Ninafuatilia mjadala huu kwa makini. Maoni yanayotolewa kuhusu uhalali wa malalamiko na hatimaye maandamano ya baadhi ya watu wa mtwara yana uzito wake. Na pia ufafanuzi wa serikali una mantiki yake. Wananchi wanyo haki ya kuhoji na kupata maelezo ya jinsi watakavyonufaika na uvunaji wa raslimali hii. Hii ni haki ya kila mtanzania, hata wale walio na dhahabu, samaki, wanyama pori nk, hata kama hawakuwahi kuuliza kwa sauti kubwa kama hii ya mtwara. Wananchi wanapouliza ni kiashiria kwamba serikali au mamlaka husika ilikuwa haitajatoa taarifa yenye kueleweka. Ombwe hili la kukosa taarifa rasmi linafungua mwanya wa mkanganyiko wa nini kinatokea na kuwafanya watu watafute taarifa na tafsiri kwa njia tofauti. Kwa mtazamo wangu, hili ni FUNDISHO MOJA KWA SERIKALI. Kwa mtazamo wangu, maelezo ya serikali (hata kabla sijatoa tathmini yangu kama ni sahihi au siyo sahihi) yalitakiwa kutolewa mapema sana sanjari na uamuzi wa kujenga bomba la gesi kuja Dar. Hii ingesaidia wadau wengi kuelewa na hata kuchangia/kuboresha mkakati wa kujenga bomba hilo. Na pia kuboresha njia ya kuwasiliana na wananchi kwa masuala kama haya. KWA UPANDE WETU WANANCHI, tunajifunza kuwa wawakilishi wetu katika vyombo vya maamuzi hawajawa na uwezo wa kutosha kushirikisha au hata kudadisi juu ya maamuzi yanayogusa maslahi ya wananchi. Sanjari na kuibana serikali kwa njia hizi zilizotumika Mtwara tutafute mbinu nyingine za kuwawajibisha madiwani na wabunge ili wasiwe sehemu ya watu wanaolalamikia serikali (na mara nyingine kijiunga na katika maandamano ya raia!). KWA SASA, serikali ione haja ya kuendeleza mazungumzo ya ufafanuzi wenye kuleta tija na kujenga mshikamano badala ya kulaumiana. Kila mtu anayechangia hapa ni mdau na ana haki ya kusikilizwa. Nafasi ya ya kujenga ndiyo imeanza, tuitumie vyema ndugu zangu. makongo ---------------------------------------------------------------- Japhet Maingu Makongo Director, Ubunifu Associates Ltd P.O. Box 32971, Dar es Salaam, TANZANIA Website: www.ubunifu.co.tz, info@ubunifu.co.tz, Tel: +255 22 2762027, Mobile:+255 754 571 256 --- On Thu, 1/3/13, alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com> wrote:
|
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment