Wednesday 24 July 2013

[wanabidii] Balozi Lumbanga Ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi PPRA

Imeandikwa Jennifer Chamila — RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amemteua Balozi Matern Lumbanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Manunuzi Serikalini (PPRA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari  na  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya PPRA, Laurent Shirima imeeleza kwamba uteuzi huo , umeanza  rasmi kuanzia  Juni 20 ,mwaka huu ambapo Balozi Lumbanga amechukua  nafasi ya Dk.  Enos Bukuku aliyemaliza muda wake katika uongozi huo.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Balozi Lumbanga ni mchumi kitaaluma,ana Shahada ya kwanza ya Uchumi ambayo ameipata katika Chuo Kikuu cha Dares salaam (UDSM).

Pia ana Shahada ya Uzamili pamoja na Shahada ya Uzamivu katika masuala ya Mahusiano ya Kimataifa taaluma aliyoipata shule ya 'Geneva School of Dipmacy and International Relations', Switzerland.

Balozi Lumbanga ameitumikia Serikali ya Tanzania katika nyazifa mbalimbali tangu mwaka 1972, mwaka 1995 aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi nafasi alioishika hadi mwaka 2006 alipoteuliwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) nchini Geneva. Amestaafu utumishi wa umma  Julai mwaka jana (2012).

Balozi Lumbanga amekuwa Mwenyekiti wa tatu wa bodi  ya PPRA tangu ilipoanzishwa mwaka 2005 ambapo Mwenyekiti wa kwanza alikuwa Bw. Philemon Luhajo na kufuatiwa na Dkt. Bukuku.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment