Wednesday 30 January 2013

[Wanabidii Place] New comment on [wanabidii] Re: Incompetence Responsible for Fault....

Antipas Massawe has left a new comment on your post "[wanabidii] Re: Incompetence Responsible for Fault...":

Ndugu Tony na Ezekiel,

Ukweli ni kwamba kasoro kubwa za elimu walizo nazo wasomi wengi wa kizalendo ni zile zinazowezesha mtu kupata ajira na kuzitenda na sio kubuni, kuanzisha, kuendeleza na kusimamia biashara zinazoendana na elimu zao.

Pamoja na kwamba mtu kasomea elimu ya kilimo na kufaulu katika kiwango cha hali ya juu mno, hata kufikia ngazi ya udaktari bado mtu huyu anashindwa kabisa kubuni biashara ya kilimo kuendeleza ardhi kubwa na nzuri zenye rutaba kama vile bonde la mto Rufiji au mto Ruvu linalomzunguka.

Anashindwa kwa vile elimu yake sio timilifu, bado alihitaji kupata ile elimu ya biashara itakayomwezesha kubuni, kuanzisha, kuendeleza na kusimamisha mashamba ya kisasa ya kilimo cha biashara ndani ya yale mazingara ya ushindani yanayomzunguka.

Elimu ya uchumi, uhasibu, biashara na usimamizi wa biashara ni muhimu kwa wanataaluma wa aina zote ili kuwawezesha kubuni, kuanzisha, kuendeleza na kusimamia biashara zenye tija kwenye fani zao.

Elimu ya falsafa, siasa ya uchumi na maendeleo ni muhimu pia kuwawezesha wanataaluma wa aina zote kuelewa dunia inayowazunguka inafanya kazi vipi na ni kwa namna inabidi wajipange ndani ya dunia hiyo katika kubuni, kujianzishia, kuendeleza na kusimamia biashara ndani ya taaluma zao ili nao waweze kufanikiwa na kuendelea kuwepo na kukua kibiashara kwa kutegemea taaluma zao ndani ya dunia inayowazunguka.

Kijana wa Australia au Canada anasoma kujipatia shahada ya kwanza ya jiolojia, anaongezea ingine ya biashara au uhasibu kwenye biashara za tafiti ya jiologia na nyingine ya usimamisi wa biashara ya tafiti za jiolojia halafu anajitafutia mtaji mbegu unaomwezesha kujianzishia kampuni ya utafutaji na uuzaji au uchimbaji wa madini ndani ya mataifa yanayoendelea. Anakuja hapa Tanzania kwa mfano na kwa kutumia geologists wetu watafuta ajira anafanikiwa kupata migodi na kuiendeleza kidogo kabla ya kuiuza na kujipatia mamilioni ya dola za kimarekani mbele ya geologists wetu fukara waliomsaidia.
Ndio maana nimesema elimu inayotolewa vyuoni ni lazima iboreshwe ili iweze kuzaa wabunifu wa biashara na wenye uwezo wa kuziendeleza na kuzisimamia na sio tu watafuta ajira.
Ukosefu wa elimu ya biashara miongoni mwa maofisa huko serikalini ndiyo ndiko kunakosababisha wao kupokea rushwa ya dola million moja kwa mfano ili kupitisha mkataba na wageni utakaolisababishia taifa hasa ya zaidi ya $ bilioni moja au kupitisha mradi mbada usiofaa na kuuacha ule usofaa kutokana na kutokuwa na uwezo wa kufanya upembuzi yakinifu ili kubaini faidi halisi za miradi ypote mbadala.
Nakubali kabisa maamuzi kuhusu matumizi mbadala ya kutumia gesi ya Mtwara kuzalisha umeme Dar es Salaamu au Mtwara ilibidi yahusishe wataalamu kutoka wizara zote na taasisi zote za maendeleo na biashara au kampuni moja au mbili bingwa kimataifa kwenye upembuzi yakinifu uliohitajika kubaini manufaa ya miradi mbada ya uzalishaji umeme Dar es Salaam au Mtwara kwa vipindi vyote vya uhai wa miradi hiyo ili kuwezesha kuchagua mbadala wenye manufaa makubwa zaidi kwa taifa.




Posted by Antipas Massawe to Wanabidii Place at 30 January 2013 08:10

0 comments:

Post a Comment