Thursday 3 January 2013

Re: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani

Nimekupata Matinyi

On 1/3/13, magreth Mulokozi <m.mulokozi@gmail.com> wrote:
> Duu anatafuta kura za 2015 sasa , duu pole sana Nd Shekifu
>
>
> 2013/1/3 matinyi@hotmail.com <matinyi@hotmail.com>
>
>> ....alikariri.....siyo alikalili.
>>
>>
>>
>>
>> T-Mobile. America's First Nationwide 4G Network
>>
>>
>> ----- Reply message -----
>> From: "adeladius makwega" <makwadeladius@googlemail.com>
>> To: "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>,
>> "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
>> Subject: [wanabidii] Mbunge wa Lushoto azomewa Kanisani
>> Date: Thu, Jan 3, 2013 4:46 am
>>
>>
>> Shekifu aunza mwaka mpya Vibaya
>>
>> Mbunge wa Lushoto Hendry Shekifu ameuunza mwaka wa 2013 vibaya
>> baada ya kuzomewa Kanisani na waamini katika sherehe za mwaka
>> mpya baada ya kupewa nafasi ya kuwasalimu washirika wa Kanisa Kuu la
>> KKKT Lushoto Tanga.
>>
>> Ibada hiyo ya kuukaribisha mwaka mpya ilianza kwa waumini kupokea
>> mahubiri ya mwaka mpya yaliyohubiriwa na Mchungaji Walelaza na
>> baadae kufuatiwa na ibada ya ubatizo ambapo watoto wawili kutoka
>> familia mbili walibatizwa.
>>
>> Mara baada ya ubatizo huo ibada ilifuatiwa na utoaji wa Sadaka
>> huku mbunge huyo wa Lushoto akionekana kushiriki kikamlifu
>> katika ibada hiyo .
>>
>> Akiwa amevalia suti ya rangi nyeusi yenye mistari midogo
>> midogo miyeupe Mbunge Shekifu ambaye aliwahi kushika nyadhifa
>> mbalimbali zikiwamo ukuu wa mkoa alipewa nafasi ya kusimama mbele ya
>> waamini mithili ya kasisi.
>>
>> Nafasi hiyo ilitolewa wakati wa Matangazo huku mchungaji
>> akiwaomba waumini hao kumsikiliza Mbunge wao ili awasalimu. Basi
>> Mbunge Shekifu alisimama huku akiweka vizuri koti kwa kujifunga
>> vifungo vya koti hili ambalo lilionekana kuutosha mwili wake
>> mkubwa uliojengeka vizuri.
>>
>> Alikisogelea kipaza sauti mara alianza kuongea kwa
>> kujiamini."Aslaam Aleikumuuu…" Duu utangulizi huo uliharibu hali ya
>> hewa ya kanisa hilo wauumini kuanza kuzomea na kuguna kutokana
>> salaam hiyo iliyotolewa mwanzoni katika sehemu isiyo sahihi.
>>
>> Hali hiyo iliwafanya waumini hao kuibua munkali huo kutokana na
>> kitendo cha mbunge huyo pengine kukalili namna ya kusalimia watu
>> katika majukwaa ya kisiasa bila ya kujua kuwa sasa madhari
>> aliyokuwa nayo ilikuwa ya salaam moja tu kama sikosei ni Bwana
>> Yesu asifiwe au Tumsifu Yesu Kristu.
>>
>> Hekima ilitumika pengine huku yule aliyempa nafasi ya kuwasalimu
>> wauumini wake akijilaumu kuitoa nafasi hiyo iliyotia shubiri
>> kanisani hapo na kuibua zomeazomea hiyo ambalo sio jambo la
>> kawaida kwa waumini kufanya hivyo.
>>
>> Mchungaji Walelaze ilibidi kuinuka na kusema waziwazi kuwa Ndugu
>> Shekifu umekosea sana kwanza ulitakiwa kujitambua kuwa wewe
>> japokuwa ni Kiongozi pia wewe ni mkiristu lolote utakalo fanya
>> popote pale tambua unamajukumu mawili kwanza ukiristu wako
>> na pili kuwa kiongozi. Hapa ni kanisani ulitakiwa kuwasalimia
>> waashirika kwa salaam yao siyo salaam hiyo uliyoitoa hapa.
>>
>> Basi mchungaji huyo alimaliza mtafaruku huo huku mbunge huyo wa
>> Lushoto akishuka katika mimbari ya kanisa hilo kwa fedhea na
>> kurejea katika kiti chake ambacho kilikuwa jirani na mlango wa
>> kutoka nje ya kanisa.
>>
>> Mara baada ua ibada hiyo ya mwaka mpaya mbunge huyo alionekana
>> kuwa mtu wa mwisho kuondoka kanisani mara baada ya washirika wote
>> kuondoka lakini washirika hao walisema kuwa mbunge huyo
>> amekalili kusalimia kwa salaam hizo ndiyo maana alipitiwa.
>>
>> "Mimi nilitaka Mbunge aombe msamaha kwa alilolifanya sio
>> kuondoka kimya kimya tu hawa wanasiasa hawana adabu kabisa wanakuja
>> na mbwembwe alafu wanapata aibu."alisema mama mmoja
>> aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Mama Sarah.
>>
>> Mshirika mwingine alimuunga mkono mchungaji Waleleza kwa kumkumbusha
>> Mbunge huyo kuwa makini sana akiwa kanisani na kuheshimu salaam
>> za ibada za makanisa sio kuja na salaam za nyumba zingine
>> za ibada.
>>
>> "Pengine inawezekana Mbunge huyu asipewe tena nafasi ya
>> kuwasalimu waumini kanisani kutokana na kosa hili," aliserma mzee
>> mmoja wa makamo ambaye alidai kuwa hilo ni kosa baya.
>>
>> Mwishoni alionekana Mbunge Shekifu akiingia ndani ya gari yake
>> nyeupe yenye Bendera ya CCM ikipeperuka mkono wa kushoto. Ndani ya
>> gari hiyo kukiwa na akina mama watatu ambao walionekana wakifunga
>> milango na dereva wa gari hilo akiondoa gari katika eneo la
>> kanisa hilo.
>>
>>
>> Wasalaam Adeladius Makwega
>>
>> --
>> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
>> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>>
>> --
>> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
>> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>>
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment