Tuesday 12 July 2016

Re: [wanabidii] Niliyoyaona bungeni: Jeuri ni kigingi cha demokrasia ya kweli

Niipofika kwenye jumba la makumbusho ya Abraham Lincoln nilinunua kitabu kinachoelezea jinsi alivyolitandika kijeshi moja kati ya majimbo lililotaka kujitenga. Wananchi wake walikuwa wanataka kujitenga na USA. Akaamua kuwatandika mpaka akawashinda. Na hiyo haikuwa matakwa ya wananchi. Alipinga lililokuwa ''kwa ajili ya wananchi''. Ndivyo siasa zilivyo. Ndivyo demokrasia zilivyo. hayanyooki yote.
--------------------------------------------
On Tue, 7/12/16, fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Niliyoyaona bungeni: Jeuri ni kigingi cha demokrasia ya kweli
To: "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, July 12, 2016, 12:39 PM

RAIS wa Marekani,
Abraham Lincoln (1809-1865) anapozungumza kuhusu
demokrasia anasema ni serikali ya wananchi inayoendeshwa na
wananchi kwa
ajili ya wananchi.

Na hii serikali inapatikana kupitia uchaguzi. Lakini
pamoja na
maelezo hayo, anakiri kwamba mifumo ya demokrasia ni moja ya
changamoto
kubwa ya uendeshaji wa jamii katika dunia ya sasa kutokana
na ukweli
kuwa maana hii ya uendeshaji bado ina utata kwa wanasiasa na
hata
wananchi pia kwa kuzingatia mahitaji ya kundi linalotaka
kutawala wakati
huo na changamoto zinazokabili ustawi wa jamii. Demokrasia
imeasisiwa
na Wagiriki ambao mfumo wao wa kutawala ulikuwa ni utawala
wa watu wa
kawaida.
Ukiangalia uhalisi wake, demokrasia ya sasa imechukua
makandokando
mengi ya demokrasia ya Wagiriki iliyokuwa inafanya kazi
katika miji ya
Rome na Athens. Demokrasi ya Wagiriki kama ilivyo ya sasa
ilitengenezwa
kwa namna ya kukabiliana na matumizi mabaya ya madaraka
yanayofanywa na
watawala au wale waliopata mamlaka.
Pamoja na ukweli huo demokrasia ambayo tunayo sasa
ilianza kuwa na
mfumo unaoeleweka na wenye kupanuka zaidi katika karne ya 17
na 18
wakati wanafalsafa walipoanza kutoa nadharia zake na tafsiri
zake pamoja
na misingi yake, katika masuala ya mgawanyiko wa madaraka
miongoni mwa
vyombo vya dola, haki za msingi za binadamu, uhuru wa
kuabudu na kuanza
kutofautishwa kwa kanisa na mamlaka ya nchi.
Ikumbukwe kuwa katika siku hizo Kanisa lilikuwa kama ndio
watawala
katika bara la Ulaya kwani yanayofanyika serikalini yalikuwa
na baraka
za moja kwa moja na kanisa na taratibu za kanisa ndio
zilizokuwa
zikitumika kutawala. Ukiachia demokrasia ya sasa ambayo
nyingi
inaendeshwa kwa mfumo wa jamhuri, zipo bado nchi zenye aina
nyingine ya
demokrasia ambayo inaendesha utawala. Demokrasia hizo ni
pamoja na
uongozi wa utawala wa kidini, wa kurithi, wa kifalme na hata
wa watu
wachache.
Udikteta unaweza kabisa kuwa ni utawala wa wananchi
kupitia unyakuaji
wa madaraka uliofanywa. Kimsingi demokrasia ina maelezo
mwafaka kwa
kuangalia utamaduni wa mahali, lakini kwa dunia ya sasa wote

tunakubaliana kwamba ilikuwa na demokrasi inayotakiwa ni
lazima kuwepo
na katiba inayofuatwa si tu na viongozi bali na wananchi
pia. Ndani ya
katiba hiyo mgawanyo wa madaraka unaelezwa wazi kati ya
serikali, Bunge
na Mahakama.
Aidha kunakuwapo na ulinzi wa haki za binadamu kwa mtu
mmoja, makundi
na hata kwa serikali yenyewe. Pia demokrasia ya sasa inadai
haki ya
kuzungumza na kupokea taarifa na uhuru wa vyombo vya habari.
Aidha
kunakuwa na haki za kuabudu, kuna uchaguzi unaofanywa kwa
mtu mmoja kura
moja na utawala wa kisheria ambapo rushwa ni kitu
kisichokuwepo.
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Winston Churchill
(1874-1965)
akizungumzia kuhusu demokrasia anasema: "Hakuna mtu ambaye
atasema kwa
kujiamini kwamba demokrasia imetimilika, au ina kila kitu na
ina busara.
Hakika, demokrasia ni aina mbaya kabisa ya kuwa na serikali
isipokuwa
pale tu aina nyingine ya utawala inapokuwa imejaribiwa na
kuonwa shubiri
yake."
Kimsingi, waziri mkuu huyu wa zamani wa Uingereza anataka
kusema
kwamba hakuna aina timilifu ya utawala, yaani serikali
duniani hapa ila
kutafuta nafuu; na demokrasia ya sasa ni nafuu zaidi kwa
kuwa hakuna
nyingine ambayo imebuniwa na kuonekana kufanya kazi kwa
ufanisi zaidi
kuliko hii.
Ukisoma magazeti na mitandao ya kijamii na kuangalia
televisheni na
kusikiliza radio kuhusu mwenendo wa Bunge la Tanzania kwa
mwaka jana na
mwaka huu na vijimambo vya vyama vya upinzani kuhusu
uchaguzi hadi sasa
kuhusu utawala uliopo unaweza kusema kwamba demokrasia
Tanzania
inaminywa: lakini ukiangalia misingi ya demokrasia utaona
kabisa mzizi
wa madai hayo umo katika ubinafsi na jeuri inayoambatana na
kasi ya
kubana waroho, wachoyo wa utajiri na wakwepa kutimiza
wajibu.
Wakati anaahirisha mkutano wa bunge mjini Dodoma wiki
mbili
zilizopita msimamizi mkuu wa shughuli za serikali bungeni,
Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa alisema serikali haijawafunga midomo wabunge
wa upinzani
au mbunge yeyote labda awe amejifunga mwenyewe. Katika
mfumo wa
demokrasia uliojengeka nchini, wabunge ndio wanaofanya
maamuzi muhimu ya
uendeshaji wa nchi na usimamizi wa serikali kwa niaba ya
wananchi
waliowapeleka kwa kuwapigia kura japo si wote.
Na Bunge la Tanzania linaloendeshwa kwa kuzingatia sheria
mama,
Katiba Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uwazi wa
uwakilishi
unaonekana bungeni na si nje ya hapo kwa kuwa ni katika
vikao vya Bunge
tu, mbunge kwa lugha safi anaweza kusahihisha, kukosoa au
kutokukubaliana na serikali, lakini akifanya mambo ambayo
ana kibali
nacho bungeni uraiani hilo linaweza kwenda kuwa kosa la
uchochezi.
Pamoja na watu kuinyambua siasa na demokrasia kwa namna
wanavyotaka
(hata wazungu walioileta) wanazuoni na wadau bado wanaona
uwakilishi na
Bunge si sahihi kutokana na mifumo iliyowekwa na wanaotaka
kututawala-
soma whatisdemocracy. net) sintofahamu iliyojitokeza katika
kipindi cha
Bunge ambapo wabunge wa upinzani walikuwa hawaketi bungeni
inaweza kuwa
na tafsiri mbalimbali.
Moja ya tafsiri ni kwamba upinzani haujakomaa, haujui
maana ya
uwakilishi na haujui haki zao wakiwa bungeni ila wanataka tu
kuleta
hisia na kukwamisha mambo kwa kutaka kuwashirikisha wananchi
kama
ilivyokuwa katika demokrasia changa za Athens na Roma.
Tafsiri nyingine
ni jeuri ya kutaka madaraka na kutojipanga kuibana serikali
kwa kutumia
mifumo iliyopo ambayo ukiwa na akili timamu inaweza kabisa
kuifanya
serikali kusimama makini zaidi.
Mambo yalitokea pale wabunge wa upinzani walipovaa nguo
nyeusi na
kuwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wenye tuhuma nzito
kwa serikali,
hakuoneshi uwakilishi bali nia ya kundi moja kulipiku
jingine ili
kuingia katika utawala kwa kuchochea hisia ambazo si za
kisheria bali
zenye tamaa ya madaraka. Kuna uvunjifu wa sheria katika
hili? Elementi
zinazobeba siasa ndizo zinazotoa nadharia ya mwisho kwamba
vyama vya
siasa lengo lake kubwa ni kushika madaraka na kuongoza
wengine, kinyume
cha hapo ni chama cha burudani.
Na si kila mwananchi atakuwa mwanasiasa lakini wale
wanaotaka
kutekeleza hisia zao walipaswa kuzingatia muda na kujipanga
kuja kueleza
wananchi kwamba wao ndio wenye mfumo mzuri zaidi wa
kuwatawala kuliko
waliopo madarakani lakini si kabla ya kuwabana waliopo humo
kutekeleza
wajibu wao katika dhana nzima ya utawala wa kisheria. Waziri
Mkuu
alisema wakati akihutubia Bunge kwamba wabunge wa upinzani
kwa makusudi
wamekuwa wakijaribu kujenga taswira potofu kwa wananchi na
nje ya nchi
ili ionekane kwamba kuna kuminywa kwa demokrasia.
Wabunge wa upinzani si tu wamekuwa wakitaka kuyumbisha
bali hata
maswali wanayouliza hayakulenga kuibana serikali kutekeleza
wajibu wake
ila kuonesha kwamba inakumbatia upuuzi unaokwamisha
maendeleo. Watu
wenye akili kama alivyosema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
wanaweza kabisa
kuona kelele za wapinzani si za kujenga, bali ni kuonesha
kutokomaa
kwao katika siasa, ambapo maana kubwa ni kutekeleza
demokrasia si kwa
mtindo wao bali kwa mtindo wa dunia wa kusimamia serikali na
kuhakikisha
hakuna rushwa na utawala ni wa kisheria.
Kwa mtu aliyekomaa kisiasa hawezi kukurupuka na kusema
kwamba kuna
udikteta wa kijeshi bali ataangalia kwa nini uvunjifu wa
amani hauwezi
kuachiwa unaendelea kwa sababu za kisiasa na kukwamisha
serikali kufanya
shughuli zake. Kiukweli kama alivyosema Waziri Mkuu katika
hotuba yake
hiyo, si jambo la kawaida kwa mbunge kuzitoa hoja za bungeni
na
kuzipeleka mitaani eti zijadiliwe na wananchi kisha zitolewe
uamuzi.
Uamuzi gani utatolewa na je haki za bunge zinatolewa na
wananchi au
ndio kutaka kuifunga kamba serikali isitekeleze wajibu wake?
Kwangu mimi
(mwandishi) ni matokeo ya kuondolewa kwa Bunge 'Live'
sasa wanaonekana
kwamba hawafanyi kazi kumbe hoja zao za msingi zenye
kusimama thabiti
zingeweza kujadiliwa ndani na wote wakajua kwamba
wanatekeleza wajibu
wao wa kutaka wananchi wawe na ustawi.
Siasa za bungeni za kutoshiriki vikao halali zimetia kiwi
na wenye
akili na maarifa. Ni kweli kama alivyosema Waziri Mkuu
kwamba kama hilo
la wananchi kuamua linawezekana, basi kusingekuwa na umuhimu
wa kuwa na
Bunge, bila shaka na uchaguzi pia.
Kama kweli wanasiasa wetu wanajua demokrasia ya kisasa ni
nini kazi
yake wakitazama msingi mkubwa wa uendeshaji wa serikali na
upigaji vita
rushwa hawawezi kujifunga na vibweka vya nguo nyeusi au
kushona midomo
yao bali wataangalia kila hatua ya demokrasia hapa nchini na
hasa
mapambano dhidi ya rushwa na utawala wa kisheria.
Mbunge anapodai kwamba kashonwa mdomo, anadai kwa kuwa
yeye mwenyewe
kwa kutumia kanuni za kudumu ameshindwa kutengeneza hoja
yenye uhakika
na si kufinyanga maneno kiasi cha kujikuta akikiuka kanuni
zinazoendesha
bunge. Na kutokana na hili unakutana na matatizo ya wabunge
kunasa
katika mchezo wa uwongo na matusi na wakasimamishwa vikao
kwa kuwa
wameenda kinyume.
Kwa kushindwa kutumia vyema Ibara ya 100 na 101 ya Katiba
ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo imetoa haki na
kinga kwa
wabunge ili waweze kujadili na kuhoji utendaji wa serikali
kwa uhuru
bila mashaka yoyote ya kuweza kushtakiwa wanapotimiza wajibu
wao huo
wakiwa bungeni, kumefanya siasa za upinzani kuonekana kuwa
majungu na
fitna na kubaki katika majukwaa ya siasa wakitafuta
'kiki' rahisi ili
wananchi wawaunge mkono.
Ni dhahiri kinga hiyo ya kikatiba haijatolewa kwa
wananchi, kwa
maneno mengine mbunge hajafungwa mdomo labda aamue kujifunga
mdomo
mwenyewe. Ndio kusema kitendo cha baadhi ya wabunge kususa
vikao vya
bunge pamoja na kwamba hakitoi picha nzuri kwa wananchi
waliowachagua
kuwasilisha matatizo yao katika Bunge, na wala hakitokana na
mkutano wa
wanachama wote wa vyama vyao, wanaonesha kiwango cha juu cha
jeuri na
kiburi (arrogance) ambayo hatima yake ni kuididimiza
demokrasia.
Mimi nadhani kama watajitahidi kusoma mifumo mbalimbali
ya demokrasia
na misingi inayobeba demokrasia hiyo na kuelewa kwamba
haijawahi kuwa
timilifu, wabunge wa upinzani watarejea bungeni na kushiriki
kutoa
ushauri kwa serikali bungeni ambao utaliletea taifa
maendeleo, na huko
wananchi wote watawaona watawasikiliza na watawaelewa.
Waziri Mkuu alisema: "Endapo kuna utata katika jambo
lolote ndani ya
Bunge letu, zipo taratibu tulizojiwekea na kanuni za kufuata
ili kupata
ufumbuzi wa jambo hilo. Kwa kususa kuingia bungeni kunaweza
kusiwe tija
kwa tunaowawakilisha na taifa letu." Sasa kama Bunge
linaongozwa na
katiba, sheria na kanuni za kudumu za bunge kwa nini
tutengeneze hisia
za kuonewa wakati tunachapia wenyewe? Kama tukiendekeza
misimamo ya
vyama vya uroho wa madaraka na utawala maendeleo na ustawi
wa jamii
tutausikia katika bomba.
Habari Leo




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment