Thursday 14 July 2016

Re: [wanabidii] Taarifa kwa umma

Na waliozusha nao ni mchango wao katika kuleta maendeleo ya Taifa letu na kuleta umoja wa taifa hili. Tunao kwenye jamii na hatuna pa kuwafungia
--------------------------------------------
On Thu, 7/14/16, 'cathysungura@yahoo.com' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Taarifa kwa umma
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, July 14, 2016, 5:52 PM


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA
WATOTO             
               
               
               
         

           


               

               
           
   

TAARIFA KWA UMMA
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na Uvumi katika
Mitandao ya Kijamii kuwa Serikali imeamua kushusha Mishahara
ya Madaktari kwa asilimia 30% ili kuendana na dhana ya Hapa
kazi tu na kuwa Serikali   imekusudia kufuta
malipo ya Posho za Wataalamu wa Afya walio katika Mafunzo
kwa Vitendo ufafanuzi kwa Umma wa Watanzania na Watumishi wa
Sekta ya Afya kuwa taarifa hizo siyo za kweli.
Taarifa aliyoitoa Katibu Mkuu (Afya) alipokuwa anaongea na
Watumishi wa  Hospitali ya Bugando  ililenga kutoa
ufafanuzi kwa Watumishi wa Hospitali hiyo kuhusu kufutwa kwa
kibali cha Msajili wa Hazina kilichowawezesha 
watumishi wa Hospitali hiyo kulipwa Mishahara ya Taasisi
zilizo chini ya Msajili wa Hazina tangu mwaka 2012.
Uamuzi huo wa Msajili wa Hazina unatokana na ukweli kwamba
Hospitali ya Bugando siyo Shirika la Umma na hivyo
wanastahili kulipwa mishahara sawa na watumishi wengine wa
Serikali Kuu kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo kati ya
Serikali na Baraza  la Maaskofu Tanzania  (TEC)
ambao ndio wamiliki wa Hospitali ya Bugando.
Aidha, ieleweke kuwa mishahara ya Watumishi wa Sekta ya Afya
haizingatii ngazi ya Vituo vya kutolea huduma kama vile
Zahanati, Kituo cha Afya, Hospitali, au Hospitali za Rufaa
bali huzingatia uzito wa kazi na majukumu ya kada husika.
Hivyo, mshahara wa Daktari wa Hospitali ya Wilaya ni sawa na
ule wa Hospitali ya Rufaa ngazi ya Mkoa na Hospitali ya
Rufaa ya Kanda.
Kutokana na maelezo haya, uamuzi huo wa Msajili wa Hazina
utaihusu Hospitali ya Bugando pekee na siyo Hospitali zote
za Kanda kwa kuwa dosari hiyo haikutokea katika Hospitali
nyingine za Kanda.
Kuhusu ajira mpya kwa mwaka 2015/2016 ufafanuzi ulitolewa na
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba
hakutakuwa na ajira mpya hadi hapo Zoezi la Uhakiki wa
Watumishi Serikalini litakapokamilika.  Hivyo, vibali
vya ajira vilivyokuwa vimetolewa vimefutwa hadi hapo
itakapotamkwa vinginevyo.
Kadhalika, kumekuwa na Uvumi kuwa Serikali inakusudia kufuta
posho ya 'Interns' kuanzia mwaka huu wa fedha. 
Taarifa hii pia siyo sahihi kwa kuwa hakuna chombo chochote
cha Serikali ambacho kimetoa maamuzi hayo.
Wizara inasisitiza kuwa maamuzi ya Serikali hutolewa na
Mamlaka husika  kwa nyaraka. Hivyo, watumishi wa Sekta
ya Afya na wananchi kwa ujumla wanaaswa kuzingatia taarifa
zinazotolewa na Mamlaka za Serikali kuhusu Masuala
yanayowahusu ambayo mara nyingi hutolewa kwa nyaraka badala
ya Mitandao ya kijamii,

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Afya
14 Julai, 2016











     



Sent from my Huawei Mobile

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment