Sunday 27 January 2013

[wanabidii] Re: Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam

Ndugu Ezekiel

Uliyosema hapo juu yote ni kweli kabisa ulichosahau ni suala la ulinzi
na usalama endapo ikijengwa Mtwara Kutokana na historia ya maeneo hayo
lakini sipo kwenye hali ya kulieleza hilo kwa sasa .

Suala lingine ni Jinsi wasomi wetu wanavyoshirikiana katika
kuhakikisha maslahi ya nchi yanatimizwa .

Kuhakikisha maslahi yanatimizwa turudi kule TPDC je wanavitengo vya
biashara kwenye masuala ya gesi kwa mfano ? ukisoma tamko la viongozi
wa waislamu mkoa wa mtwara wanasema TPDC ndio walioamua bomba kujengwa
kwenda DSM na Kila kitu kufanyika DSM wakati mwanzo ilikuwa ni
Mtwara .

Tukitoka TPDC twende ERB na Bodi nyingine za uhandisi je hawa
walihusishwa vipi kwenye mradi kama huu kama bodi na sio kwa kuhusisha
wafanyakazi waliosajiliwa huko ambao wako kwenye kampuni zao binafsi ?
Je tuwe na bodi tofauti ya masuala ya Nishati ?

Kuna mgogoro fulani toka mwaka jana au juzi unaohusisha kampuni
zinazojengwa miundombinu kadhaa ya mabomba ya gesi nchini , kuna moja
imefunga vifaa ambavyo sio sahihi na viko na vipimo tofauti sio kama
walivyokubaliana kwenye mkataba , wengine wana matatizo na baadhi ya
benki ambazo inasemakana zinajihusisha na fedha haramu na ndipo fedha
zao zinapopitishwa kununulia baadhi ya vitendea kazi .

Kwa kumalizia tuangalie mfano wa wenzetu hawa wanaokuja kuwekeza
kwenye miradi hii jinsi wanavyopeana majukumu ya kuyatekeleza
kikamilifu , kwa mfano ukienda kwenye kisima kinachoitwa SIMBA -
Unakuta aliyefanya utafiti , mchimbaji , msambazaji , mtu wa masoko ,
ulinzi ni watu au kampuni tofauti tofauti na pengine zote zimetoka
nchi tofauti lakini waliobobea kwenye suala husika .

Nina taarifa hapa za mkutano wa gesi na mafuta uliofanyika mwaka jana
mlimani city kama kuna mtu anahitaji ntaweza kumpa uone tofauti ya
wenzetu na sisi maana wote walitoa taarifa zao .

On Jan 27, 9:28 am, "Tony PT" <tony_u...@yahoo.co.uk> wrote:
> Ezekiel,
>
> Nikubaliane nawewe kuwa kuna kudharauliana kwingi kati yetu waTz. Utaona hata hapa jukwaani watu walivyo wepesi kudadavua uwezo wa mtu hata pale fani ya huyo mtu mchangiaji ni "innocent" kabisa. Hii ni sifa kubwa ya ujinga wetu, tunaangalia nani kasema badala ya nini kimeongelewa!
>
> Tunafika hadi kudharau watu performers bila msemaji kutoa au kujielewa kuwa huenda yeye ndiye mjinga au mhurumiwa wa umbumbumbu kwenye fani husika. Imefikia hadi an undergrad anadharau a graduate kwenye fani yake au chuo alichosoma au mfumo alioutumia kupata elimu. Waelevu wa kielimu hawajiingizi kwenye mabishano kama hayo kwavile kila mtu aliyepata elimu na kupita hithibati, anayo elimu aliyoipata na kwa maeneo mengine anayebisha huenda akawa mwanafunzi wa huyo anayedharaulika!
>
> KEMS, point ambayo nimeieleza hapo awali ni ya uhusishwaji wa fani tofauti tofauti kwenye miradi yetu; unakuta wizara moja ambayo ina wataalamu wa sekta fulani kuona wanajitosheleza kwenye miradi bila kuhusisha sekta au utaalaam toka sekta nyingine. Ndipo nikasema huenda sekta za uchumi na biashara hazijahusishwa na wasimamizi wa mradi wa gesi kwenye kupata muafaka wa mradi unaohusisha sekta tofauti.
>
> Mfano utayarishaji wa wananchi wa Mtwara ungefanyika mapema na wakaelewa faida na hasara ya mradi kwenye nyanja zote. Wataalam wa jamii na maendeleo vijijini nao wangehusika na hata taasisi za kiraia kwenye utayarishaji wa wananchi.
>
> Makosa haya yanafanyika kila siku, hata kwenye ujenzi wa barabara, hawahusishi sekta nyingine ukiacha EIA, kitu kinachoangalia mazingira zaidi ya other socioeconomic au socio-political impact ya miradi.
>
> Hapa ndipo upweke wa uelewa wa wataalam wetu unapoanza kuonekana kwa hali zote na sijui hili la kujiamini sana kwa fani moja na kupuuza fani nyingine linatoka wapi!  Lakini ndicho kinachojitokeza mwisho wa siku kutoonekana uzuri wa mradi kwa jamii moja au zote.
> Tatizo jingine ni kutanguliza mbele sana fedha! Unakuta mradi uliosanifiwa miaka 10 iliyopita ukakwama kwa ukosefu wa fedha, ghafla unaanzishwa baada ya fedha kupatikana bila kupitiwa upya kujua kama bado unahitajika na kwa kiwango kipi mahitajio ya vipengele vya mradi vinatakiwa kubadilishwa au la. Hapa utaona mdudu rushwa au ufisadi unatawala maamuzi ya leo na kudharau umuhimu wa mapitio ya mradi. Hii inaonekana kuathiri miradi mingi mipya iliyotekelezwa kwa misingi hii.
> Huenda kuna siku tutabadilika baada ya makosa makubwa na madhara makubwa kama ilivyo mtwara kwa sasa kutokea!
> Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
> Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
>
>
>
>
>
>
>
> -----Original Message-----
> From: ezekiel kunyaranyara <ekunyarany...@yahoo.co.uk>
> Date: Sun, 27 Jan 2013 05:11:10
> To: tony_u...@yahoo.co.uk<tony_u...@yahoo.co.uk>; wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
>
> Reply-To: ezekiel kunyaranyara <ekunyarany...@yahoo.co.uk>
> Subject: Re: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam
>
> Tony PT
>
> Nashukuru kwa maoni yako. Ninavyoelewa mimi CHINA wanataka kusaidia sana katika nchi za kiafrica kwa vile wanataka kuliteka soko hivi kwa miaka ijayo. Lakini huenda mkakati wao wanamanufaa nao pia. Kwamba utakapofika wakati basi kuwe na mahitaji makubwa ya wao kwa kuwa ndio wanakuwa wanajua walichokifanya katika miradi husika.
>
> Chukulia kwa mfano uwanja wa taifa, kwa mtizamo wangu kama mtanzania wa kawaida viti vilivyowekwa havikuwa vya kiwango kile walivyoweka katika viwanja vya kwao. Hapa nafikiri walitaka (na wameweza) kutengeneza soko la baadaye. Na ukiangalia sana utaona kwamba ili nchi nyingine ziweze kutoa viti vya kurekebisha pale ni lazima kuwe na uzalishaji mpya kwa vile vipimo kidogo vinapishana na standard zinzokubalika.
>
> Huko china kuna kazi pia zinazofanyika lakini zinafail. Ninayo mifano ya madaraja na barabara yaliyoanguka au kubomoka baada tu ya kujengwa. bahati yao ni kuwa kila wanapojenga wanatunza kumbukumbu kiasi kwamba kabla ya kuchukua hatua kufuatilia tatizo lilikuwa wapi. Ikitokea kwamba kilichosanifiwa ni tofauti na kilichojengwa basi hatua huchukuliwa.
>
> Sina hakika sana na adhabu ya kifo ambayo mara zote imekuwa ikitamkwa hapa. kwa hiyo sina uwezo wa kuijadili. Ninachofahamu ni kuwa hatua zinachukuliwa ikiwa ni pamoja na kifungo ambacho wengine wanakuja huku kwetu ni wataalamu lakini wako katika vifungo na kutmika kufanya kazi. Huenda ni uataratibu mzuri lakini sijui kama forced labour inaweza kuwa na productivity nzuri, hili nal;o linahitaji mjadala wake.
>
> Nije kwa mradi wa GAS Mtwara, kwa taarifa nilizo nazo mimi wahisani walitaka ije DSM kwa vile kwao ni biashara ya ajira kwa watu wao na Tanzania ingepewa fedha nyingi pamoja na kuwa haina riba kubwa lakini itakuwa imeongeza kiwango cha madeni kwa nchi husika kwa hiyo hapo baadaye ingewezekana kuwa na uhakika wa kuwekeza katika maeneo nyeti. Lingine ambalo sina uhakika nalo sana ni kuwa katika sehemu ambazo bomba lingepitia kuna uwezekano wa madini ya URANIUM na mengine kama Corbat nk hasa sehemu za Lindi na jirani na bonde la Rufiji. Huenda katika kuchimba na kuchukua madini hayo gharama yao ingerudi na hivyo kazi hiyo ingefanyika kwa hasara.
>
> Hoja ya uzembe kwa wasomi wetu wetu mara nyingi mimi siiafiki sana. Unajua Tony, tunao wasomi wazuri sana. Na mara nyingi wamekuwa watumishi wazuri sana huko wanakokuwa wameajiriwa. Inakuwaje sasa wanapokuja hapa usomi wao haueleweki wala hauwasaidii wananchi wenzao?
>
> Chukulia mfano Prof. Muhongo. Niliwahi kuhudhuria presentation yake kuhusu ujenzi wa Chuo Kikuu pale Musoma. Hoja ya Mkoa ilikuwa kujenga Chuo Kikuu cha Waalimu lakini akaja na wazo la kujenga chuo kikuu cha  Bio - Science. Wote tuliokuwepo tulimkubali sana jinsi alivyokuwa anajenga hoja yake. wakati huo alikuwa SA katika Tume ya Science ambayo kama sikosei ndiko alikokuwa hadi uteuzi wake kama Mbunge na Waziri.
>
> Huenda tatizo lipo jingine ambalo inabidi tutafute kwa nini wasomi wetu hawakubaliki nyumbani. Tukijua hili na kulifanyia kazi tunaweza kujenga heshima yao na kujiamini kiasi kwamba tutakuwa tayari kuwasikiliza na wao kutusikiliza. Ilivyo kwa sasa kuna uadui mkubwa kati ya wasomi na wananchi wa kawaida. Siku zote wananchi wanadhani wasomi wanawadanganya na wasomi anaona kwamba wananchi hawaelewi. Tukiweka sawa hapo naamini tutakwenda.
>
> kazi ya msingi ninayoiona hapa ni kuweka sawa kwanza uwanja wa maelewano kati ya wananchi na viongozi wao kisha mjadala uendelee wa jinsi ya kufanya. Timu ya wataalamu ikae iangalie nini cha kufanya halafu kuwekwe mazingira ya kukaa pamoja kila upande ukitoa hoja na kupata majibu kisha utakelezaji ukianza kila mtu ashiriki upande wake.
>
> Njia hii inatumiwa sana na Wajapani. japani hata mtu pale anapotaka kubadilisha matumizi ya eneo lake au hata serikali hushirikisha wananchi. Matangazo hutolewa, michoro huandaliwa na kuwekwa hadharani na kwenye mitandao yao. wananchi wanatoa maoni yao na majibu yanatolewa kisha kunakuwa na siku ya kukutana pamoja na kujadiliana kwa pamoja. watumishi wa eneo hilo hupewa ruhusa kuhudhuria na kutoa michango yao. Huenda hawa wako katika kiwango cha juu cha ushirikishaji wa jamiii, lakini bado tunaweza kuanzia mahali.
>
> Samahani kwa maelezo mafupi kiasi hiki.
>
> K.E.M.S.
>
> ________________________________
>  From: Tony PT <tony_u...@yahoo.co.uk>
> To: ezekiel kunyaranyara <ekunyarany...@yahoo.co.uk>
> Sent: Saturday, 26 January 2013, 8:22
> Subject: Re: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam
>
> Ezekiel,Mikopo ya kichina haina shinikizo kama ya nchi za magharibi; wanachojali sana sana ni maslahi yao. Huo mkopo ni maombi ya Tanzania kwa kushauriwa na wataalam ambao au hawajaiva au nao kwa maslahi yao. Ukumbuke mara nyingi nchi yetu huletewa wataamu wengi wao ni toka 2nd world, sio premium! Nawaheshimu sana Ethiopia ambao kwa miradi yao mingi wataalam ni wao na akikosea mtu na kuitia hasara serikali anapotelea kuzimu! Wanakuwa very careful na they always score best. Injinia aliyejenga uwanja wa ndege wa Addis nasikia alipotea baada ya uwanja kufunguliwa na ukawa unavuja sana ikinyesha mvua! Hapa njaa, rushwa na kutoelewa mambo kunatuponza sana!
> Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
> Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
>
> ________________________________
>
> From:  ezekiel kunyaranyara <ekunyarany...@yahoo.co.uk>
> Date: Sat, 26 Jan 2013 15:37:50 +0000 (GMT)
> To: tony_u...@yahoo.co.uk<tony_u...@yahoo.co.uk>
> Subject: Re: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam
>
> Tony
> Nakusihi usikatee tamaa, nchi hii ni yetu wote.lazima tuisaidie kwa.kadri tuwezavyo. Sijui kama kuna mtu anaweza kutusaidia kuangalia gharama za kujenga mitambo ya kuzaalisha umeme Mtwara na gharama.za.kuusafirisha na kuunganisha na Grid ya taifa hapa DSM halafu ilinganishwe na gharama ya kuleta hiiyo.Gas kwa maana ya mabomba.
> Kwa uamuzi wa.kiserikali nadhani kama uamuzi ulikuwa tayari huko.nyuma nafikiri Ngeeleja asingeweza kuubadilisha ukizingatia kuwa mara nyingi tumekuwa tunasukumwa kufanya mambo yetu ya.kiuchumi kwa.matakkwa ya.wawekezaji.au wahisani.
> Usije ukakuta kwamba kwa.kuwa.fedha yenyewe ni ya mkopo basi masharti yake yalikuwa haya yaanayotiletea msuguano kama wananchi kwa upande mmoja na Serikali kwa upande mwingine.
> Maamuzi.ya.wahisani mara zote.yamekuwa.na.athari kubwa katika chumi za nchi nyingi zinzoendelea, mfano rahisi tu ni hapa kwetu tulipoambiwa kuuza nyumba zote za.Serikali na kuacha hakuna utaratibu maalumu.wa.watumishi.wapya.wanapohaamia inuwaje. Serikali imekuwa inaingia hasara kubwa kihifadhi watu hasa mawaziri katika hoteli kubwa kwa kipindi kirefu. Jambo pia liloingia naaufisadi yake.
> Nina hakika hata kama tukiridhia kkama taifa kujenga mfumo wa.uzalishajii umeme hapo Mtwara ili kuvutia wawekezaji kama si matakwa ya wakubwa
>
> ...
>
> read more »

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

1 comments:

  1. Ndugu Tony na Ezekiel,

    Ukweli ni kwamba kasoro kubwa za elimu walizo nazo wasomi wengi wa kizalendo ni zile zinazowezesha mtu kupata ajira na kuzitenda na sio kubuni, kuanzisha, kuendeleza na kusimamia biashara zinazoendana na elimu zao.

    Pamoja na kwamba mtu kasomea elimu ya kilimo na kufaulu katika kiwango cha hali ya juu mno, hata kufikia ngazi ya udaktari bado mtu huyu anashindwa kabisa kubuni biashara ya kilimo kuendeleza ardhi kubwa na nzuri zenye rutaba kama vile bonde la mto Rufiji au mto Ruvu linalomzunguka.

    Anashindwa kwa vile elimu yake sio timilifu, bado alihitaji kupata ile elimu ya biashara itakayomwezesha kubuni, kuanzisha, kuendeleza na kusimamisha mashamba ya kisasa ya kilimo cha biashara ndani ya yale mazingara ya ushindani yanayomzunguka.

    Elimu ya uchumi, uhasibu, biashara na usimamizi wa biashara ni muhimu kwa wanataaluma wa aina zote ili kuwawezesha kubuni, kuanzisha, kuendeleza na kusimamia biashara zenye tija kwenye fani zao.

    Elimu ya falsafa, siasa ya uchumi na maendeleo ni muhimu pia kuwawezesha wanataaluma wa aina zote kuelewa dunia inayowazunguka inafanya kazi vipi na ni kwa namna inabidi wajipange ndani ya dunia hiyo katika kubuni, kujianzishia, kuendeleza na kusimamia biashara ndani ya taaluma zao ili nao waweze kufanikiwa na kuendelea kuwepo na kukua kibiashara kwa kutegemea taaluma zao ndani ya dunia inayowazunguka.

    Kijana wa Australia au Canada anasoma kujipatia shahada ya kwanza ya jiolojia, anaongezea ingine ya biashara au uhasibu kwenye biashara za tafiti ya jiologia na nyingine ya usimamisi wa biashara ya tafiti za jiolojia halafu anajitafutia mtaji mbegu unaomwezesha kujianzishia kampuni ya utafutaji na uuzaji au uchimbaji wa madini ndani ya mataifa yanayoendelea. Anakuja hapa Tanzania kwa mfano na kwa kutumia geologists wetu watafuta ajira anafanikiwa kupata migodi na kuiendeleza kidogo kabla ya kuiuza na kujipatia mamilioni ya dola za kimarekani mbele ya geologists wetu fukara waliomsaidia.
    Ndio maana nimesema elimu inayotolewa vyuoni ni lazima iboreshwe ili iweze kuzaa wabunifu wa biashara na wenye uwezo wa kuziendeleza na kuzisimamia na sio tu watafuta ajira.
    Ukosefu wa elimu ya biashara miongoni mwa maofisa huko serikalini ndiyo ndiko kunakosababisha wao kupokea rushwa ya dola million moja kwa mfano ili kupitisha mkataba na wageni utakaolisababishia taifa hasa ya zaidi ya $ bilioni moja au kupitisha mradi mbada usiofaa na kuuacha ule usofaa kutokana na kutokuwa na uwezo wa kufanya upembuzi yakinifu ili kubaini faidi halisi za miradi ypote mbadala.
    Nakubali kabisa maamuzi kuhusu matumizi mbadala ya kutumia gesi ya Mtwara kuzalisha umeme Dar es Salaamu au Mtwara ilibidi yahusishe wataalamu kutoka wizara zote na taasisi zote za maendeleo na biashara au kampuni moja au mbili bingwa kimataifa kwenye upembuzi yakinifu uliohitajika kubaini manufaa ya miradi mbada ya uzalishaji umeme Dar es Salaam au Mtwara kwa vipindi vyote vya uhai wa miradi hiyo ili kuwezesha kuchagua mbadala wenye manufaa makubwa zaidi kwa taifa.

    ReplyDelete