Monday, 27 January 2014

Re: [wanabidii] VYAMA VYA SIASA VINAPIGA TEKE MASLAHI YA UMMA!

Hotuba ndefu majibu ni sentensi moja. "Tatizo ni Katiba na sheria mbovu"


Send from Samsung Mobile



-------- Original message --------
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Date:
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] VYAMA VYA SIASA VINAPIGA TEKE MASLAHI YA UMMA!


By Faridi Abdalla Ze Prudent

VYAMA VYA SIASA VINAPIGA TEKE MASLAHI YA UMMA!

Hakika kujikwaa ni jambo la bahati mbaya kwa mtembezi aliye makini na ni jambo la kawaida kwa mtembezi asiye makini!

Na ni mtembezi makini pekee ambaye atathubutu kujiuliza pale atakakapokuwa amejikwaa, yule asiyekuwa makini hatojiuliza kamwe.

Tangu kuingia kwa muhula wa pili wa Serikali ya awamu ya nne, Watanzania wameshuhudia matukio ya kushtusha mno ndani ya vyama vya siasa.

Vyama vya siasa vimekuwa vikitoa maamuzi ambayo yamekuwa yakivuruga maslahi ya wananchi wapiga na kuacha sononeko kwa umma.

Taasisi hizi zimekuwa zikithubutu kuwavua uanachama wawakilishi halali wa wananchi, na ni wawakilishi ambao wamepigiwa kura kutetea wanyonge nchini.

Maamuzi ya vyama hivi huweka kando maslahi ya umma na badala yake hutekeleza maslahi ya watu wachache.

Viongozi wa vyama hivi hufikiria nini wakati wanapotoa adhabu za kuwavua uanachama wawakilishi halali wa umma?

Matukio haya ya kusikitisha yameshuhudiwa yakitekelezwa na vyama kadhaa vikiwemo NCCR-Mageuzi, Chama cha Wananchi CUF pamoja na Chama cha Mapinduzi CCM.

Mwaka 2011, chama cha NCCR Mageuzi kilithubutu kumvua uanachama Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini Mheshimiwa David Kafulila.

Kafulila aliamua kufungua kesi Mahakama Kuu kuzuia uamuzi huo wa chama chake.

Mwanzoni mwa mwaka 2012, mwakilishi wa jimbo la Wawi, Mheshimiwa Hamad Rashid alifukuzwa uanachama na chama chake cha CUF.

Hamad Rashid naye hakuridhishwa na uamuzi wa wana CUF, akafungua kesi Mahakama Kuu kuzuia uamuzi huo.

Kafulila na Hamad Rashid wakapachikwa jina la "wabunge wa mahakama" na baadhi ya vyombo vya habari!

Hata wanahabari walijisahau kuwa David Kafulila na Hamad Rashid ni wawakilishi halali walioshinda kwa kura halali za Watanzania wanyonge ili wakawalishe maslahi na matakwa ya kundi hili kubwa linaloishi katika maisha duni hapa nchini.

Mikasa ya vyama hivi haikuishia hapo, Agosti 2013 Chama cha Mapinduzi kilimtimua Mansour Yusuf Himid, mwakilishi wa jimbo la Kiembe Samaki, kutokana na kutofautiana na chama chake katika suala la muundo wa serikali katika Jamhuri ya Mungano.

Na hivi karibuni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mheshimiwa Zitto Kabwe (CHADEMA) ametakiwa kujitetea kwanini asifukuzwe chamani na Kamati Kuu ya chama chake!

Suala la Zitto lina sura ileile ya ubabe wa vyama vya siasa katika kuyaendea maslahi ya umma.

Wakati maamuzi haya yakifanywa, umma mkubwa wa wanyonge ambao ulitumia muda wake kufanya maamuzi sahihi kuwachagua wawakilishi wao unapuuzwa na hakuna hata anayethubutu kuutetea!

Je, kwanini watoa maamuzi ya namna hii wanapigiga teke kiholela maslahi ya umma?

Kwanini wanawaacha kando watu muhimu zaidi kwa uwepo wao? Au wamesahau kusudi la uwepo wao?

Kuna haja kubwa kwa Kamati Kuu pamoja na Baraza Kuu la kila chama kutathmini maamuzi yao dhidi ya matakwa ya umma.

Kuna haja ya kujisahihisha ili kufikia lengo la kutetea maslahi ya umma na kuleta maendeleo nchini.

Kujiuliza baada ya kujikwaa ni hekima kubwa! Tujiulize na tubadilike.

Mabadiliko ni mimi, wewe na yule: pamoja tunaweza!
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment