Sunday 27 January 2013

Re: [wanabidii] HALI NI MBAYA MTWARA DAMU YA WATU SABA YAMWAGIKA NYUMBA ZA WABUNGE ZACHOMWA MOTO

Tabia hii tumeianzisha na kuilea wenyewe sasa ona yanayotupata, huko
nyuma viongozi wetu waliona kutumia polisi katika kuzima ghasia ndo
suluhisho pekee. Watu wamebadilika hawana utii kwa viongozi wala jeshi
la polisi, tukubali mabadiliko hayo na kutafuta mbinu mbadala. Kitendo
cha kuchoma nyumba za wanasiasa kinaonyesha kwamba kuna chuki
zilizojengeka kati ya wanasiasa hao na raia au kati ya makundi yenye
itikadi tofauti

Imefikia kiwango raia wanaliona jeshi la polisi kama si lao bali ni la
watu wanaoishi dunia nyingine. Tuanze kufikiria njia za kutmia
ushawishi badala ya kutumia nguvu kama njia pekee ya kumaliza
manunguniko ya watu. kama kuna malalamiko ni vyema kukaa chini na
kujaribu kulielewa tatizo lenyewe ndo ufumbuzi wa kudumu utapatikana.
Kwa mwendo huu tuna tofauti gani na nchi nyingine zenye vurugu? Kidogo
kidogo mwisho ni mauaji ya wenyewe kwa wenyewe. watu hawaliogopi jeshi
la polisi wala mamlaka iliyo madarakani, ni unyama tu. Lazima tutafute
suluhisho sahihi tofauti na hapo maisha yetu ni wasiwasi, uhasama
mkubwa na hatari tupu na tuisubirie misiba kila uchao

2013/1/27 richard bahati <ribahati@gmail.com>:
> HALI NI MBAYA MTWARA DAMU YA WATU SABA YAMWAGIKA NYUMBA ZA WABUNGE ZACHOMWA
> MOTO
>
> Habari zaidi na picha hapa:
> http://goldentz.blogspot.com/2013/01/hali-ni-mbaya-mtwara-damu-ya-watu-saba.html
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment