Wednesday 1 May 2013

[wanabidii] DR KIGWANGALLAH AHUSISHWA NA UFISADI.

MBUNGE wa Nzega, Dk.Hamisi Kigwangalla (CCM), anadaiwa kuliibia taifa
kwa kutumia vibayamisamaha ya kodi ya mamilioni ya shilingi kwa ajili
ya ujenzi wa chuo cha afyaeneo la Uchama, wilaya ya Nzega.

Kwa mujibu wa nyaraka ambazo Tanzania DaimaJumatano imezipata, Dk.
Kigwangallah amejipatia misamaha ya kodi ya ongezeko lathamani na
ushuru wake kupitia kampuni ya Emergent Africa Limited,
anayoimilikikwa asilimia 78 na Bayoun Kigwangallah ana asilimia 22.

Kupitia kampuni hiyo, mbunge huyo ameingiza nchinibidhaa mbalimbali
ambazo badala ya kuzielekeza katika ujenzi, amefungua duka lakuuza
vifaa vya ujenzi eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam na nyingine
anaziuza kwawafanyabiashara wengine.

Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa kampuni yaEmergent Africa Ltd,
ilisajiliwa katika Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC)Septemba 27,
2011 na iliruhusiwa kupata misamaha hiyo kuanzia Septemba 2011hadi
Agosti 2014.

Kwa mujibu wa makubaliano kati ya kampuni yaEmergent Afica Ltd na TIC,
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliombwa kuisamehekodi kampuni hiyo
ya Dk. Kigwangallah vitu mbalimbali vyenye orodha toka namba1 hadi
390.

Bidhaa hizo kwa uchache ni kompyuta 1042,mashine za kutolea kopi 12,
printa 12, 'binding machines' 12, vikokotozi(calculator) 640, projekta
12, video kamera 12, feni 30, vifaa vya simumasanduku 28, jenereta
moja, magari aina ya Toyota 13, lori 3, Nissan NavarraPik up 4,
Mitsubishi Canter 2 na mabasi madogo manane.

Pamoja na msahama huo, Dk. Kigwangallahkupitia kampuni hiyo, aliingiza
nchini vitu bidhaa mbalimbali vikiwemo vigaevya sakafuni 2500 vyenye
ukubwa wa 600X600 na 1000 vyenye ukubwa wa 400 X 400pamoja na vigae
vya ukutani.

Katika orodha hiyo viko viti na meza za kulia,hema la bustanini, sofa,
kabati za kuwekea nguo, mazulia, vitanda na magodoro,televisheni na
vingine.

Aidha nyaraka hizo zinaonyesha baada yakupokea bidhaa hizo kutoka
nchini China, ziliuzwa katika madukambalimbali ya Kariakoo na vigae
vingine kuuzwa kwa mkuu wa wilaya moja mkoaniTanga (hatukumtaja) kwa
kuwa hakupatikana kujitetea.

Hata hivyo, kumeonekana utata katika nyakarahizo kwani kampuni ya
Delmas iliyosafirisha kontena la bidhaa hizo kuja kwa Dk.Kigwangallah,
ziko tofauti na ankaraza malipo.

Ankarahizo zinaonyesha kuwa zilitolewa na makampuni ya Louis Valentino
Investment andDevelopment Co. Ltd iliyopo Na. 19 Ji Hua 3 Road Foshan
na Sharpeye Furniture.

Wakati manunuzi yakionekana kufanyika ChinaOktoba mosi, 2012, nyaraka
nyingine zinaonyesha kuwa mali zilishaingizwa nchini tanguAprili 14
mwaka huo, kupitia kampuni ya Innovative Freight yenye TIN100-145-596,
risiti namba 2012/0000002986.

Na nyaraka za mamlaka ya mapato zinaonyeshabidhaa hizo ziliingia
nchini Aprili 3 mwaka jana, hali inayoonyesha kupishanakatika tarehe
za kununua na kuingiza bidhaa hizo.

Pia utata huohuo unaonekana katika taarifa zaShirika la Viwango
Tanzania (TBS) ambazo zinaonyesha bidhaa hizo zilikaguliwaMachi 28,
2012.

Huku kukiwa na orodha zinazotofautiana zamakampuni mawili ya
kibiashara wakati ankaraya malipo ilikuwa moja.

Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa kontena hilo lilipofika nchini
lilionekana kuwa na vitu tofauti navile vilivyoorodheshwa, hivyo
kusababisha kontena hilo kufanyiwa uchunguzi usio wa kawaida
kwakupekua mzigo mmoja mmoja.

Dk. Kigwangallah alipotafutwa kwa simukufafanua tuhuma hizo, alisema
amebanwa na kazi. Na alipoambiwa ametumiwamaswali kwenye barua pepe
yake, aliahadi kujibu lakini hakufanya hivyo.

Alipopigiwa tena jioni, alisema, "Sema harakaunataka nini?"
Alipoulizwa juu ya tuhuma hizo alikata simu.

Lakini baadaye aliandika ujumbe kwa simu:"Nitakupigia jioni nikitoka bungeni."

Alipoambiwa inaandikwa habari gazetini,alijibu kwa ujumbe mfupi kuwa
tuhuma zilikuwa za uongo bila kufafanua.

Source: TANZANIA DAIMA

--
"Tukosoane, Turekebishane, Tuwajibishane, ndipo Tusameheane". Regia Mtema.
--
Mobile: +255 (0) 713 24 67 64
Alternative: +255 (0) 784 24 67 64
Skype: Mohamedi.Mtoi
Twitter: @mohamedimtoi
Facebook: http://www.facebook.com/mouddymtoi
--

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment