Wednesday 17 October 2012

[wanabidii] Re: ADHABU YA KIFO NI LAZIMA KATIKA SHERIA ZETU


-----Original Message-----
From: LENGAI OLDOINYO
Sent: 10/17/2012 8:37:15 AM
To: info@butmaninternational.com , sematangotours@cybernet.co.tz , serenacarhire@habari.co.tz , sgresort@yahoo.com , sss@habari.co.tz , tours@albatros.co.tz , mia@albatros.co.tz , info@chadema.or.tz , rassingida@pmoralg.go.tz , mhariri@habarileo.co.tz , advertising@dailynews.co.tz , jennie@albatros.co.tz , shidolya@yako.habari.co.tz , sssafaris@cybernet.co.tz , s-s.kolowa@web.de , worldtourstanzania@hotmail.com , wanabidii@googlegroups.com , unasemaje@radiofreeafricatz.com , mwananchipapers@mwananchi.co.tz , globalpublishers@dar.bol.co.tz , educate@intafrica.com , costech@costech.opc.org , info@satif.or.tz , info@satf.org , eotf@raha.com , eotf@cats-net.com , zitto@chadema.or.tz
Subject: [wanabidii] RE: ADHABU YA KIFO NI LAZIMA KATIKA SHERIA ZETU

 

Mimi ni Mtanzania wa kwanza kukubali adhabu ya kifo iwepo kwenye katiba ya nchi yetu na itekelezeke kisheria japokuwa naogopa kufa. Hii inatokana na tabia ya watu kuchukua sheria mikononi mwao. Itasaidia pia Polisi kuacha tabia za kuwaua raia wasio na hatia hovyo. Polisi anatakiwa ampekele mshitakiwa kwa Hakimu lakini hawafanyi hivyo wao wanachukua jukumu lisilo lao kutoa adhabu. Ikiwepo sheria ya kuhukumu kifo kwa anayeua mwenzake watakoma kutumaliza na risasi.

 

Watanzania wamekuwa na kiburi sana hasa wanapoona kuwa hata wakichuna wenzao ngozi, au wakiua kwa makusudi bado Rais atawatetea kwa kuwafutia adhabu hiyo.

Kwa nini Rais asiwafutie adhabu ya Kifungo cha Maisha gwiji la Muziki wa dansi Nguza (Papi Kocha) sijui na wanawe kama anayo huruma sana. Kesi yao haikuwekwa bayana na pia adhabu yao haikuwa wazi kulingana na kosa walilolitenda. Hii ni kutokana na kesi yao kufanyika kwa mda mfupi ukilinganisha na kesi zingine. Watu tuliitilia mashaka Ikulu kuhusika na kesi hii. Sasa kama Rais anaona kuua ni dhambi kwa nini asione kifungo cha maisha kuwa pia ni dhambi.

 

Katika nchi zingine kama China adhabu ya kifo ni jambo la kawaida. Ukikutwa na kosa lenye adhabu ya kifo lazima utahukumiwa kifo. Nchi za Kiarabu wanazo adhabu za Kifo tukichukua mfano mdogo tu. Mwanamke aliyezini anahukumiwa kupigwa mawe mpaka kufa kwani hiyo sio adhabu. Nchi ikiwa na sheria kali na zinazotekelezeka watu wanakuwa waoga kufanya makosa. Siku hizi Tajiri anachukua Bastola Serekalini na ukiingiza mifugo kwenye shamba lake kwa bahati mbaya hangoji Polisi akukamate upelekwe mahakamani bali anakuhukumu kwa kukupiga risasi na Serekali haichukui hatua zozote sasa hii ni nchi au danguro. Watu wanajenga nyumba za kuishi na kulaza wageni magirili kila mahali nchi nzima nyumba zimekuwa kama magereza. Hii inaonyesha wazi wazi kuwa Watanzania hatuaminiani. Nyumba za Biashara grili, nyumba za kulala girili, nyumba za mahabusi girili, nyumba za wafungwa girili, Mochwari girili, hii ni nchi au ahera kusikorudi watu.

 

Lazima ifikie mahali sasa tuachane na Siasa zilizopitwa na wakati tuijenge Tanzania yenye amani kwa kutunga sheria kali za kuwabana wahalifu wa aina zote na sheria tukitunga ziwe zinatekelezeka. Ndugu zetu wa Kenya wananifurahisha jambo moja. Wakitunga sheria ukavunja unawajibika. Walitunga sheria ya kutokojoa hovyo inatekelezeka, walitunga sheria ya kutokuvuta sigara hadharani ni kweli usijaribu, wakatunga sheria ya kutoongea na simu ukiendesha gari inafanya kazi barabara. Sasa wametunga sheria hakuna kuuza Simu bandia Simu zote zimeletwa Tanzania na wafanya biashara wakijua hiki ni kisiwa cha uhalifu. Pita madukani utakuta wafanya biashara wa Kenya wameleta Simu kuziuza kwa wafanyabiashara wahalifu wa Tanzania. Hivi viongozi wetu kwa nini mko kama masanamu Serekalini. Kwa nini mnaifanya Tanzania iliyokuwa na heshima enzi za Mwalimu kuwa kichaka cha uhalifu. Tunataka mabadiliko ya haraka sana Tanzania.

Mkereketwa

Lengai Ole Letipipi

 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment