Tuesday, 12 July 2016

[wanabidii]

1. Kwanini kada yeyote wa CCM, anayejiona maarufu kisiasa, anapoamua kuhamia upinzani, anawadharau viongozi wote wa vyama vya upinzani?

2. Kwanini katika dharau hiyo, kada wahuyo wa CCM anapoamua kuhamia upinzani, yeye ndiye hujiona pekee alfa na omega, kwa kutoa masharti ambayo kila kiongozi wa upinzani lazima ayatii na kuyatekeleza?

3. Kwanini makada hao wa CCM, wakishajiunga na upinzani, hawataki kusikia tena wala kuheshimu dhana nzima ya demokrasia, bali demokrasia inapaswa kufata mawazo yao?

4. Kwanini kila kada wa CCM anayejiona ni maarufu wa kisiasa, kila anapoamua kuhamia upinzani, basi anataka ajimilikishe yeye miaka yote nafasi ya urais hadi kifo?

5. Kwanini kila kada wa CCM, anayejiona maarufu akihamia upinzani anadai kwamba huko aliotoka CCM amekimbia kwa kuwa hakuna demokrasia, lakini akikaribishwa na kupewa fursa kanuni na misingi ya demokrasia inakuwa kazi ngumu kwake, hivyo hutaka yeye kuwa alfa na omega?

6. Kwanini vyama vyote vikubwa vya upinzani hapa nchini, vilivyokubali kuwapokea makada maarufu wa CCM na kuwafanya kuwa wagombea wao wa urais mfano vyama vya NCCR Mageuzi, TLP vya mlema, hatma ya vyama hivyo inakuwa kupotea katika ramani siasa nchini kama inavyoelekea kuwa hivyo kwa Chadema muda mchache ujao baada ya kumpokea Lowassa?

Wadau ili kujua ninachomaanisha angalia ujio wa Mrema alipojiunga na NCCR Mageuzi 1995 na Mafuriko yake yanavyofanana na Ujio Lowassa alipojiunga Chadema 2015 na mafuriko yake hali ya kuwa wote wawili ni zao la CCM, Walilelewa na kujengwa kisiasa na CCM na wote wawili waliingiwa na mdudu wa tamaa , anayetamani kweli kweli nafasi ya urais.
 

0 comments:

Post a Comment