kwa staili hiyo hiyo, kuwa ni la siri!

Wanachoshindwa wengi kutofautisha ni hiki; muhimu na siri. Lililo la muhimu, na pengine nyeti, si lazima liwe la siri.

Na hilo ni Neno Fupi la Usiku Huu.

Maggid Mjengwa,

Iringa.
0788 111 765
http://mjengwablog.co.tz

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment