Thursday 31 January 2013

Re: [wanabidii] Facebook newsfeed post by: Hamisi Kigwangalla: Hoja Binafsi ya Kuongeza Ajira kwa Vijana na Kukuza Uchumi


Inasikitisha tu hasa pale unapofika kuna ardhi na mabonde mazuri yanayozalisha, barabara ya lami au inayopiyika ipo ila wao wapo kukaa vijiweni walimao ni wazee. Jioni au usiku kuiba hayo mazao ya vizee na kuyasafirisha ktk mafuso. Kupanda minazi usiku kuiba nazi, machungwa, mananasi. Ni hao watoao shinikizo kwa bibi na babu, wazazi wao kuuza ardhi ili wapate mtaji. Unakuta ardhi imekwisha kuuzwa na mtaji umetumika katika kucheza kamali na kunywa pombe anarudi kijiweni. Kwa sasa ardhi ya Rufiji-Mtwara, Bunju-Bagamoyo-Makurunge-Chalize imeuzwa kichizi ni milingoti tu ionyeshayo mali za watu unaona. Kwa vile kunakuja uwekezaji na barabara za lami zinajengwa ardhi wameuza hovyo wenyewe baadae watachoma moto hizo nyumba za wafanya biashara na viwanda vya wawekezaji kusema wanaonewa.

Baada ya mauzo ya ardhi kunakuwa na mkesha wa mchiriku wa mtoto kutoga masikio!! Hata wakielekezwa kuwa wasiuze hovyo waitumie kuzalisha ili wauzie wafanyakazi na viwanda mazao hawasikii. Anakuambia haikuhusu au nauza nifanye mipango yangu mingine baadae ndio hao wa maandamano na kujenga barabarani kwenye road reserve. Wakipewa ardhi mabwepande etc-wanauza wanashuka mambondeni. Usiuze kariakoo uwe mbia katika ujenzi ujao-ni wachache wamekubali hilo. Wengi wameuza nyumba Kariakoo lakini billioni biyo moja ya nyumba ya vyumba 6 wamegawana na zimeishia. Vijana wameomba power tiller ili walime, wanapewa pamoja na mbegu na vifaa vya kumwagilia dawa mazao lakini unakwenda unakuta story. Ekari 5 za shamba na bustani wanapewa na fedha za kuanzia kilimo na training ya ujasiriamali NGO inatoa unarudi kufuatilia maendeleo unakuta story mwaka nenda rudi mifano mingi TZ ipo. Hata vikundi wanavyoanzisha wenyewe mfano vya bajaji na Pikipiki wanachanga ili baadae kila mmoja awe na kifaa hicho-unakuta vinakufa kutokana na kutapeliana. Mtu anakimbia na milioni 2-4 etc na kupotelea kumbe akikusanya kama mweka hazina hapeleki benki. Vya upatu ni hivyo. Vya VICOBA na FINCA- unakuta wanakikundi waliomdhamini mwezao daima kulipa madeni ya wenzao wanaotoroka baada ya kuchukua mkopo wa kudhaminiwa. Juhudi za GVT kuwakwamua na mashirika yanayowasaidia zinakwama. Inabakia kuwa-kila mtu anajifanyia binafsi pekepeke na kama hana mtaji na vifaa na mali ya kuweka dhamana bank-tatizo. Hii ndio Tanzaniana ya mameno mengi. Akina Mh Mengi wanajitahidi lakini fanya evaluation ya vikundi saidiwa utakuta 80% mikogoro na kumegeka.

Ukiwa Ulaya na Marekani, etc unaona hata kijana wa Masters, PhD anafagia barabara, kuosha vyombo cafeteria, kufagia bweni, kuendesha taxi, town bus, kugawa barua za posta na magazeti nyumba hadi nyumba kwa baiskeli kulipa ada ya shule au apate upungufu wa ada au chumba cha kulala chuoni kama akiwa anaosha vyombo cafeteria au kufagia bweni, kuwa maktaba. Hapa TZ bora azurure kuliko kufanya ajira za namna hii. Ego zetu zinatumaliza. Elimu bure zamani inachangiwa na donors pia miradi ya maji ya bure na uzoaji taka na serikali kutoa ajira kwa kila amalizae secondary hadi University. Wenzetu hata PhD anasaka kazi na huko wameendelea. Wana viwanda, mataasisi etc. Jee sisi wa shule za msingi kamaliza hata kusoma hajui na kujituma hataki anataka 'serikali ituletee.' Serikali itufanyie, itusafishie, ituondolee taka hizi (tulizotupa wenyewe) zinazoziba mitaro halafu maji yanajaa majumbani mwetu!!'


--- On Thu, 31/1/13, hkigwangalla@gmail.com <hkigwangalla@gmail.com> wrote:

From: hkigwangalla@gmail.com <hkigwangalla@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Facebook newsfeed post by: Hamisi Kigwangalla: Hoja Binafsi ya Kuongeza Ajira kwa Vijana na Kukuza Uchumi
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, 31 January, 2013, 21:55

Hamisi Kigwangalla wrote:

Kesho asubuhi nimealikwa TBC1 kuanzia saa moja asubuhi kwenye kipindi cha jambo Tanzania kuzungumzia Hoja yangu binafsi ya kuongeza ajira kwa vijana na kukuza uchumi. Hoja ambayo natarajia kuiwasilisha bungeni kesho ijumaa baada ya kipindi cha maswali na majibu. Karibu utoe maoni yako ili usaidie kunipa mawazo ya kuboresha mjadala, pia fuatilia ujue nini kitaamuliwa na kuazimiwa na Bunge letu tukufu?!
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment