Thursday 31 January 2013

Re: [wanabidii] Serikali iweke bayana uamuzi wa gesi izalishe umeme Dar es Salaam na si Mtwara

mtwara pia utazalishwa umeme utakaoenda songea kuungana na umeme wa grid


On 1/31/13, Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
> Serikali iweke bayana taratibu zilizofanikisha uamuzi gesi ya Mtwara
> izalishe umeme Dar es Salaam badala Mtwara
> Dkt A. Massawe/massaweantipas@hotmail.com
>
> Pamoja na habari njema za maelewano kupatikana baina ya Serikali na
> wenyeji wa Mtwara kuhusiana na swala la gesi asilia ya Mtwara kutumika
> Dar es Salaam badala ya huko huko Mtwara kwa ajili ya uzalishaji wa
> umeme, ukweli ni kwamba bado hilo sio jibu kwa watanzania wengine
> wengi ambao bado wanaona kwamba gesi ya Mtwara ilibidi izalishe umeme
> huko huko Mtwara badala ya Dar es Salaam ili kuwezesha taifa kupata
> faida kubwa zaidi.
>
> Ukweli ni kwamba upembuzi yakinifu ulikuwa ni muhimu sana ili kubaini
> faida na hasara za matumizi yote mbada ya gesi asilia ya Mtwara kwa
> ajili ya uzalishaji wa umeme ili kuwezesha ule mbada wenye faida kubwa
> zaidi kwa taifa kwa kipindi chote cha uhai wa mradi kuchaguliwa.
>
> Hii ni kuzingatia kwamba, uzalishaji wa umeme tarajiwa kutokana na
> gesi asilia ya Mtwara ni mradi mkubwa unaogharimu fedha nyingi sana na
> wa muda mrefu na kwamba matumizi mbadala ya gesi asilia ya Mtwara kwa
> ajili ya uzalishaji umeme ni mingi na inayotofautiana sana kwa gharama
> na faida kwa vipindi vyote vya uhai wake. Miongoni mwa matumizi hayo
> mbadala ni yale ya gesi asilia ya Mtwara kuzalisha umeme huko huko
> Mtwara na gesi asilia ya Mtwara kuzalisha umeme Dar es Salaam ambayo
> hutofautiana sana kwa gharama na manufaa kwa taifa kwa vipindi vyote
> vya uhai wake.
>
> Pia maamuzi ya Serikali kuhusu ni mbadala upi miongoni mwa matumizi ya
> gesi ya Mtwara mbadala kwa ajili ya uzalishaji wa umeme utumike hapa
> Tanzania yalibidi yahusishe wataalamu kutoka wizara zote, sekta
> binafsi na watanzania wote kupitia Bunge lao tukufu kwani matarajio na
> matakwa ya sekta mbalimbali za kiuchumi hapa nchini kutokana na
> matumizi mbada ya gesi asilia kwa ajili ya uzalishaji umeme yanaweza
> kutofautiana na kupingana sana.
>
> Hivyo, ilibidi upembuzi yakinifu ufanywe kwa kuzingatia mapendekezo ya
> wataalamu kutoka Wizara zote, sekta binafsi na watanzania wote kwa
> kupitia Bunge lao tukufu ili kuwezesha kubaini gharama na faida za
> matumizi yote mbadala ya gesi asilia ya Mtwara kwa ajili ya uzalishaji
> wa umeme kwa kuzingatia matarajio na matakwa ya wote kitaifa ili
> kuwezesha kuchaguliwa kwa ule mbadala wa matumizi ya gesi asilia ya
> Mtwara kwa ajili ya uzalishaji mkubwa wa umeme unaozingatia matarajio
> na matakwa ya wote na ulio na manufaa makubwa zaidi kwa wote na kwa
> taifa lote kwa ujumla kwa kipindi chote cha uhai wake.
>
> Ni vizuri serikali ikaweka bayana vipengele vilivyozingatiwa na
> taratibu zote zilizofuatwa kuwezesha kuamuliwa na Serikali gesi asilia
> ya Mtwara izalishe umeme Dar es Salaam badala ya Mtwara.
>
>
> Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2Ja1Vzi7j
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment