Thursday 31 January 2013

RE: [wanabidii] Kwa nini serikali tatu?


Issa,
 
Nadhani uliupata ujumbe kwamba jina la nchi halitawaliwi na vitu vilivyodhani vinatawala. Pili, ni ukweli kuwa mlitumia longolongo kwenye hoja ile; ndiyo maana nikakwambia umfikishie ujumbe mhusika lakini naona unakwepa kuonekana mbaya kwake. Heri ya urafiki kuliko ukweli.
 
Kuhusu tafsiri yako ya iwapo Zanzibar ni kama nchi gani au sehemu gani hapa duniani umedai kwamba Zanzibar siku zote ni sovereign state. Hakuna kitu kama hiki. Zanzibar ilikoma kuwa sovereign state mnamo Aprili 26, 1964. Zanzibar haina sovereignty tangu siku hiyo na hali kadhalika Tanganyika na ndicho Karume na Nyerere walichowaambia wenzao kwenye kikao cha OAU cha mwaka 1964 mjini Cairo. Kasome hotuba. Ngoja nirudie: Zanzibar is not a sovereign state.
 
Kuhusu madai uliyozua hapa: 
"Kaka Matinyi, hili ndilo tatizo lenu ndugu zetu wa Bara, kwani mnapoizungumzia Zanzibar siku zote mnaiona kama ni jimbo la Bara na ndio maana mnatoa hii mifano ya Sudan. Yes, we are just one million na kuwa hata Mwanza inatupita, lakini hili halitufanyi sisi tukawa jimbo kama Mwanza."
 
Hayo ni maoni yako na hayanihusu na sidhani kama ni busara kuitana "ninyi" na "sisi". Huu ubaguzi ni tatizo kubwa na haufai kuwepo kwenye nchi moja kama TANZANIA na yoyote ile. Ni ulimbukeni na hapa Marekani sijawahi kusikia watu wakiitana hivyo.
 
Kuhusu jina:
Kuna somo refu sana la majina ya nchi na zipo zilizoungana kijamii mathalani, Indonesia, lakini si kwa muungano kama wetu. Ipo Bara Hindi na hadithi zake za jina. Ipo iliyokuwa Yugoslavia, n.k. Jambo moja la msingi la kufahamu ni kwamba si lazima hapa duniani kuwepo na mfano kama wa TANZANI na matukio kama yetu ndio pointi ieleweke kwa mtazamo wako. Jina la Tanzania ni jina llilitokana na MATASHI yetu tu na UREMBO wa jina lakini si suala la kisheria na wala si suala la mahitaji ya kimataifa, kidiplomasia, n.k. Jina lenye nguvu za kisheria ni lile nililokufafanulia na kukutolea mifano lakini cha ajabu hukuelewa.
 
Narudia tena: Jina Tanzania halina nguvu za kisheria na ni suala la matashi na urembo tu. Jina hili lilianza kutumika baada ya kupatikana Oktoba 1964 huku tukiwa tumedumu kwa miezi sita bila jina hili lakini tukiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hakukuwa na tatizo na hatukuombwa na mtu yeyote kwamba tutafute jina moja na wala hatukuhitajika kisheria kufanya hivyo. Kwa njia hiyo hiyo, tunaweza kulibakiza hilo jina na kwa kuwa hakuna nguvu za kisheria za uundaji majina ya namna hii, hakuna mahakama yoyote duniani itakayoamua vinginevyo. Zaidi sana swali moja litakuwa hivi: Nani aliyetunga jina hilo? Jibu litakuwa ni bwana mmoja aliyekuwa na uraia wa Tanganyika kabla ya Muungano. Swali la pili litakuwa hivi: Zanzibar inapoteza nini katika jina lake iwapo Bara itajiita Tanzania. Jibu unalijua.
 
HITIMISHO.
Mimi nitapigania jina TANZANIA libakie hivyo hivyo iwapo watatokea vichaa wa kuuvunja Muungano. Binafsi yangu sikubaliani na suala la kuuvunja Muungano hata kama una usumbufu na maneno na malalamiko ya kitoto. Muungano udumu tu hata kwa mbinde! Vizazi vijavyo vikijua thamani yake na umaana wa TAIFA vitautunza.
 
Matinyi.

Date: Wed, 30 Jan 2013 22:29:56 -0800
From: saidissa100@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Kwa nini serikali tatu?
To: wanabidii@googlegroups.com; matinyi@hotmail.com

Dear Kaka Matinyi,
Samahani,  kazi uliyonipa imenishinda, kwasababu uliyoyaeleza sio ya kweli kutokana na kuwa umechanganyisha mambo yasiofanana.
Huwezi hata siku moja kulinganisha Sudan na Tanzania. Huwezi pia kulinganisha Korea na Tanzania na wala huwezi kulinganisha Germany na Tanzania yetu tulivyo.
Kaka Matinyi, usijifanye hujui nini maana ya neno 'Tanzania'. Mifano yako yote uliyoitoa haifai kulinganishwa na nchi yetu ya Tanzania.
Kama Mbeya ikijitenga kutoka Jamhuri ya Tanganyika, bado Tanganyika itajiita Tanganyika. Hata pia kama Arusha, Dodoma, etc zote zikitoka kutoka Jamhuri ya Tanganyika na zikajiita kivyao, bado Tanganyika itabakia Tanganyika hata kama itabakia na region moja tu. Lakini, Zanzibar ikitoka kutoka Jamhuri ya Tanzania kinachobakia sio tena Jamhuri ya Tanzania. Itabidi mtafute jina jengine, else tutakutana The Hague!
Hivyo, Kaka Matinyi, shemeji iwe ushamwacha ( God forbids) bado utamuachia aendelee kujiita Mrs Matinyi?
Nieleze nchi gani mbili au zaidi zilizoungana na baada ya Muungano kuvunjika moja katika hizo ikaendelea na jina la Muungano? Hapa nataka nchi kamili kama Zanzibar na Tanganyika zilivyokuwa, na sio nchi zilizotengana kwa vita au kutoa mfano wa Sudan ya Kusini na Kazkazini.
Sudan ya Kusini was never a fully fledged country by its own. Sudan ya Kusini ilikuwa ni kama Mwanza au Mbeya tu na kwahivyo kutoka kwake hakubadilishi jina la Sudan. In fact, South Sudan seceded on 9th July 2011 and became an independent state - unlike Zanzibar which has always been a sovereign State. Vipi kujitenga kwa South Sudan kutaifanya Sudan isiwe Sudan? Kwani South Sudan na North Sudan waliungana kama Zanzibar ilivyoungana na Tanganyika na wakawa kwenye Muungano uitwao SUDAN? In other words, kwani neno 'Sudan' ni Muungano wa nchi mbili au ni jina la nchi mmoja tu?
Kaka Matinyi, hivyo unalinganisha South Korea na North Korea na Tanzania ilivyo? Ni wapi na wapi! We are miles apart!
Sasa kurejeana kwa GDR na FRG kuwe na tatizo la nini? Kwani hizi hazikuwa nchi moja kabla ya vita? Zanzibar na Tanganyika kwani zilikuwa nchi moja kabla?
Kaka Matinyi, hili ndilo tatizo lenu ndugu zetu wa Bara, kwani mnapoizungumzia Zanzibar siku zote mnaiona kama ni jimbo la Bara na ndio maana mnatoa hii mifano ya Sudan. Yes, we are just one million na kuwa hata Mwanza inatupita, lakini hili halitufanyi sisi tukawa jimbo kama Mwanza.
Kama Tanzania ingelikuwa ni Muungano wa Zanzibar, Tanganyika, Kenya, Uganda, etc na baadae Zanzibar ikatoka, basi still Muungano ungeliweza kuendelea kutumia jina la Tanzania, lakini in case of 2 countries only, ikitoka moja jina linakuwa lishakufa!
Kaka Matinyi, usisahau ile equation maarufu tuliofundishwa - yaani: 1+1 = Tanzania. Sasa kama ikiwa hivyo ni sawa, je, 1+0 = ???? Still
jawabu litakuwa Tanzania? Basi tutakuwa ni vichaa!
With Zanzibar gone, there will NEVER be a Republic of Tanzania again! May be a Republic of Tangania or Danganyia!
 
...bin Issa.
 
From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, January 30, 2013 12:21:34 PM
Subject: RE: [wanabidii] Kwa nini serikali tatu?

Issa,
 
Nadhani huko kwenye blogu yenu ya Zanzibar ni Kwetu mlidanganyana. Naomba unifikishie jibu langu kwa mhusika na blogu.
 
Mambo ni hivi:
1. Kuna jina la nchi la kawaida na jina rasmi la nchi, mfano, "Malawi" ni jina la kawaida lakini "Republic of Malawi" ni jina rasmi na linalotambuliwa katika sheria za kimataifa. Majina rasmi ndiyo hutumika kwenye utambulisho na mikataba ya kimataifa. Mfano mwingine ni America na United States of America au Saudia (Saudi Arabia pia) na Kingdom of Saudi Arabia.
 
2. Baadhi ya nchi kutokana na historia zao zina majina yenye umaalumu fulani, mathalani, North Korea huitwa kwa jina rasmi Democratic People's Republic of Korea, wakati South Korea huitwa kwa jina rasmi - Republic of Korea. Hakuna mvurugano wowote hapo.
 
3. Kwa nchi zilizokuwa za muungano na baadaye zikavunjika, kanuni ya msingi ni kubadilisha jina rasmi na si lazima kubadili jina la kawaida. Mfano, Sudan (Republic of Sudan) imebakia hivyo hivyo bila kubadili kitu.  Mfano wa Abdul Nasser na ile UAR (siyo UAE kama mlivyoandika) ni suala la siasa na uzalendo wa Wamisri na si tatizo la jina kama mnavyodhani. Suala lilikuwa kuhusu jina rasmi na isingewezekana kuitwa hivyo wakati haikuwa tena jamhuri ya muungano. Hakina kichaa kama hiki.
 
4. Suala la USSR nadhani hapa kuna uongo wa mchana kweupe. Isingewezekana nchi hii iendelee kuitwa hivyo baada ya kuvunjika kwa kuwa maana yake ilikuwa Union of Soviet Socialist Republics ambazo zilikuwa 15 na baadaye ikabakia MOJA tu. Putin siyo mpuuzi kiasi hicho kwamba ashindwe kuelewa maana ya jina la nchi. Jina Russia ni la iliyokuwa jamhuri mama. Hapa mmedanganyana. Pia nchi hii iliitwa kwa kifupi (siyo jina rasmi) kama Soviet Union na kamwe wasingeendelea na jina hili kwa kuwa maana haikuwepo.
 
5. Tanzania ni jina la kawaida na United Republic of Tanzania ni jina rasmi. Muungano ukivunjika hatuwezi kuendelea kutumia jina hili rasmi na badala yake tutachagua moja kati ya haya matatu:
(i) Republic of Tanzania (ii) Republic of Tanganyika (iii) Jina jingine lolote tutakalopenda.
 
6. Hakuna sheria wala taratibu zinazotuzuia kuendelea kulitumia jina TANZANIA na wala hakuna mgongano wowote, iwe kimaslahi au kidiplomasia kama mlivyodai au vyovyote vile. Ndiyo maana leo German Democratic Republic iliporudiana na German Federal Republic hakukuwa na tatizo kwenye kuendelea na jina la "Bundesrepublik Deutschland" ambalo kwa Kiingereza ni Federal Republic of German pia.
 
7. Sudan haikubadilisha jina hata baada ya Sudan nyingine kuzaliwa; na pia Korea Kusini imeendelea kuitwa Jamhuri ya Korea licha ya kuwa kuna Korea nyingine.
 
Tafadhali, mfikishie ujumbe mwandishi wa hoja hii iliyopotosha. Mwambie kama hajaridhika na maelezo haya aseme nimpe marefu zaidi na mifano mingi zaidi. 
 
Mobhare Matinyi.
Date: Wed, 30 Jan 2013 00:57:20 -0800
From: saidissa100@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Kwa nini serikali tatu?
To: wanabidii@googlegroups.com; lingsadam@yahoo.co.uk

>Natamani hata baada ya kutimia mgawanyiko unaopigiwa chapuo, upande wa bara ubaki kuitwa TANZANIA tu,
 
Adam, kama kutamani basi wanatamani wengi na sio peke yako, lakini kwa bahati mbaya dunia ya leo haiendi kwa matamanio yetu.
Kuhusu kutumia jina la Tanzania naona Wazanzibari washalijibu hilo suala na labda nikudokeze kidogo hapa chini kutokana na barua ya wazi aliyopelekewa ndugu yetu mmoja.
"....sote tunajua kuwa jina la Tanzania ni zuri na tunalipenda sana. Itakuwa vigumu na kinyume kwenu nyinyi kujiita tena Tanganyika, lakini Muungano ukivunjika sio nyinyi wala sio sisi watakaoweza kulitumia jina la Tanzania isipokuwa kwenye mabuku ya historia tu. Hapatokuwa  na uwezekano wa watu wa Bara kuamua kuendelea kujiita Watanzania. Wabara kuamua kuendelea kujiita Watanzania - in a diplomatic lingo that would amount to willfully fooling the world....".

Jamal Abdel Nasser alitamani (wakati  umoja wa Egypt na Syria unavunjika ile 1961) ili Egypt ibakie kuitwa United Arab Republic (UAE) - due to his strong sentiments of collective Pan-Arab nationalism, lakini haikuwezekana na ikabidi iendelee kuitwa Egypt.

Rais wa Urusi Bw. Vladimir Putin inasemekana wakati USSR inasambaratika na akiwa yeye kama boss wa KGB alitamani (kama unavyotamani wewe), kuwa Urusi peke yake ichukue jina la USSR, lakini haikuwezekana na ikabidi jina la USSR liende na maji.

Ushauri wetu ni kuwa, tumieni jina lile lile lenu la Tanganyika kwani litaleta maana zaidi, lakini kama hamtolikubali tena jina lenu la zamani ... na mtataka kushikilia kuitwa Tanzania, basi labda baada ya Muungano kuvunjika mjiite TANGANIA which is very close to our beautiful name of Tanzania!
The name TANGANIA encompasses Tanzania, Tanganyika and even Tanga. What a great and a beautiful name this will be !"
 
 

From: "lingsadam@yahoo.co.uk" <lingsadam@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, January 29, 2013 1:05:00 PM
Subject: RE: [wanabidii] Kwa nini serikali tatu?

Hakika Bariki. Tanzania moja. Nata,ani hata baada ya kutimia mgawanyiko unaopigiwa chapuo, upande wa bara ubaki kuitwa TANZANIA tu, sio Tanganyika. Kiukweli; ni ama tunauhitaji muungano au hatuutaki. Wazo la serikali moja lililomnyongelea mbali malecela enzi za uongozi wa rais Mwinyi, lilikuwa wazo bora! But wishes are never horses!
-----Original message-----
From: Bariki Mwasaga
Sent:  29/01/2013, 18:57
To: wanabidii
Subject: Re: [wanabidii] Kwa nini serikali tatu?



Mimi ingekuwa ni uamuzi wangu, tungebaki na jitu linaitwa Tanzania
tu....kwangu ni bora basi tukawa na "lander" kama huko Ujerumani kuliko
kuwa na Serikali sijui mbili ama tatu. Lakini kwa sababu haya
yanashindikana basi Serikali 3 ndiyo mbadala wa ninachopendezewa nacho


2013/1/29 Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>

>  Baraka,
>
> Sihitaji kupiga kampeni yoyote lakini ni lazima watu wazima wenye akili
> timamu tujadiliane kwa kuangalia uhalisia wa mambo na si ushabiki,
> kuchanganya mambo ama hata unafiki. Ndiyo maana nimesema, kama watu
> hamuutaki uvunjeni tu huu muungano badala ya kuota ndoto za miujiza. Porojo
> za muungano wa mkataba za Karume na Seif ni mfano mmoja wa uongo na unafiki
> kwa kuwa hakuna kitu kama hicho bali wanachokisema wao ni kuuvunja na kisha
> kubakia na ujanjaujanja. Hali kadhalika mawazo ya Chadema kwamba tuwe na
> serikali ya muungano nusu-mkate hayawezekani. Hakuna serikali nusu-mkate
> duniani kwa kuwa serikali ni chombo kamili chenye mamlaka ndani na nje na
> hasa pale inapofikia kwenye masuala yanayotegemea sovereignty.
>
> Malalamiko kwamba eti Zanzibar ina wimbo, bendera, na vidudu vingine, ni
> malalamiko kama ya watoto kulia vidue vya kuchezea. Mbona kila jimbo
> (wanaita state) la Marekani lina vitu hivyo na zaidi? Mbona kila jimbo
> (wanaita country) la Ujerumani lina vitu hivyo na zaidi? Mbona kila jimbo
> (wanaita nchi pia, nchi ndani ya dola moja) la Uingereza lina vitu hivyo na
> zaidi? Tukishakuwa na vya Tanganyika tutapata nini cha zaidi?
>
> Wazo kwamba tuwe na serikali tatu lakini yenye serikali ya muungano ndogo
> (dhaifu) linazua mambo mengi ambayo nashangaa kwa nini watu hawajiulizi
> kwayo. Mfano. Tukiwa na serikali ya muungano yenye wizara nne au tano, au
> sita, yale mambo yasiyokuwa ya muungano yatabakia kwenye serikali za
> Zanzibar na Tanganyika, mathalani suala la mazingira, elimu, maji, nishati,
> madini, ujenzi, n.k. Je, itakuwaje pale tutakapohitajika kusaini
> makubaliano ya kimataifa? Waziri yupi atasaini na kwa mamlaka yapi kisheria
> (za kimataifa)?
>
> Ngoja niweke kirahisi zaidi. Kwenye sheria ya kimataifa itakayotambulika
> ni sovereign state ya TANZANIA. Kama hii Tanzania haina usimamizi wa
> masuala, tuseme ya mazingira, ni nani atayesimamia mazungumzo na utiaji
> saini wa masuala ya mazingira huko duniani wakati Tanganyika na Zanzibar
> hazina sovereignty?
>
> Chadema walisema kwamba tushirikiane kwenye diplomasia lakini kwenye
> ushirikiano wa kimataifa kila mtu aende kivyake. Hebu nieleze,
> inawezekanaje? Eleza kwa ufahamu wako.
>
> Aidha, ina maana kwamba kwenye jumuiya kama SADC au AU sisi tutakuwa na
> Tanganyika na Zanzibar lakini kwenye eti "diplomasia" tutakuwa pamoja - *
> kivipi?* Sovereignty iko kwa nani? Sera ya nje iko kwa nani? Diplomasia
> ni mbinu ya utekelezaji wa siasa za kimataifa, sasa mnawezaje kuwa pamoja
> kwenye diplomasia lakini kwenye ushirikiano wa nje hamko pamoja? Hii ni
> alinacha!
>
> Kushindwa kutambua huu mvurugano ni dalili kwamba Watanzania hatujui
> tunadajili nini na ndiyo maana ile blogu ya Kwetu ni Zanzibar iliona kwamba
> walichosema Chadema na walichosema CUF na Seif na Karume ni sawa wakati
> ukiviangalia ni vitu viwili tofauti kabisa.
>
> Lakini pia watu msibweteke na suala la IDADI YA SERIKALI. Jambo la msingi
> ni ubora wa mfumo kabla ya kuangalia idadi ya serikali - idadi ya serikali
> ni matokeo ya mfumo na kanuni (principles), pengine na malengo ya kitaifa.
>
> Matinyi.
>  ------------------------------
> Date: Tue, 29 Jan 2013 18:22:25 +0300
> Subject: Re: [wanabidii] Kwa nini serikali tatu?
> From: bmwasaga@gmail.com
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
> hahah Matinyi piga kampeni mawazo yako yakubalike kwa Watanzania walio
> wengi kinyume na hapo hakuna mabadiliko
>
>
> 2013/1/29 <msiwahili@gmail.com>
>
> **
> Matinyi,
> Ni serikali moja tu au Zanzibar waachiwe waende zao kwa amani.
>
> Mwamba
> Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania
> ------------------------------
> *From: *matinyi@hotmail.com <matinyi@hotmail.com>
> *Sender: *wanabidii@googlegroups.com
> *Date: *Tue, 29 Jan 2013 10:14:35 -0500
> *To: *<wanabidii@googlegroups.com>
> *ReplyTo: *wanabidii@googlegroups.com
> *Subject: *Re: [wanabidii] Kwa nini serikali tatu?
>
> Chadema is totally misled in this. Sad.
>
>
>
> T-Mobile. America's First Nationwide 4G Network
>
> ----- Reply message -----
> From: "Emmanuel Muganda" <emuganda@gmail.com>
> To: <wanabidii@googlegroups.com>
> Subject: [wanabidii] Kwa nini serikali tatu?
> Date: Tue, Jan 29, 2013 10:01 am
>
>
> Lakini, bara tunahitaji serikali ya nini? Kikwete ni rais wetu na amiri
> jeshi mkuu, kwa nini mnataka kutuongezea viongozi?
> Mimi naunga mkono Chadema lakini sijaona mantiki ya kuwa na serikali tatu.
> Ni matumizi juu ya matumizi na matatizo juu ya matatizo tu. Zanzibar hawana
> jeshi na hatuwezi kuwa kwenye mizani sawa, a million people versus 45
> million.
> em
>
> 2013/1/29 Said Issa <saidissa100@yahoo.com>
>
> > >Mbowe na wafuasi wa CHADEMA wako sahihi kusema ziwepo serikali tatuMbowe
> > na wafuasi wa CHADEMA wako sahihi kusema ziwepo serikali tatu
> >
> > Yes!  Now you are talking sense brother!
> > Sasa sio tuseme tu, lakini na nyinyi huko Bara piganeni mpate hio
> serikali
> > yenu ya Tanganyika.
> > Waungeni mkono hao Chadema, kwani wao wanaonesha kuwa they are very
> > practical na sio wa midomo mitupu kama wengine.
> >
> > >Je vitambulisho vya Tanzania vitakuwa vya aina ngapi?
> >
> > Sijui hapa Nd. Mngonge unazungumzia vitambulisho gani, lakini kama ni
> > passports, basi passports zote zitakuwa kama zilivyo hivi sasa isipokuwa
> > kwa nyuma zitaandikwa :
> > THE GOVERNMENT OF TANGANYIKA or THE GOVERNMENT OF ZANZIBAR.
> > Kwahivyo, mtu ukimpa passport yako atajua mara moja kuwa wewe ni
> Mtanzania
> > lakini unatoka either Tanganyika au Zanzibar. Hili naona Chadema
> wakichukua
> > nchi 2015 litakuwa
> > ni jambo rahisi sana kukubaliana nao, kwasababu muelekeo mzuri wanao
> > tayari.
> > Tukeshakubaliana hilo na baadae kila mtu akawa na sarafu yake na
> wakilishi
> > wake wa nje (diplomats), basi hatuna tena cha kugombania. Itakayobakia
> > itakuwa ni kuchapa kazi tu!
> >
> > ...bin Issa.
> >
> > N.B.
> > I hope Matinyi will not see this msg.
> > Kama Admin utaweza kufanya yeye asiipate msg hii nitashukuru sana,
> > kwasababu sina mood ya ugomvi kwa leo.
> >
> >  ------------------------------
> > *From:* mngonge <mngonge@gmail.com>
> > *To:* wanabidii@googlegroups.com
> > *Sent:* Tuesday, January 29, 2013 3:42:17 AM
> > *Subject:* Re: [wanabidii] Kwa nini serikali tatu?
> >
> > Nafikiri sababu ya msingi wanayosimamia CHADEMA ni pale Mbowe
> > aliponukuliwa akisema "tayari wakitoa uhuru wa Zanzibar kuwa na Rais,
> > bendera na wimbo wao wa taifa"
> > Ukiangalia kwa makini uwepo wa serikali tatu unaletwa zaidi na kitendo
> > cha wazanzibar kutaka kuwa na nchi yao inayojitegemea. Kama hilo
> > lisingekuwepo sidhani kama tungekuwa na mjadala unaohusu muungano.
> > Wote tungependa tuwe na serikali moja ya kitaifa na hivyo kila kitu
> > kuwa sawa kati ya bara na visiwani.
> >
> > Mbowe na wafuasi wa CHADEMA wako sahihi kusema ziwepo serikali tatu (
> > Tanganyika au Tanzania bara, Zanzibar au Tanzania Visiwani na Serikali
> > ya Muungano). Kama Zanzibar wanapenda kutambuliwa kama wazanzibar
> > chini ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iweje Tanganyika isiendelee
> > kutambuliwa kama Tanganyika na watanganyika wake? Nafikiri jibu liko
> > wazi, ni ama kuwa na serikali moja au tatu hiki kiini macho cha kuwa
> > na serikali mbili ambapo tuna serikali ya muungano na serikali ya
> > Zanzibar kitaendelea mpaka lini? Je vitambulisho vya Tanzania vitakuwa
> > vya aina ngapi?
> >
> > 2013/1/29 Ntunaguzi Ntiyakunze <ntunaguzin96@gmail.com>:
> > > Wanabidii,
> > >
> > > Nanukuu kauli moja ya mwenyekiti wa CHADEMA katika kikao cha Kamati Kuu
> > (CC)
> > > juzi ambapo agenda moja kubwa ilikuwa ni kupitisha mpango mkakati wa
> > mwaka
> > > 2013 ili kushinda chaguzi zote kuanzia serikali za vitongoji, vijiji na
> > > mitaa mwaka 2014 na Uchaguzi Mkuu 2015.
> > >
> > >
> > > Katika suala zima la Muungano, Mbowe alisema uwepo wa serikali tatu
> > > hauepukiki kwa kuwa tayari Tanzania Visiwani wameshakuwa na serikali
> yao
> > > hivyo ni jukumu la Watanzania Bara kupata serikali ya Tanganyika na
> kisha
> > > kuwepo na serikali ndogo ya Muungano. Alisema serikali tatu inawezekana
> > > ikiwa viongozi wataacha unafiki wa kusema muungano utavunjika huku
> tayari
> > > wakitoa uhuru wa Zanzibar kuwa na Rais, bendera na wimbo wao ya taifa.
> > > Tunawaunga mkono wenzetu Wazanzibar katika kupigania uhuru kamili na
> kwa
> > > sasa sisi ndio tunaoonekana wa ajabu kushindwa kuuliza serikali ya
> > > Tanganyika," alisema.
> > > Swali;
> > > Je kuna sababu za msingi ambazo CHADEMA wanazo mpaka kufikia hatua ya
> > > kuzitaka serikali tatu tofauti na ilivyo hivi sasa?
> > >
> > > --

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment