Huyu mzee ni tatizo ndio maana nampangia magogo 2015.
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network
From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thu, 3 Jan 2013 16:32:22 +0000
To: Wanabidii googlegroups<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: RE: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani
Kiukweli kabisa, salamu si dini. Dini ni utii wa mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu. Kuitumia salamu visivyo ni tatizo.
Biblia haijamfundisha muumini yeyote salamu ya "Bwana Asifiwe" au "Tumsifu Yesu Kristo". Huu ni ubunifu tu wa watu na hauna ulazima wowote kufuata; sana sana ni ujuha tu. Mbona zamani hii salamu haikuwa na umaarufu huu? Wa nini leo kama si ulofa wa mawazo tu na hisia?
Kurani haijamfundisha muumini yeyote salamu ya "Asalam Aleikum" bali hii ni salamu ya Kiarabu, kama zilivyo "Ugonile" kwa Kinyakyusa au "Oyimore" kwa Kijaluo, au "Salut" kwa Kifaransa, au "Konichiwa" kwa Kijapani, au "Namaste" kwa Kihindi, n.k. Hakuna dini kwenye hii salamu na ndiyo maana hata Waarabu wakristo wanaitumia.
Hivyo, kuzitumia salamu hizi kwa kudhani kwamba ni kuziheshimu dini si sahihi. Hilo moja. Ni kujichanganya na kupotosha umma.
Pili, unapowasalimia Watanzania kwa dini zao, je, inakuwaje kwa wale wasiokuwa na dini hizo? Je, vipi kwa wasiomwamini Mungu? Je, vipi kwa Wakristo wasiotumia salamu hizo? Inakuwaje kwa muislamu asiyekitumia Kiarabu mathalani yile wa Bosnia au Uchina?
Lakini mbaya zaidi ni kujikuta kwamba tunajenga mbegu mbaya ya kujitambulisha kwa dini zetu badala ya utu wetu na Utanzania wetu. Hili ni jambo la hatari na linapaswa kupigwa vita na wote wanaoitakia mema Tanzania na wenye ufahamu wa wanachokisema na kukifanya; tusiendeende tu kama maboya majini, tutakuja kujuta. Hii ni mbegu ya kibaguzi na ni ulofa wa kiitikadi, kisiasa na ugonjwa wa kutojifahamu. Kwa nini unataka usalimiwe kwa unachodhani ni dini na wakati si lolote si dini?
Tanzania ni nchi ya Watanzania; siyo nchi ya Wakristo na Waislamu.
Matinyi.
Date: Thu, 3 Jan 2013 08:26:11 -0800
From: bertmutta@yahoo.com
Subject: RE: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani
To: wanabidii@googlegroups.com
Kama wanasiasa na watu wengine hutumia salaam za aina tatu majukwaani kujali makundi matatuya kiimani (asalaam alikum, Bwana Yesu asifiwe, Tumsifu Yesu Kristu) basi asalaam aleikum sio sahihi tukiwa kanisani. ELIMU YA KUKARIRISHWA
Gosbert Mutasingwa P.O Box 40 Biharamulo KAGERA-Tanzania 0784 857 775/0758 491 247
--- On Thu, 1/3/13, Juma abdallah <juma.abdallah@huawei.com> wrote: From: Juma abdallah <juma.abdallah@huawei.com> Subject: RE: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com> Date: Thursday, January 3, 2013, 5:49 AM
Asalam alikum-Amani ya bwana iwe juu yenu Waalaikum salaam- Nanyi juu yenu iwe amani ya bwana. From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On Behalf Of Reuben Mwandumbya Sent: Thursday, January 03, 2013 3:05 PM To: wanabidii@googlegroups.com Subject: Re: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani Katika uhalisia Shekifu kakosea,alitakiwa kusoma mazingira asikwaze wengine. Salamu hii ni ya Kiarabu hata kama maana yake kwa kiswahili ni Jambo lakini haikutakiwa pale,then bado kachanganya dawa zinazoripuka. Pamoja na kwamba wapo Waarabu Wakristo ukweli unabaki kwamba sio asili yao,inawezekana walislimu kama wengine wanavyofanya Reuben From: Salim Rupia <zabarelo@gmail.com> To: wanabidii@googlegroups.com Sent: Wednesday, January 2, 2013 11:08 PM Subject: Re: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani
Sikuwepo, labda ilikuwa Swaumu hiyo nyingine lakina alikuwa na Sheikh Ramia Bagamoyo na kichwa kilimuuma sana siku hiyo na pia hapa nam "quote" yeye mwenyewe kwenye hotuba zake; ukipenda kusikiliza utasikia. Lakini sikuwa na maana ya kuchanganya hoja na Swaum; tuseme nimekosea. Vipi kuhusu hiyo Salaam? Maana ndo hoja nilochangia kuna mtu alisema ya kijinga na upumbavu... 2013/1/3 Reuben Mwandumbya <ipyana75@yahoo.com> Salim usitupotoshe tafadhali; Au labda upe ufafanuzi swaum unayoongelea hapa ni ipi?kama ni ya Kiislamu hutakuwa sahihi. Hata Wakristo tunafunga na tunakuwa na swaumu wakati wa mfungo wetu kipindi kuelekea PASAKA. Reuben Jamani, "Asalaam Alaykum" ni sawa na "jambo?"; yaani greetings" tu ila kwa lugha ya Kiarabu. Mnajua kuwa kuna Waarabu Wakristo na wanasalimia hivyo hivyo? Na ujinga na upumbavu unaosemwa hapa ni wa salaam hiyo na walioanzisha ama ni huyo Muumini binafsi? Mi namkumbuka Mkatoliki mmoja aliekuwa hadi anafunga Swaum ndiye aliehamasisha sana kusalimia kwa salaam hiyo majukwaani; alikuwa Mkuu wa kwanza wa Nchi hii. Tunasemaje hapo... Huyo M bunge alikosea sana kwa kuwa kama wengi waliochangia wanavyosema, inawezekana alikariri salaam; kuwa akiwa mbele ya watu wengi aanze na salaam hiyo bila kukumbuka mkusanyiko ule ulikuwa wa watu gani. Mi nakumbuka wakati wetu kwa wale tulopita National Service (JKT) ukipangwa ulinzi "Main Gate" kuna amri na maswali ambayo unakariri kuuliza kwa kila dereva wa gari litakalotaka kuingia kambini. Tulikuwa tunawatania kina "green kwanja" kuwa wao hata mchana watamwambia dereva "zima taa za mbele, washa taa za ndani" kwa kuwa hiyo ndo ilikuwa amri ya kwanza! Kisa; kukariri... 2013/1/3 matinyi@hotmail.com <matinyi@hotmail.com> Hizi salamu ni za kijinga mno mno. Sijui huu upumbavu ulianzishwa na nani? Yaani tu taifa la ajabu sana. Matinyi.
T-Mobile. America's First Nationwide 4G Network
----- Reply message -----
From: "godfred mbanyi" <mbanyibg@yahoo.com> To: <wanabidii@googlegroups.com> Subject: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani Date: Thu, Jan 3, 2013 5:14 am
Huu unafiki wa kisiasa utawaponza wengi!!! Utakuta kiongozi ni mwislamu safi, swala zote na hija ameenda, lakini anasimama kwenye jukwaa la siasa na salaam za " Tumsifu Yesu Kristo"!!!!!!!!!! Kisa, kutafuta sapoti ya wapiga kura!!! Asifiwe, mtu usiyemwamini?
--- On Thu, 1/3/13, magreth Mulokozi <m.mulokozi@gmail.com> wrote:
From: magreth Mulokozi <m.mulokozi@gmail.com> Subject: Re: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani To: wanabidii@googlegroups.com Date: Thursday, January 3, 2013, 2:07 AM
Duu anatafuta kura za 2015 sasa , duu pole sana Nd Shekifu
2013/1/3 matinyi@hotmail.com <matinyi@hotmail.com> .....alikariri.....siyo alikalili.
T-Mobile. America's First Nationwide 4G Network
----- Reply message ----- From: "adeladius makwega" <makwadeladius@googlemail.com> To: "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> Subject: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani Date: Thu, Jan 3, 2013 4:46 am
Shekifu aunza mwaka mpya Vibaya
Mbunge wa Lushoto Hendry Shekifu ameuunza mwaka wa 2013 vibaya baada ya kuzomewa Kanisani na waamini katika sherehe za mwaka mpya baada ya kupewa nafasi ya kuwasalimu washirika wa Kanisa Kuu la KKKT Lushoto Tanga.
Ibada hiyo ya kuukaribisha mwaka mpya ilianza kwa waumini kupokea mahubiri ya mwaka mpya yaliyohubiriwa na Mchungaji Walelaza na baadae kufuatiwa na ibada ya ubatizo ambapo watoto wawili kutoka familia mbili walibatizwa.
Mara baada ya ubatizo huo ibada ilifuatiwa na utoaji wa Sadaka huku mbunge huyo wa Lushoto akionekana kushiriki kikamlifu katika ibada hiyo .
Akiwa amevalia suti ya rangi nyeusi yenye mistari midogo midogo miyeupe Mbunge Shekifu ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwamo ukuu wa mkoa alipewa nafasi ya kusimama mbele ya waamini mithili ya kasisi.
Nafasi hiyo ilitolewa wakati wa Matangazo huku mchungaji akiwaomba waumini hao kumsikiliza Mbunge wao ili awasalimu. Basi Mbunge Shekifu alisimama huku akiweka vizuri koti kwa kujifunga vifungo vya koti hili ambalo lilionekana kuutosha mwili wake mkubwa uliojengeka vizuri.
Alikisogelea kipaza sauti mara alianza kuongea kwa kujiamini."Aslaam Aleikumuuu…" Duu utangulizi huo uliharibu hali ya hewa ya kanisa hilo wauumini kuanza kuzomea na kuguna kutokana salaam hiyo iliyotolewa mwanzoni katika sehemu isiyo sahihi.
Hali hiyo iliwafanya waumini hao kuibua munkali huo kutokana na kitendo cha mbunge huyo pengine kukalili namna ya kusalimia watu katika majukwaa ya kisiasa bila ya kujua kuwa sasa madhari aliyokuwa nayo ilikuwa ya salaam moja tu kama sikosei ni Bwana Yesu asifiwe au Tumsifu Yesu Kristu.
Hekima ilitumika pengine huku yule aliyempa nafasi ya kuwasalimu wauumini wake akijilaumu kuitoa nafasi hiyo iliyotia shubiri kanisani hapo na kuibua zomeazomea hiyo ambalo sio jambo la kawaida kwa waumini kufanya hivyo.
Mchungaji Walelaze ilibidi kuinuka na kusema waziwazi kuwa Ndugu Shekifu umekosea sana kwanza ulitakiwa kujitambua kuwa wewe japokuwa ni Kiongozi pia wewe ni mkiristu lolote utakalo fanya popote pale tambua unamajukumu mawili kwanza ukiristu wako na pili kuwa kiongozi. Hapa ni kanisani ulitakiwa kuwasalimia waashirika kwa salaam yao siyo salaam hiyo uliyoitoa hapa.
Basi mchungaji huyo alimaliza mtafaruku huo huku mbunge huyo wa Lushoto akishuka katika mimbari ya kanisa hilo kwa fedhea na kurejea katika kiti chake ambacho kilikuwa jirani na mlango wa kutoka nje ya kanisa.
Mara baada ua ibada hiyo ya mwaka mpaya mbunge huyo alionekana kuwa mtu wa mwisho kuondoka kanisani mara baada ya washirika wote kuondoka lakini washirika hao walisema kuwa mbunge huyo amekalili kusalimia kwa salaam hizo ndiyo maana alipitiwa.
"Mimi nilitaka Mbunge aombe msamaha kwa alilolifanya sio kuondoka kimya kimya tu hawa wanasiasa hawana adabu kabisa wanakuja na mbwembwe alafu wanapata aibu."alisema mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Mama Sarah.
Mshirika mwingine alimuunga mkono mchungaji Waleleza kwa kumkumbusha Mbunge huyo kuwa makini sana akiwa kanisani na kuheshimu salaam za ibada za makanisa sio kuja na salaam za nyumba zingine za ibada.
"Pengine inawezekana Mbunge huyu asipewe tena nafasi ya kuwasalimu waumini kanisani kutokana na kosa hili," aliserma mzee mmoja wa makamo ambaye alidai kuwa hilo ni kosa baya.
Mwishoni alionekana Mbunge Shekifu akiingia ndani ya gari yake nyeupe yenye Bendera ya CCM ikipeperuka mkono wa kushoto. Ndani ya gari hiyo kukiwa na akina mama watatu ambao walionekana wakifunga milango na dereva wa gari hilo akiondoa gari katika eneo la kanisa hilo.
Wasalaam Adeladius Makwega
-- Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
-- Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

-- Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. -- Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

|
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment