Thursday 14 July 2016

[wanabidii] Taarifa kwa umma

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO







TAARIFA KWA UMMA
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na Uvumi katika Mitandao ya Kijamii kuwa Serikali imeamua kushusha Mishahara ya Madaktari kwa asilimia 30% ili kuendana na dhana ya Hapa kazi tu na kuwa Serikali imekusudia kufuta malipo ya Posho za Wataalamu wa Afya walio katika Mafunzo kwa Vitendo ufafanuzi kwa Umma wa Watanzania na Watumishi wa Sekta ya Afya kuwa taarifa hizo siyo za kweli.
Taarifa aliyoitoa Katibu Mkuu (Afya) alipokuwa anaongea na Watumishi wa Hospitali ya Bugando ililenga kutoa ufafanuzi kwa Watumishi wa Hospitali hiyo kuhusu kufutwa kwa kibali cha Msajili wa Hazina kilichowawezesha watumishi wa Hospitali hiyo kulipwa Mishahara ya Taasisi zilizo chini ya Msajili wa Hazina tangu mwaka 2012.
Uamuzi huo wa Msajili wa Hazina unatokana na ukweli kwamba Hospitali ya Bugando siyo Shirika la Umma na hivyo wanastahili kulipwa mishahara sawa na watumishi wengine wa Serikali Kuu kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo kati ya Serikali na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambao ndio wamiliki wa Hospitali ya Bugando.
Aidha, ieleweke kuwa mishahara ya Watumishi wa Sekta ya Afya haizingatii ngazi ya Vituo vya kutolea huduma kama vile Zahanati, Kituo cha Afya, Hospitali, au Hospitali za Rufaa bali huzingatia uzito wa kazi na majukumu ya kada husika. Hivyo, mshahara wa Daktari wa Hospitali ya Wilaya ni sawa na ule wa Hospitali ya Rufaa ngazi ya Mkoa na Hospitali ya Rufaa ya Kanda.
Kutokana na maelezo haya, uamuzi huo wa Msajili wa Hazina utaihusu Hospitali ya Bugando pekee na siyo Hospitali zote za Kanda kwa kuwa dosari hiyo haikutokea katika Hospitali nyingine za Kanda.
Kuhusu ajira mpya kwa mwaka 2015/2016 ufafanuzi ulitolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba hakutakuwa na ajira mpya hadi hapo Zoezi la Uhakiki wa Watumishi Serikalini litakapokamilika. Hivyo, vibali vya ajira vilivyokuwa vimetolewa vimefutwa hadi hapo itakapotamkwa vinginevyo.
Kadhalika, kumekuwa na Uvumi kuwa Serikali inakusudia kufuta posho ya 'Interns' kuanzia mwaka huu wa fedha. Taarifa hii pia siyo sahihi kwa kuwa hakuna chombo chochote cha Serikali ambacho kimetoa maamuzi hayo.
Wizara inasisitiza kuwa maamuzi ya Serikali hutolewa na Mamlaka husika kwa nyaraka. Hivyo, watumishi wa Sekta ya Afya na wananchi kwa ujumla wanaaswa kuzingatia taarifa zinazotolewa na Mamlaka za Serikali kuhusu Masuala yanayowahusu ambayo mara nyingi hutolewa kwa nyaraka badala ya Mitandao ya kijamii,

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Afya
14 Julai, 2016















Sent from my Huawei Mobile

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment