Tuesday 12 July 2016

Re: [wanabidii]

Mpombe, Mrema hakuwahi kuwa kada wa CCM ila alikuwa mwanachama wa kawaida kama nilikuwa mimi. Mrema alipata bahati ya kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nafasi aliyoitumia vizuri kujitafutia umaarufu. Tofauti na Lowasa aliyekuwa waziri kwa muda mrefu sana. CCM ilikuwa na utaratibu wa kuwatengeneza makada kupitia chuo cha chama Kovukoni sasa Mwl Nyerere University. Vijana wengi wasiojua historia ya chama wanadhani mtindo huu ndiyo utaratibu wa chama. CCM ulikuwa na utaratibu wa kusomesha watu miezi mitatu kabla ya kuwapa kadi. Vyama vya upinzani vilianzishwa na watu makini vikazoa ovyo.
Lazima vijifunze makosa yao kwanza ndipo vitaweza kushindana kweli. Kama wakiendelea kuokota makapi kama Nape alivyopata kuwaambia vitapotea



On Tue, 12 Jul, 2016 at 19:57, 'mpombe mtalika' via Wanabidii
<wanabidii@googlegroups.com> wrote:
1. Kwanini kada yeyote wa CCM, anayejiona maarufu kisiasa, anapoamua kuhamia upinzani, anawadharau viongozi wote wa vyama vya upinzani?

2. Kwanini katika dharau hiyo, kada wahuyo wa CCM anapoamua kuhamia upinzani, yeye ndiye hujiona pekee alfa na omega, kwa kutoa masharti ambayo kila kiongozi wa upinzani lazima ayatii na kuyatekeleza?

3. Kwanini makada hao wa CCM, wakishajiunga na upinzani, hawataki kusikia tena wala kuheshimu dhana nzima ya demokrasia, bali demokrasia inapaswa kufata mawazo yao?

4. Kwanini kila kada wa CCM anayejiona ni maarufu wa kisiasa, kila anapoamua kuhamia upinzani, basi anataka ajimilikishe yeye miaka yote nafasi ya urais hadi kifo?

5. Kwanini kila kada wa CCM, anayejiona maarufu akihamia upinzani anadai kwamba huko aliotoka CCM amekimbia kwa kuwa hakuna demokrasia, lakini akikaribishwa na kupewa fursa kanuni na misingi ya demokrasia inakuwa kazi ngumu kwake, hivyo hutaka yeye kuwa alfa na omega?

6. Kwanini vyama vyote vikubwa vya upinzani hapa nchini, vilivyokubali kuwapokea makada maarufu wa CCM na kuwafanya kuwa wagombea wao wa urais mfano vyama vya NCCR Mageuzi, TLP vya mlema, hatma ya vyama hivyo inakuwa kupotea katika ramani siasa nchini kama inavyoelekea kuwa hivyo kwa Chadema muda mchache ujao baada ya kumpokea Lowassa?

Wadau ili kujua ninachomaanisha angalia ujio wa Mrema alipojiunga na NCCR Mageuzi 1995 na Mafuriko yake yanavyofanana na Ujio Lowassa alipojiunga Chadema 2015 na mafuriko yake hali ya kuwa wote wawili ni zao la CCM, Walilelewa na kujengwa kisiasa na CCM na wote wawili waliingiwa na mdudu wa tamaa , anayetamani kweli kweli nafasi ya urais.
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment