Wednesday 3 October 2012

Re: [wanabidii] Mahusiano yetu ya kifamilia hayahusiki na sababu na dhamira yetu ya kujiunga CHADEMA

Muganda,
Alichohoji Dr nami namuunga mkono ni: Mwanzilishi wa CHADEMA ni baba yao mzazi (kwa kauli yao) nasi tunafahamu Steven (Baba yao mdogo) ndiye mwanzilishi wa CHADEMA. Basi wafafanue conflict hiyo

--- On Tue, 10/2/12, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:

From: Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Mahusiano yetu ya kifamilia hayahusiki na sababu na dhamira yetu ya kujiunga CHADEMA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tuesday, October 2, 2012, 7:46 AM

Dr,
Soma tena kwa makini. Baba yao ni George Wassira, kaka yake Steven Wassira na mwanzishi wa Chadema. Upo hapo?
em

2012/10/2 Dr. Hamisi A. Kigwangalla <hkigwangalla@gmail.com>
mbona wanajichanganya hawa warembo? Maana kuna para moja hapo juu (para ya pili) wanakana kuwa si watoto wa Stephen Wassira na kwamba huyo ni baba yao mdogo, baadaye kule mwisho wanasema CDM ilianzishwa na baba yao mzazi...sasa which is which? Aliyeanzisha CDM ni Stephen ama ni George? na je Baba yao mzazi ni nani, ni Stephen ama ni George Wassira? 

2012/10/2 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Tarehe 30/09/2012 mimi Esther Wasira na dada yangu Lilian Wasira
tulijiunga na CHADEMA na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CHADEMA
Mh. Dr Willibrod Slaa. Tulielezea kwa kirefu sababu za sisi kujiunga
Chadema na tukasisitiza kuwa tumeridhika kuwa CHADEMA ni chama chenye
dhamira safi ya kuiongoza Tanzania na kwamba ni chama kinacholeta
matumaini mapya ya kuijenga Tanzania mpya yenye neema.

Waandishi wa habari walijaribu sana kutudodosa kujua tuna uhusiano
gani na Waziri Steven Wasira. Tulielezea wazi kuwa mahusiano yetu ya
kifamilia hayahusiki na sababu na dhamira yetu ya kujiunga CHADEMA.
Hata hivyo tulielezea kuwa Waziri Steven Wasira ni baba yetu mdogo
ambaye alinyang'anyana ziwa na baba yetu mzazi, wakili George Wasira.
Tulidhani hiyo ilitosha na lisingekuwa swala tena la kujadili na
badala yake hoja ya kujadiliwa ingeweza kuwa sababu tulizozieleza za
kujiunga CHADEMA.

Tunasikitishwa sana na malumbano yaliyofuata baada ya hapo kuhusu kama
sisi ni watoto wa Wasira au la. Kama tulivyoeleza, tumejiunga CHADEMA
kwa sababu tulizozieleza hapo awali na wala si kwa sababu nyingine
yeyote. Hatujajiunga CHADEMA kumdhalilisha mtu, kumfedhehesha mtu au
kukipatia umaarufu CHADEMA kwa vile tu tunatumia jina la Wasira.
CHADEMA ni chama cha siasa tena chenye wanachama na wafuasi wengi
Tanzania hivyo si kashfa bali ni fahari kubwa mtu kujiunga CHADEMA na
tena ni ushahidi wa mtu kujitambua.

 Pia CHADEMA ni Chama maarufu sana Tanzania kwa sasa hata pengine ni
maarufu kuliko CCM hivyo hakihitaji kujipatia umaarufu kwa mgongo
wetu. Sisi tunawaheshimu sana wazee wetu na tutaendelea kuwaheshimu
ila linapokuja swala la chama cha kujiunga linabaki kuwa hiari yetu
kwa kuzingatia sera za chama na uwezo wa chama husika katika kujenga
Tanzania tunayoitaka na hilo ndilo lililotupeleka CHADEMA. Na hii ni
haki yetu ya msingi kabisa inayolindwa na Katiba ya nchi hii chini ya
ibara ya 20(1).

Ikumbukwe kuwa mmoja wa Waanzilishi wa CHADEMA ni Mzee Wasira. Dhamira
ya kuanzisha CHADEMA ilikuwa ni kushika dola na hili ndilo CHADEMA
imekuwa siku zote inajaribu kuwashawishi Watanzania kuwa sasa
wamekomaa na wanastahili kuchukua dola. Kwa vile kuchukua dola ilikuwa
ndio ndoto ya baba yetu mzazi Mwanzilishi wa CHADEMA, sisi kama watoto
tumejiunga na M4C ya CHADEMA ili tuweze kutimiza ndoto ya baba yetu
kuwa CHADEMA siku moja ichukue jukumu la kuiongoza Tanzania.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Lilian Wasira 0719 604156
Esther Wasira 0655 048797

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
                +255 782 636963
website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment