Monday, 25 February 2013

[wanabidii] Habari ya michezo frm Thehabari.com-TFF

Serikali Yaishukia TFF, Yazuia Katiba Mpya Kutumika

Na Thehabari.com

SERIKALI imeingilia suala la uchaguzi wa Shirikisho la

Michezo nchini Tanzania (TFF) na kuamua kuifuta katiba

ya shirikisho hilo inayotumiza hivi sasa ambayo

ilirekebishwa mwaka jana (2012) pamoja na kuagiza

ifuatwe katiba ya awali ya mwaka 2006.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Habari, Vijana,

Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara

akuzungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam na

kuitaka TFF iitishe Mkutano Mkuu kama inataka kufanya

marekebisho ya Katiba yake.

Katika ufafanuzi wake Dk. Mukangara ameagiza TFF

kufuata sheria na Kanuni za Baraza la Michezo Tanzania

(BMT) ikiwa inataka kufanya marekebisho ya katiba

yake.

"Naelekeza na ifahamike kuwa hakuna chama chochote cha

michezo nchini kilicho juu ya BMT. TFF wafanye

uchaguzi wa viongozi kwa mujibu wa Katiba ya TFF ya

mwaka 2006 kwa kuzingatia sheria na kanuni za baraza

la michezo la Taifa," alisema Dk. Mukangara.

Akifafanua zaidi Dk. Mukangara alisema baada ya wataala kupewa kazi yakuangalia mchakato wa mabadiliko ya katiba ya TFF na mgogoro wa uchaguzi unaoendelea, wizara imebaini; sheria Na. 12 ya BMT na marekebisho yake Na. 6 ya mwaka 1971, pamoja na kanuni za BMT za usajili Na. 442 za mwaka 1999 zimekiukwa.

"...Ha kanuni ya BMT Na. 11(1) inayoeleza wazi utaratibu wa marekebisho ya katiba; 'haukufuatwa'. Kimsingi TFF walitakiwa wajaze fomu Na. 6, 7, 8 na 9 kwa mujibu wa sheria na kanuni za BMT. Sasa TFF hawakufuata taratibu nilizozielekeza kwa mujibu wa sheria na kanuni za BMT," alisema Waziri huyo mwenye dhamana ya Michezo Tanzania.

Aidha Serikali imeitaka TFF na Msajili wa Michezo Tanzania kuwajulisha FIFA ambao walikuwa wameingilia mgogoro huo uamuzi uliofikiwa na Serikali ili nao wajue kinachoendelea kwa sasa.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com


--
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment