Kikweli-huu udini upo toka wengine tunazaliwa. Kikwete anaonya Kikweli si CCM inaoueneza na Wasira kasema jambo la kweli ambalo utamaduni wetu uliuweka toka zama hizo ili kutumisha maisha ya amani kwa madhehebu mbalimbali kwani tunaishi kwa kuchanganyika. Hata kule ambapo wakichinja na kupika nyamba ya mbuzi au ng'ombe ambapo wao KIMILA hawasafishi utumbo kuondoa kinyesi ndani (Kichuri), kama kuna wageni-huwaandalia chakula cha kusafisha utumbo ukawa msafi na kumtumia mwalimu au mpishi hodari kutayarisha chakula ambacho wageni hao watakula. Kuichoma nyama ikaiva sio ile mbichi yenye damudamu ambao wao ndio wanapendelea kula sio ya kukaushwa sana. Desturi hizi unwritten tumehiwekea. Ninaomba kukumbusha historia ninayoifahamu na ni ya kweli. Kanisa la ZNZ la kikatoliki lilikuwa la kwanza kujengwa East and Central Africa sasa limetimiza miaka 150 hivi. Hili lilijengwa wakati wazungu wakikomboa watumwa ili wapate kutawala na kupata uchumi wa nchi zetu. Wakabatizwa walioingia ukristu, wakalelewa na kanisa. Hata waliokuwa hawakuingia ukristu walipata msaada. Kanisa lilihamishiwa Bagamoyo na baadhi ya watumwa kuhamishiwa Bagamoyo 1868. Sababu kubwa ilikuwa UDINIi. Kulianza vurugu/mchafuko kati ya Sultani na Uislamu na Ukristu ulioingia. Udini huu ulikuwa mkubwa sana Bagamoyo kwa ushahidi wapo mapadri waliofundisha seminary ya kwanza ya Bagamoyo ambayo imehamishiwa Morogoro baada ya Serikali kuchukua mali za kanisa na kuweka chuo cha ualimu MANTEP ambacho sasa ni Agency. Waislamu wakiingia kanisani kufanya fujo. Hii imeendelea maisha na kwa sasa kutumia walinzi wa makampuni zamani kuomba polisi kuwepo kanisani siku za sikukuu kama Kristmas na Pasaka. Wakiingia kupika kelele, kutukana na kusema 'Yesu si Mungu, Allah wa kbar' (whatever the name is). Wakristu wamekuwa wajinga-wakimya, hata siku moja hawajawahi kuvamia ndani ya msikiti kufanya fujo na wala kuchoma misikiti. Ukimya na ujinga huu una maana. Kama ni kusimama kulipa kisasi, nchi haitokalika. Bora kuwa mjinga uwe na amani kuliko ujanja na kisasi uwe mtumwa daima wa kuhamahama na kupoteza familia, kukatwa mikono, kubakwa na mateso mengine. Kanisa la Bagamoyo lilikuwa na makazi ya wakoma (Ukoma), Jumba la watoto Yatima ambalo liliweka wenye matatizo ya ngozi (Zeruzeru) ambao walitupwa au kuuawa wako wakiokotwa na kulelewa hapo. Kambi ya wazee ambao walikuwa watumwa wamezeeka hawana ndugu. Picha zao zipo makumbusho hapo ya kanisa na hawa walitoka nchi mbali mbali. katika kusaidia masikini kwa chakula au nguo-kanisa halikuchagua dini mtaani au waendao kuomba msaada. Kulikuwa na mechanical na carpentry workshop ambako watu walipata mafunzo; zizi na la ng'ombe wakifugwa kisasa na watu wakichunga na josho lake lipo hadi leo, Zahanati ya matibabu ambayo imerejeshwa na matibabu kwa watu wa dini zote. Huko bagamoyo kuna ushahidi ambapo mtu akihasi dini mkristu kuingia uislamu-alikuwa akipewa hela. Lakini akihasi muislamu kuingia ukistu kuolewa au ameamua tu-alikosa amani na pakuishi ilikuwa vita-aliipata. Na hii ipo nchi kama Misri. Mkristu kupata ajira-usitegemee labda ujiajiri; ukiolewa na muislamu ukihasi dini marufuku kurudia dini yako-unanyongwa ukirudia dini yako. Nilifika Cairo nikafahamishwa haya na watu wa huko. Huku TZ watu hufuata hela/mshiko leo kaingia huku kesho kule mara kaokoka kaingia kanisa fulani kama kuna mikopo au kiimani hasa au kaanzisha kanisa na kukusanya mihela- hakieleweki. Uhuru wa dini upo lakini ubaguzi-wakristu wanaonewa ila umefika muda nao wanaamka. Wamechoka kuchomewa makanisa hata kama maandamano na matatizo ni ya kisiasa au yako binafsi lakini adui anakuwa-Mkristu na Padri na kanisa lake. Ninawafahamu kwa majina watu wazima walioteseka hivyo ktk kurudia dini yao ya kikristu wakahasi, wamezeeka wanataka kurudi ukristu-anaona bora afe ktk dini yake ya zamani akapata sulubu na kufuatwa kutolewa kanisani na waliokuwa wakisali nae msikitini alipohasi. Huyu alikuwa baba wa ndugu yangu. Kwa wanafunzi waliosoma shule za serikali Bagamoyo-mfano Mwambao Primary School iliyo karibu na Majamat na Misikiti kabibu na Pwani, siku za sikukuu walikuwa wanapelekwa kula pilau/ubwabwa msikitini na Jamatini. Foleni mstari kuelekea huko wasichana kwao na wavulana kwao, mtu hawezi kugeuka uwe wa dini ya kikristu au kiislamu. Ilikuwa kama lazima hivi. Marashi yakipita wote mnayapata matone yake. haikuwa hivi ktk shule za kikristu ila zilikuwa na kusali darasani ambapo kila mwalimu akiingia anasalisha na waislamu wote walijua kusali kikristu (baba yetu, salam Maria) lakini wao hukaa chini wakristu wanaposimama darasani kusali. Kwa sasa, hasa vijana (Youths) hawajali dini, wao wakiona kifo/mazishi wanachoangalia ni mlo/ubwabwa na wanaomba masufuria wakwangue na wakoshe vyombo. Watakuwepo mpaka msiba uishe. Hawajali dini wao hata kama mnyama kanyongwa wao ni ganga njaa tu. Zamani, daima waislamu wakiitwa kuchinja nyama kwa mkristu kuwapo na sherehe maana ktk ujirani hakukua na fujo watu waliishi kwa usalama na walichangia sherehe, mazishi na mengineo. Lakini ktk ujumla kulikuwa na ushabiki wa kidini ambao hao wa jazba wachache walileta vurugu. Shule za GVT wakristu wakivutwa magauni yao na kutiwa madukuo ya kichwa na watoto wa kiislamu wakiitwa-makombo ya masea na wala nguruwe. Shule za GVt in 1960s-1970s ndio zilizokuwa na waislamu wengi katika wanafunzi 100 kwa mfano 15 tu ndio walikuwa wakristu kutokana na wao kusoma shule za kanisa. Kikwete na CCM wasilaumiwe kuleta udini, huu upo na malalamiko ya kusema waislamu wanaonewa-Baba wa Taifa alitaifisha shule za Makanisa kuweka usawa. Sasa ni Uchumi binafsi, huria na private sector inanguvu ya kujiendesha-Makanisa yapo juu na mashule na vyuo vya kila aina. Hakuna anayezuia mashirika ya dini nyingine mfano Waislamu, wasijichangishe kanisani kama wachangavyo wakristu michango iumizayo kujenga nursery schools, na aina nyingine za taasisi za elimu. Ukijenga msikiti-weka na shule ya vidudu sio madrasa tu. Tuliosoma nao sisi wazee huko nyuma shulea za kanisa-walipomaliza std 4 au 7 waliolewa. Na wakati huo sifa kuolewa na mwalimu wa madrasa, sharif, sheikh au mtu ktk ukoo wake. Wachache sana 2 ktk mia ya wasichana waliruhusiwa kwenda secondary-waliozwa. Kanisa lilikuja na Elimu Dunia. Padri ni msomi, ni padri na mwalimu na anajua lugha zaidi ya kiswahili-kiingereza, Kilatini, Kifaransa na huyo ni padri mwafrika wa TZ-amesoma. Jee huko nyuma miaka 1960-1970 mwalimu wa madrasa au sheikh anaelimu gani na ujuzi gani? Kwa sasa wamwsoma lakini muhimu kule ambapo Waislamu ni wengi mfano coastal areas (Mafia, Rufiji, Lindi, Mtwara, Saadan, Pangani etc) elimu dunia ikazaniwe. Unguja na Pemba walikuwa na english medium school wakati wa ukoloni wa uingereza. Baada ya Uhuru waliingia Kiswahili na uswahili. Somesheni kama walivyosoma Wamisri badala ya malalamiko ya kuonewa huku unamuoza mwenyewe mtoto na hukazanii Elimu Dunia na skills za kupata ajira. Tanzania bara wafugaji wanaozurura na mifugo watoto hawasomi na baadhi yao wanawaoza umri mdogo-kisha wanalalamika kutokupata huduma na kujaliwa kielimu. Alichosema WASIRA sahihi na hii ndivyo ilivyokuwa toka zama hizo ili kuondoa mtafaruku wa kidini nchini. waacheni Waislamu wachinje kunapokuwa na sherehe za michanganyiko ya dini (wakristu tuendelee kuwa wavumilivu) na wachinje ktk bucha za umma au serikali-kwani haitotubadili Imani yetu wala ujirani wetu. Unapokula mwenyewe home-nyoga mnyama wako. akija muislamu au mtu wa dini ingine-atakula akiwa na njaa yake bila kuhoji. Mbona wapo waislamu wanywao gongo vibaya sana, walao kitimoto, kubwia unga au madawa ya kulevya na bhangi; wapo waliowapangia vyumba mashoga; majambazi na mengine mengi kama walivyo watu katika dini nyingine. Sasa inapokuja vurugu ya -Kuchoma makanisa hakieleweki; kuingiza Udini katika masuala mengi ambapo watendaji ni sisi wenyewe ambapo hatuweki kipaumbele ktka maisha yetu-Elimu dunia kwa watoto; nafasi za uongozi ambapo etc na madai mengine Ndipo KIkwete akasema-Someni/Somesheni msilalamike tu. Maonyo yake sio mabaya. Jitumeni fanyeni kazi kwa bidii msikae barazani tu. Wacheni wizi mkiajiriwa mahotelini-hamtapata ajira hata kama mahoteli hayo yapo makwenu huku pwani na kwingineko. Sio Udini-Tabia yenu. Msimuongopee yapo TZ. Kukemea ni muhimu kwa sababu yanageuka kuwa uonevu na kutengwa kiudini kumbe SIO. Tukubali ukweli wa kubadilika. Tuangalie matatizo yetu scientifically na kuyatatua kiukweli badala ya kutafuta popular politics ya kukuza jina au vyama vyetu. Tuangalie usalama, mahitaji ya raia na maendeleo endelevu ya kweli. --- On Fri, 1/2/13, Solomon Msomba <msomba2000@yahoo.com> wrote:
|
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment