Sunday, 19 June 2016

Re: [wanabidii] Ukawa wanavyodharau Bunge, Viongozi wake

Kama watanzania wangefanya kosa tarehe 25 October na kukiweka madarakani chama chenye wabunge kama hawa. na hawa wakatokea kuwa mawaziri. Nchi ineelekea wapi. Tunahitaji kujifunza namna nyingine ya kuvilea vyama vya siasa vifikie kuweza kuongoza. CHADEMA iliyokuwa ikiongozwa na Dr. Slaa imeporokoka na kukosa nidhamu kiasi hiki. Tunayo safari na si fupi.
--------------------------------------------
On Sun, 6/19/16, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Ukawa wanavyodharau Bunge, Viongozi wake
To: "ELISA MUHINGO' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, June 19, 2016, 9:40 AM

WAKATI
Bunge likitarajiwa kupitisha Bajeti ya Kwanza ya Serikali ya
Rais
John Magufuli kesho, bila uwepo wa Kambi ya Upinzani,
gazeti hili
limefanya tathmini ya baadhi ya matukio yaliyoanza
kuongezeka
kutoaminiana kati ya kambi hiyo na uongozi wa Bunge, hasa
Naibu Spika,
Dk Tulia Ackson.



Ingawa taarifa nyingi zimekuwa zikieleza kuwa Dk Tulia ndiye
mbabe,
taarifa za uendeshaji wa shughuli za Bunge tangu mwanzoni
mwa mwaka huu,
zinaonesha namna wabunge wa Ukawa, walivyoonesha kutojali
heshima ya
chombo hicho na viongozi wake.



Taarifa hizo za Bunge zilizopitiwa na gazeti hili wiki hii,
zimeonesha
bila kuacha shaka namna baadhi ya wabunge wa kambi hiyo,
wanavyodharau
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mtu yeyote
aliyekalia Kiti
cha Spika, achilia mbali Dk Tulia ambaye ndiye anayetajwa
zaidi kuwa
mbabe.



Mbali na dharau kwa Bunge na viongozi wake, wabunge hao
wameonesha namna
walivyotayari kutumia ubabe ndani ya Bunge ikibidi
kupigana, huku
wengine wakitumia uongo kwa nia ya kuichafua serikali na
viongozi wake
kwa umma.



Dharau za Bulaya



Mbali na matukio ya mara kwa mara na ya kawaida ya wabunge
hao wa Ukawa
kukaidi agizo la kutakiwa kukaa chini au kukaa kimya kutoka
kwa
aliyekalia Kiti cha Spika, ambaye ndiye anakuwa na Mamlaka
ya Spika,
dharau kubwa iliyosikitisha viongozi wa Bunge, ilioneshwa na
Mbunge wa
Bunda Mjini, Esther Bulaya.



Mbunge huyo baada ya kuonekana kushiriki kufanya vurugu
Januari 27, 2016
wakati wabunge hao wa Ukawa walipozuia shughuli za Bunge za
mchana na
jioni kutofanyika kwa kusimama na kupiga kelele mfululizo,
yeye na
watuhumiwa wenzake walitakiwa kufika mbele ya Kamati ya
Haki, Maadili na
Madaraka ya Bunge, kutoa maelezo kuhusu tuhuma zilizokuwa
zikiwakabili.



Watuhumiwa wengine walioitwa mbele ya kamati hiyo Machi 9
mwaka huu, kwa
kutumia hati ya wito yenye nguvu sawa na ya Mahakama, ni
Mbunge wa
Singida Mashariki, Tundu Lissu; Mbunge wa Arusha Mjini,
Godbless Lema na
Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul. Pamoja na
kuthibitisha kuwa
Bulaya na watuhumiwa wenzake walipokea hati hiyo, ni mbunge
huyo pekee
wa Bunda ambaye hakufika na wala hakuona umuhimu wa kutoa
taarifa yoyote
ya kutofika kwake.



Kwa kutumia nguvu ya kisheria ya kamati hiyo ambayo ina
hadhi sawa na ya
kimahakama, Kamati hiyo ililazimika kumwandikia Spika barua
kumjulisha,
kuhusu hatua ya Bulaya kukaidi wito wa kamati.



Kukamatwa kwa Bulaya



Spika wa Bunge, Job Ndugai, hakuwa na namna bali kutoa
kibali chake cha
kukamatwa kwa Bulaya, kilichokabidhiwa kwa Inspekta Jenerali
wa Polisi
(IGP) na polisi walifanya kazi yao, walimkamata Mbunge huyo
akiwa katika
Hoteli ya Gold Crest, Mwanza.



Akiwa chini ya ulinzi wa Polisi, Bulaya alipandishwa ndege
na kupelekwa
jijini Dar es Salaam Machi 11, 2016 kwenda kujibu tuhuma
zilizokuwa
zikimkabili.



Utetezi wa Bulaya



Taarifa za Bunge zinaonesha Bulaya alipewa fursa ya
kujitetea kwa nini
hakutii wito wa Kamati ya Bunge, kama walivyofanya
watuhumiwa wenzake
ambao nao ni wabunge kama yeye, ambapo mbunge huyo alitoa
utetezi wa
aina mbili uliokuwa ukipingana.



Kwanza Bulaya alidai kuwa alikuwa anaumwa na kwamba kwake
yeye suala la
afya yake, lilikuwa muhimu zaidi kuliko kutii wito huo wa
kamati. Katika
utetezi wa pili alioutoa baada ya Kamati hiyo kumdadisi,
alijikuta
akiacha hoja ya ugonjwa na kukiri kuwa alikuwa Mwanza
kuhudhuria mkutano
wa Kamati Kuu ya Chadema, kama mjumbe mwalikwa.



"Kamati ilisikitishwa na kitendo cha Mheshimiwa Bulaya
kudharau wito wa
Kamati," taarifa rasmi za Bunge zimemnukuu Mwenyekiti wa
Kamati hiyo,
Mbunge wa Newala, George Mkuchika (CCM).



Dharau zaidi, busara ya Bunge Pamoja na Lema, Lissu na Gekul
kutii wito
wa kwanza ambao Bulaya alikaidi, katika tukio lililoonesha
dharau
nyingine kwa Bunge, ni pale wabunge hao waliotii wito wa
kwanza
walipoomba kupewa muda ili washauriane na mawakili wao,
kabla ya kujibu
tuhuma zilizokuwa zikiwakabili.



Kwa busara, Kamati hiyo iliamua kuwapa wabunge hao haki yao
ya
kusikilizwa iliyotimia kwa kuwapa muda wa siku mbili zaidi,
ili
wawasiliane na kupata ushauri wa mawakili ambapo walitakiwa
kurudi
katika Kamati Machi 11, 2016 ili kujibu tuhuma zao baada ya
kupata
ushauri wa mawakili.



"Kamati iliamua kutoa fursa kwa mashahidi walioomba kupewa
fursa ya
kupata mawakili. Mashahidi hao ni Tundu Lisu, Godbless Lema
na Pauline
Gekul. Kamati iliwapa muda wa siku mbili toka Machi 9 hadi
Machi 11,
2016 ili kuwawezesha kupata mawakili kama walivyoomba,"
ilieleza taarifa
hiyo ya Bunge.



Katika tukio linaloonesha dharau 'iliyopangwa' kwa
Bunge, wabunge hao
watatu waliamua kutofika kati tarehe waliyokubaliana kuwa
wangefika
mbele ya Kamati na hawakuwahi kuwasilisha maelezo yoyote
mbele ya
Kamati, kuhusu sababu za kushindwa kufika.



Busara ya Kamati hiyo, haikuelekeza kutumia kibali cha
kuwakamata, bali
ilielekeza kwamba kwa kuwa walipewa fursa ya kutosha ya
kusikilizwa na
walifahamishwa kuwa wakishindwa kufika, kamati itaendelea na
kazi zake,
Kamati hiyo ikaendelea kujadili tuhuma zao bila kupata
utetezi wao.



Ubabe



Wakati anayetajwa zaidi kwa ubabe ni Dk Tulia, lakini
wabunge hao wa
Ukawa na hata Kabwe Zitto wa ACT, mbali na kuonesha dharau
iliyolazima
viongozi wa Bunge kutumia busara kuwa nao, wamekuwa
wakitumia ubabe na
kelele zenye lengo la kuzuia Bunge kufanya shughuli zake na
dhidi ya
aliyekalia Kiti cha Spika.



Ubabe wa hali ya juu uliowahi kuoneshwa ndani ya Bunge hilo,
ulifanywa
na Lema, ambaye aliwahi kabisa kuvua koti na tai tayari
kupigana, huku
akisema yuko tayari kuuawa akigombea haki.



Taarifa za Bunge zinaonesha siku waliyofanya vurugu, Lema
"alivua koti
na tai, ikiwa ni ishara ya kujiandaa kupigana, jambo ambalo
halitegemewi
kufanywa na kiongozi wa hadhi ya Mbunge.



"Mimi wataniua, hapa tunagombea haki," alisikika Lema
akisema huku
amevua koti na tai hatua ambayo imetafsiriwa kuwa "utovu
wa nidhamu wa
hali ya juu kwa Mamlaka ya Spika ambao haupaswi kuvumiliwa
kwa vyovyote
vile…" Mbali na Lema, Zitto alionekana akipiga kelele na
kubishana na
Spika mfano: Spika: Naomba waheshimiwa mkae.



Zitto: (Akikaidi agizo la Spika) Mheshimiwa Spika, Hoja ya
hadhi ya
Bunge. Spika: Naomba sana mkae, naomba nichukue nafasi hii
kumkaribisha
Mwenyekiti, Mheshimiwa Andrew Chenge, ili aendelee na ratiba
iliyoko
mezani. Mheshimiwa Chenge.



(Anaita Spika) (Makofi).



Zitto: (Akitumia ubabe) Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya
kuahirisha
mjadala… Mwenyekiti: Mheshimiwa Zitto nakusihi sana, hiyo
Kanuni ya Haki
za Bunge, hailazimishi Kiti kukubali kama ilivyo, nakusihi
isome
vizuri. (Makofi).



Zitto: Kanuni ya 69 hoja ya kuahirisha mjadala Mheshimiwa
Mwenyekiti.
Taarifa za Bunge zinaonesha kuwa matukio kama hayo
yamefanywa pia na
Mdee na Lissu, ambaye wakati fulani alikuwa akihamasisha
wabunge wote wa
Ukawa wasimame, wakati aliyekalia Kiti cha Spika,
amekataza.



Lissu: Mwongozo wa Mwenyekiti… Simameni basi.



Mwenyekiti: Ni mwongozo tu, wote mnataka mwongozo?



Wabunge wengi: Ndiyo.



Mwenyekiti: Unafanana na hili alilosema Mheshimiwa Heche?



Lissu: Si mnataka mwongozo, simameni muombe mwongozo.



Mwenyekiti: Waheshimiwa wabunge, naona sasa tunataka kutumia
utaratibu wa kuchelewesha shughuli za Bunge.



Lissu: Mwongozo, mwongozo, tunataka mwongozo. Mwenyekiti:
Nimesimama (Kanuni inataka wote wakae).



Lissu: Mwongozo (anakaidi).



Mwenyekiti: Nimesimama. (Akisihi). Matumizi ya uongo Mbali
na dharau,
vurugu na ubabe juzi taarifa nyingine ya Bunge iliwashika
wabunge wa
Viti Maalumu wa Ukawa, Susan Lyimo na Anatropia Theonest kwa
kusema
uongo.



Susan alipokuwa akichangia mjadala wa Hotuba ya Wizara ya
Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mei 11 mwaka
huu, alidai
kuwa Serikali imenunua magari 777 ya 'washawasha',
ambapo alidai kuwa ni
magari 50 tu yaliyotumika kwenye uchaguzi.



Alipotakiwa kufuta kauli alionesha kuwa anao ushahidi,
alipotakiwa
kuupeleka, alitumia ushahidi aliodai ni wa Mwananchi Online,
taarifa
rasmi za Bunge, taarifa za mtandao wa Alibaba na kielelezo
kutoka
Habarikablog. blogspot.com. Hata hivyo vielelezo hivyo,
vilipofanyiwa
uchambuzi hakukuwa na kielelezo cha Mwananchi Online, bali
cha
Mwanahalisi Online na pia kielelezo cha Habarikablog.
blogspot.com
hakikuainishwa.



Pili hakukupatikana kielelezo hata kimoja kilichothibitisha
kuwa
Serikali imenunua magari hayo 777 ya 'washawasha'.
Anatropia Anatropia
yeye katika kusema uongo, alidai bungeni kuwa Waziri wa
Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipokuwa Mkuu wa Mkoa
mwaka 2011,
alihusika na uporaji wa maeneo ya wananchi yaliyopo
Tegeta.



Mbunge huyo wa Ukawa alidai kuwa maeneo yaliyoporwa na
Lukuvi, yalikuwa
ya wananchi waliokuwa wakiishi mabondeni, wakiwemo wa Jimbo
la Segerea
na wananchi wa Ilala, ambao sasa wanataka maeneo yao huku
wakidai kuwa
Lukuvi alihusika kuyapora.



Kutokana na uongo huo, Lukuvi alilalamika kuwa mwaka 2011,
alikuwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge
na si Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam na wala hakuhusika na tuhuma
hizo.



Katika malalamiko yake, taarifa za Bunge zinaonesha kuwa
Lukuvi alisema
tuhuma zilizotolewa na Anatropia, si tu kwamba zilikuwa za
uongo, bali
pia zimemfedhehesha kwa kumhusisha na uporaji wa viwanja vya
watu
wanyonge.



Akiri ni muongo Alipoitwa Anatropia taarifa za Bunge
zinaeleza; "alikiri
mbele ya Kamati kuwa alisema uongo bungeni kwa kuwa ni
kweli Lukuvi
hakuwa Mkuu wa Mkoa mwaka 2011, hivyo asingeweza kuhusika na
uporaji wa
viwanja vya waathirika wa mafuriko."



Anatropia ameelezwa katika taarifa hiyo kuwa, iwapo
angeambiwa jambo
hilo akiwa bungeni, kuwa kauli aliyokuwa ameitoa siku hiyo
ilikuwa ya
uongo angeifuta.



Kutokana na vitendo hivyo, ingawa wabunge wa Ukawa wanasema
Bunge
linaongozwa kibabe, lakini ilibidi Bunge litoe adhabu
mbalimbali za
kinidhamu kwa wabunge saba wa Ukawa na Zitto wa ACT. Mbali
na Zitto,
wengine waliopewa adhabu ni Susan, Anatropia, Lema, Heche,
Mdee, Gekul
na Bulaya.



Chanzo habari Leo
 



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment