Wednesday 3 October 2012

Re: [wanabidii] Kauli Ya JK Kuhusu Kifo Cha Daudi Mwangosi - Mwanzo

Kauli hii ilikuwa sahihi kuitoa siku tatu nne za kwanza. Angekuwa anaagiza vyombo vyake kuchukua tahadhari katika kuadhibu wasiathibu wasiohusika.
 
Kwa sasa nilitegemea atweleze haki imefikia wapi katika kutendeka. Ingekuwa ni hospitali tungesema Prescription imetoka wakati wa maziko, si mgonjwa tena. Tunategemea serikali itweleze sasa imefikia wapi katika kuwaadhibu waliokosea na hatua zilizochukuliwa jambo kama hilo kutotokea..
Pili sielewi msingi wa lawama kwa taasisi kutofuata maelekezo ya Polisi katika kuandamana au kufanya mikutano. Kama halihusiani na mauaji ya Daudi sawa maana hakukuwa na maandamano wala mkutano wa hadhara ninavyokumbuka, ila Mkutano wa ndani wa chama cha siasa.

--- On Tue, 10/2/12, Magiri paul <kiganyi@gmail.com> wrote:

From: Magiri paul <kiganyi@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Kauli Ya JK Kuhusu Kifo Cha Daudi Mwangosi - Mwanzo
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tuesday, October 2, 2012, 11:21 AM

RAIS Jakaya Kikwete amezungumzia mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel 10, Daudi Mwangosi na kusisitiza umuhimu wa haki kutendeka katika suala hilo.
Akizungumza katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi uliopita, Rais Kikwete alisema mauaji hayo ni ya kusikitisha na kuongeza; "Jambo la msingi ninalotaka kusisitiza ni polisi na kutendewa haki. Asiwajibishwe asiye husika."
Mbali na kusisitiza umuhimu wa haki kutendeka katika mauaji hayo, aliliagiza Jeshi la Polisi, pale panapotokea malumbano kati yake  na wafuasi wa kikundi cha kijamii au vyama vya siasa au wananchi, lazima wahakikishe hawatumii nguvu kupita kiasi, "Polisi lazima wahakikishe kuwa hawatumii nguvu kupita kiasi. Wao wenyewe wanatambua vyema maana yake.  Wanapofanya kinyume chake na ikathibitika hivyo nao pia huchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Haipendezi mbele ya macho na mioyo ya askari wetu lakini lisilobudi, hutendwa," alisema Rais Kikwete.

http://wotepamoja.com/archives/7909#.UGswhmEO3JQ.gmail
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment