TAMKO LA KUTOA UFAFANUZI DHIDI YA TAARIFA BATILI ZILIZOZALISHWA NA
MWENYEKITI WA BAVICHA
BWANA: JOHN HECHE [WEGESA CHARLES SUGUTA] KUHUSU KUVULIWA UANACHAMA WA
BAVICHA, NA KUSHABIKIWA NA MH. FREEMAN MBOWE, MWENYEKITI CHADEMA TAIFA
Nawashukuru sana wanahabari, kwakuchukua muda wenu kuja kunisikiliza.
Natambua mnakiu ya kusikiliza mambo mengiya kuwaeleza kutokana na
taarifa zilizosambaa kuhusu hiki kichefuchefukinachosambazwa kwa
makusudi na virusi vichache vilivyojivika ngozi yaukombozi.
Nimepokea simu nyingi kutoka kwawatu mbalimbali kutoka ndani na nje ya
Tanzania wakitaka kupata ufafanuzi baadaya kupata taarifa kupitia
vyombo vya habari kuwa nimevuliwa uanachama naU-Makamu Mwenyekiti wa
BAVICHA Taifa.Kama mlivyo ninyi, nami pianimeyasikia hayo kupitia
vyombo vya habari, maana sijapata barua au mawasilianoyoyote toka kwa
Mwenyekiti wa BAVICHA, Ndugu Wegesa Suguta (John Heche)aliyetoa tamko
hilo.Kwanza kabisa naomba kuweka wazikwamba sijawahi pewa shutuma
zozote au mashitaka yoyote yale yanayohusiana nahicho alichokiongea.
Niliamua kupuuzia kwa sababunamjua Heche ni mlopokaji, kiongozi
asiyejua wajibu wake, anayetumikiawasiomchagua, mtu asiye na malengo
na mtegemezi wa siasa ili kuendesha maishayake na ya familia yake. Pia
nilimpuuza kwa sababu najuasio Mwenyekiti aliyechaguliwa kidemokrasia,
aliwekwa kwa matakwa ya wakubwazake ambao wanamtumia kwa malengo
yaliyokusudiwa, ikumbukwe kuwa vijana watatu,Habibu Mchange, Mtela
Mwampambwa na Grayson Nyakarungu walienguliwa kimizengweili Heche
ashinde, hivyo kwetu sisi yeye ni sawa na Mwenyekiti wa
kuteuliwa.Hivyo sikumjibu mtu asiyekuwa na sifa sawa na zangu katika
harakati za kusakademokrasia ya kweli.
Lakini kitendo cha Mwenyekitiwangu, Mh. Freeman Mbowe kujitokeza
kupitia gazeti mojawapo na kudai madaiyangu ni ya kitoto,
kwanza kimenifedhehesha, ni dharau kwa vijana walionionanina sifa na
ukomavu na kunipa kura nyingi ili niwe Makamu Mwenyekiti waBAVICHA
Taifa.
Pili ni kama anahalalisha kikaobatili, kilichokiuka kanuni na katiba
ya CHADEMA ili kuhalalisha matakwa yaoyenye lengo la kuminya
demokrasia na uhuru wa kujieleza ndani ya chama.
Tatu anahalalisha hoja za vijana,ambazo ndio uhalisia kuwa Heche
hakuwa na sifa, na uwezo, hivyo alibebwa na Mh.Mbowe ili akae pale kwa
malengo yake.Ndio maana nilisema ukionakifaranga kimepanda juu ya figa
ujue mama yake yuko chini, hivyo mama yakekifaranga kajitokeza
kuhalalisha kifaranga chake kupanda juu ya figa.
MADAI YAALIYODAI MH. MBOWE KUWA NI YA KITOTONiseme wazi kwamba
nimesikitishwamno na madai aliyoyatoa Mwenyekiti wangu wa CHADEMA Mh
Freeman Mbowe kupitiagazeti la Mtanzamia la tarehe 12/01/2013 kwamba
madai yangu ni ya kitoto .
Kwanza niweke wazi kabisa kwambanamuheshimu sana Kiongozi wangu huyu
mkuu ambaye ndiye alipaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha
kwambahaligawi baraza la Vijana na chama kwa ujumla, ahakikishe kuna
utawala borandani ya chama, na utendaji haki, lakini cha kushangaza
ameibuka kumtetea Hechekwa hoja za mwegemeo wa upande mmojabila
kuangalia maelezo ya upande wa pili.
Niweke wazi kabisa kwamba kaulialiyoitoa dhidi yangu ni yakiushabiki
maana kama ni madai yangu kuhusu namna ninavyohujumiwakupitia kwa
Katibu Mkuu yeye anayo nakala ya malalamiko [ushahidi upo],
lakinihakuna hatua ambayo ameichukua.
Namshangaa Mwenyekiti kudai madaiyangu ni ya kitoto sasa sijui ni
madaiyapi anayazungumzia ? madai ya kitoto ni yapi? na madai ya
kikubwa ni yapi ? naje madai ya kitoto ni haya mimi kuhoji kwanini
hatuweki akiba kwenye akauntikwa ajili ya uchaguzi 2015 kama
tulivyokubaliana kwenye baraza kuu mara baadaya uchaguzi wa
2010.Naombaniwajulishe wanachadema kuwa, nimejitahidi sana kushauri
juu ya
1; Uanzishwaji wa chuo chamafunzo ya uongozi kwa makada wa CHADEMA ,
badala yake ni matumizi mabaya yafedha za ufadhili wa wadau tofauti na
hasa mfadhili mkuu ndugu SABODO. Hiiingesaidia pia kulea ki-mfumo wa
maadili ya uongozi kwa vijana wa umoja wawanafunzi wa CHADEMA wa vyuo
vikuu yani " CHASO" ambapo mimi ni mwasisi wamkakati huu nchini.
2; Chama kwa ujumla kutokuwa na jengo letu na hasa makao makuu yetu.
Niaibu kwa chama kikubwa kama CHADEMA kuwa na ofisi tulizopanga na
kulipa mamilioni ya fedha za ruzuku na misaada kwa manufaa ya
Mwenyekiti Freeman Mbowena Mkurugenzi wa fedha wanaomjua mmiliki wa
jengo la makao makuu. Kimsingi mimi natambua chama kina uwezo mkubwa
wa kuwa na majengo yetu.
3; Kupunguza mshahara wa katibumkuu Ndugu Dk. Slaa ambao ni zaidi ya
milioni saba kwa mwezi na marupurupu kibao ili pesa hizo na mamilioni
zielekezwe kujenga chama mikoani kama kweli tunataka2015 tuingie
Ikulu.
4; Kuhakikisha pesa zilizochangishwa kwenye M4C zinatumika ipasavyo na
si kama zitumikavyo kipindihiki ambapo ni kama tumelewa wingi wa watu
kwenye mikutano ya hadhara.
5; Kitendo cha Mwenyekiti wa chama kufumbia macho hatua ya ndugu Slaa
(katibu mkuu) kujikopesha pesa ya ruzuku ya watanzania zaidi ya
shilingi milioni mia na arobaini.
6; Hatua ya mwenyekiti ndugu Heche kulipwa mshahara na marupurupu hali
kanuni za chama haziruhusu huku Mbowe akifumbia macho wakati viongozi
wa mikoa na wilaya hawapewi pesa na vifaa vya uenezi.
7; Kitendo cha mchumba wa Dk.Slaa, Josephine Mushumbusi kuzunguka
mikoani na kulazimisha kupokelewa kama mke wa mfalme na kuendesha
vikao vya ndani na mikutano ya hadhara yenye kulenga kuwajenga
wagombea ubunge anaowataka yeye na katibu mkuu kwa mwaka 2015.
Ndugu wanahabari, je hizi ndo hojaza kitoto anazodai Mh. Mbowe? Hivyo
basi namtaka Mh. Mbowe sasa asikimbiliekujibu hoja kiushabiki.
Ajitahidi kuwa na fikra na Busara ili kukisaidia chama kuvuka kwenye
daraja la sasa la pepo kufukuzana. Atambue Baraka anazozitoa wanachama
wafukuzwe hovyo na kunyanyaswa ni hatari kwa kuwa anaandaa kundi kubwa
nje ambalo litageuka mwiba siku za usoni.
UHALISIA ULIOPO:
Ndugu waandishi wa habari,
Naomba kuweka wazi kwamba mimi Juliana Shonza ni Makamu Mwenyekiti
halali wa baraza la vijana (BAVICHA). Taarifa zozote zile mlizozisikia
kuhusu kuvuliwa kwangu uanachama, naomba kwa nguvu moja kupitia
taaluma yenu muwaambie watanzania kwamba wazipuuze. Ni taarifa
zilizotolewa na kikundi cha kihuni kilicholenga kutimiza matakwa ya
wakubwa wao. Kikundi hicho hakina mamlaka ya kikatiba yoyote yale ya
kunivua uongozi huunilio nao.
Kuthibitisha hilo kuwa ni kikundimufilisi, hadi ninapoandika waraka
huu kwenu sijapewa barua yoyote ile inayonitaarifu kuwa nimevuliwa
uongozi wangu. Hii ni wazi wanatambua kuwa wanachemka, wanatengeneza
makundi kwa maslahi wanayoyaona yanawafaa.
Sikuchaguliwa ili niwe chombo cha kuwatumikia watu, na badala yake
nilichaguliwa ili niwatumikie vijana waCHADEMA na watanzania kwa
ujumla, na pale nilipoona kuna ukiukwaji na kuhoji ndio chanzo cha
mizengwe na matamko ya Ndugu Wegesa (John Heche).
Nimekuwa nikiwasumbua viongozi wenzangu kuhusu kutengeneza kadi za
BAVICHA na kusajili wanachama katika mfumo mzuri (database) ili tuwe
na kumbukumbu ya wanachama wetu lakini yote yameshindikana kwasababu
amekuwa akiendeshwa na mfumo dume kandamizi kwa mwanamke, mara nyingi
nimemshauri kwa ajili ya maendeleo ya Baraza na nimekuwa nakwamishwa
na Mwenyekiti na Katibu na hata leo sisi wote ni wanachama kwa
kufikirika (imagination), kwa kuwa bado hatuna kadi za uanachama kwa
vijana wa BAVICHA zaidi ya kutambulika na katiba ya chama.
KUKIUKWA KWA KATIBA
Ndugu wanahabari, ni wazi kuwakatiba pamoja na mwongozo wa baraza letu
la vijana bavicha ulikiukwa katikakikao walichokiita kamati tendaji
iliyokaa tarehe 05/01/2012 ambayo iliongozwa na Bwana Wegesa Suguta
(John Heche) kama Mwenyekiti, hali inayonilazimu kusema wazi, bila
kumung'unya maneno kwamba maamuzi yaliyotolewa na kikao hicho
yalikwishapangwa na viongozi wa kitaifa hayakuwa halali. Nasisitiza
kwamba ni ukweli ulio wazi kwamba agenda na maazimio ya kikao hicho
yalikwisha amuliwa hata kabla ya kikao hicho kwasababu kubwa mbili:
1; Taarifa za kufukuzwa kwetuzilikwisha anza kusikika kwenye mitandao
ya kijamii kama vile jamii forum nafacebook mwezi mmoja kabla ya kikao
cha kamati tendaji batili.
2; Pili ushahidi wa kimazingirakwa maana ya ukiukwaji mkubwa wa
kikatiba na mwongozo wa Baraza letu la Vijana uliofanyika siku ya
kikao.
Ndugu wanahabari,
Ikumbukwe kuwa pamoja na uwepo wa taarifa za kikao mwezi mmoja kabla
binafsi nililetewa taarifa hizo siku mbili kabla ya kikao, tena kwa
njia ya ujumbe mfupi wa maandishi {sms} na baadae kupigiwa simu na
Katibu wa Baraza Bwana Munishi ikinitaka kuhudhuria kikao hicho
kutokana na kuwa nje ya Dar-es –salaam kwa mambo ya kifamilia zaidi
niliwataarifu viongozi wenzangu kwa utaratibu maalumu wa mawasiliano
ya kiuongozi kwa maana ya kuwatumia barua ya udhuru wa kutohudhuria
kikao.
Lakini cha kushangaza na kustaajabisha kwa viongozi wenzangu hawa
ambao kwa namna moja ama nyingine napata ugumu wa kuelewa kama kweli
wana sifa za kuitwa viongozi tena wa idara nyeti sana katika ustawi wa
chama chetu, kwa makusudi kabisa ama kwa kutumwa kufanya hivyo ama kwa
utashi wao mdogo wa kiupembuzi yakinifu waliamua kuvunja na kukiuka
katiba ya chama na kujipa vyeo vya kiunyampara kwa kuamua kuchukua
maamuzi ya kutuvua uanachama wa kufikirika wa baraza mimi na vijana
wenzangu Ndugu Mwampamba na Mchange ambao nao hawakupewa nafasi ya
kusikilizwa, ambao moja kwa moja tunapoteza sifa yakuwa wanachama wa
CHADEMA.
Ndugu wanahabari,
Naomba sasanijikite katika katiba ya chama changu na mwongozo wa
baraza la vijana sura ya sita kipengele cha 6.5 ambacho kinasema
taratibu zifuatazo lazima zifuatwe katika kuchukua hatua za kinidhamu.
6.5.2 kwa mujibu wa ibara 5.4.3 na .4.4 ya katiba, mwanachama
yeyotehatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama
kufukuzwa uanachama bila kwanza
{a} kujulishwa makosa yake kwamaandishi na kutakiwa kutoa majibu
katika muda usiopungua wiki mbili.
[b] kupewa nafasi yakujiteteakatika kikao kinachohusika.
{c} Mwanachama atajulishwa kwamaandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki
mbili baada ya kusikilizwa.
Ndugu waandishi wa habari,Nisemewazi kwamba hakuna kifungu
kilichofatwa kati ya hivyo niliyoviainisha hapo juu,hakuna barua
yeyote niliyojulishwa ya hayo waliyoyaita mashitaka yangu zaidi ya
kuyasoma na kuyasikia kwenye vyombo vya habari baada ya wao na kikao
chaoharamu kuchukua maamuzi yakunivua uanachama wa Bavicha .
Sikupewa nafasi yakujitetea maanasikuwepo kwenye kikao, barua ya
udhuru wakutohudhuria walikuwa nayo. Na vilevile mpaka leo hii
sijajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao hicho batili badaa yake
viongozi wenzangu hawa wameamua kuujulisha umma wa Watanzania na
wanachadema kwa ujumla pasipo kunijulisha mimi kwanza. Ukiangalia pia
kifungu cha 6.5.6 cha katiba kinasema KIONGOZI YEYOTE hatachukuliwa
hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na
mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu kwa maandishi.
Sasa basi namtaka Bwana Wegesa Suguta awaeleze umma wa watanzania kama
alivyokurupuka kuwaeleza kwamba Shonza amevuliwa uanachama wa Chadema
ni wapi na lini yeye kama Mwenyekiti nilipewa barua ya hayo
wanayoyaita mashitaka, na ni lini niliwapa majibu ya mashitaka hayo.
UHALALI WAKIKAO CHA KAMATI TENDAJI
Ndugu wanahabari,
Ikumbukwe kwambakikao cha juu kuliko vyote kwenye ngazi ya chama
husika ni Mkutano Mkuu ambao ndio ulioniweka madarakani kutokana
nakuwa na imani na mimi na kikatiba ndiohaswa ulipaswa kuniandikia
mashitaka, kunijadili, kunihoji na kutoa maazimio ambayo yangepelekwa
kamati kuu ambao kimsingi ndiyo yenye mamlaka ya mwisho yakumvua mtu
yeyote uanachama wake baada ya kujiridhisha na taarifa na uchunguzi
kutoka kwenye kikao husika kilichomwandikia mwanachama mashitaka na
kumuhoji.
Ndugu wanahabari ifahamike wazikwamba kikatiba kuna ngazi mbili tu
zinazoweza kumvua mtu uanachama wake ambazoni ngazi ya tawi na ngazi
ya kamati kuu.
Hivyo basi namtaka sasa Bwana Wegesa Suguta auambie umma wa watanzania
kwamba ni lini kamati tendaji ya vijanailigeuka ama kukaimishwa
madaraka ya ngazi ya tawi, ngazi ya mkutano mkuu amakamati kuu yakuwa
na uwezo wakumvua kiongozi uanachama wake?
Ndugu waandishi wa habari,
Wajumbe wa kamati tendaji kikatiba ni makatibu wa kamati za uratibu za
mikoa lakini badala yake Bwana Wegesa Suguta (John Heche) amekuwa
akiwaita wenyeviti wamikoa na sababu kubwa ikiwa ni kwamba wengi wa
wenyeviti hao hawastahili kuwepobavicha kutokana na kwamba umri wao
kuwa zaidi ya miaka 35 hivyo kupoteza sifa za kuwa viongozi wa BAVICHA
ambayo katiba inamtaka mwanabavicha yeyote kuwa namiaka 18-35, hivyo
basi kwa kuhofia kupoteza nafasi zao hulazimika kukubaliana na lolote
lile ambalo bwana Wegesa Suguta analitaka hata kama wakijua kwamba ni
kinyume kabisa na matakwaya katiba na mwongozo wa baraza.
Hivyo kumpa Heche mwanya wakuamua lolote lileanalotaka ama kutumwa
kulifanya. Kutokana na hilo natangaza wazikwamba kikao cha kamati
tendaji kilichopita ni batili, chenye wajumbe batili, kimesimamiwa na
viongozi batili kwa maana ya mwenyekiti na katibu wake maana
wameshindwakuheshimu misingi ya kikatiba katika namna ya demokrasia ya
chama chetu hivyo basi nachukua nafasi hii kuutangazia umma wa
watanzania na wanachadema kwa ujumla wao kwamba maamuzi ya kamati
tendaji yaliyotangazwa na kiongozi kilazana daraja la viongozi wa juu
bwana Wegesa Suguta ni batili.
Ndugu wana habari,
Sifa ya Mwalimu ni kuweza kubadilisha hali ya umbumbumbu wa wanafunzi
wake, Heche kama kiongozi, na Mwalimu kitaaluma (nina wasiwasi na
ufaulu wake katika huo ualimu) alipaswa kuwa mfano bora kwa vijana wa
Chadema kuwaelekeza na kuwafundisha namna ya kuheshimu misingi ya
kikatiba ambayo kama chama na baraza tumejiwekea na tunapaswa kuifuata
ni wazi kuwa Heche ameshindwa kuwa mfano bora kwa vijana, hajui kanuni
za BAVICHA wala katiba ya CHADEMA, mkurupukaji, mropokaji, mwenye
uwezo mdogo wa kufikiri, dikteta anayetumia mamlaka asiyokuwa nayo
(akipewa mamlaka atatuchinja huyu) hivyo hafai kuwa hata Mwenyekiti wa
serikali za mtaa, wala kuaminiwa popote kupewa nafasi ya kiuongozi. Ni
wazi ubongo wake yeye nakatibu baraza bwana Munishi haujapewa tohara
la kisiasa, ifike mahali wakubali kufundwa unyagoni na manyakanga wa
kisiasa.
KUHUSUKUVULIWA UANACHAMA WA BAVICHA;
Ndugu wanahabari,
Kuhusu kuvuliwauanachama wa Bavicha ambao moja kwa moja napoteza sifa
ya kuwa mwanachadema namshangaa kiongozi huyu ambaye sifa yake kuu
siku zote ni ukurupukaji kwa kusema kwamba nimevuliwa uanachama wa
Bavicha huku akijua wazi Bavicha haijawahi kuwa na kadi za baraza.
Katika mwongozo wa baraza lavijana kipengele cha 4.4 KUJIANDIKISHA
UANACHAMA 4.4.1 inasema ili kijanaaruhusiwe kujiunga bavicha ni lazima
awe na sifa zifuatazo
[a] Awe mwanachama wa CHADEMA
[b] Awe na umri kati ya miaka 18 na 35
[c] Awe anakubaliana na misingiya mwongozo wa BAVICHA
4.4.2 Inasema kijana aliyekidhimatakwa hayo hapo juu, atanunua kadi ya
uanachama wa BAVICHA
Kutokana na kipengele hicho namtaka bwana Wegesa Suguta auambie umma
wa watanzania na wanaCHADEMA kadi yake yeye ya baraza la vijana ni
namba ngapi na aliichukulia wapi? Aueleze umma wa watanzania kadi
yangu ya baraza la vijana ni namba ngapi na niliichukulia wapi?
Ndugu waandishi wa habari,
Nidhahiri baraza la vijana chadema hatuna kadi ambayo kimsingi ndiyo
utambulisho wa mwana BAVICHA endapo akishakidhi sifa zilizoainishwa
hapo juu. Na ni wazikwamba vijana wote wa CHADEMA tuna sifa za kuwa
wana Bavicha lakini si wanachama wa BAVICHA kutokana na kwamba
nimekuwa nikimwambia mara kwa mara umuhimu wa kuirasimisha na
kuianzisha ili iwe taasisi kamili kwa kuwa na kadi za vijana kama
mwongozo wa vijana unavyojieleza.
UELEWA WANGU KUHUSUKUNDI ANALOLIITA NDUGU WEGESA SUGUTA (JOHN HECHE)
NI "MASALIA"
Ndugu waandishi wa habari,
Hakuna kundi linaloitwa masalia ndani ya Chadema na BAVICHA. Gazeti la
MWANAHALISI ndilo lililoandika kuwa vijana wote waliofutwa na
kuondolewa kwenye uchaguzi wa BAVICHA mwaka 2011 ni MASALIA ya Zitto
yanayopukutishwa Chadema. Kimsingi gazeti hili lilikuwa linafanya kazi
yake ya kipropaganda ndani ya CHADEMA ili kukigawa Chama. Lilikuwa
linatimiza wajibu wake wa kupika mpasuko ndani ya chama tena kwa
kuhusisha na viongozi wakubwa ndani ya chadema.
Ni aibu kubwa sana na ni hatari kuona kiongozi kama Wegesa Suguta
anakuwa mstari wa mbele kushabikia neno masalia, huku akijua wazi
kufanya hivyo ni kuligawa baraza la vijana. Kwa nguvu moja nalaani
kitendo hiki cha kipuuzi kinachofanywa na Mwenyekiti huyu wa BAVICHA
cha kuchekelea upuuzi uliopikwa na gazeti la MwanaHalisi. Naomba
atumie rasilimali za chama kujenga umoja wa vijana imara, tushirikiane
kuimarisha Bavicha yenye tija kwa chama na sio kusherekea mpasuko
ndani ya baraza la vijana.
UELEWA WANGU KUHUSU KITU KINACHOITWA PM7
Ndugu waandishi wa habari,
Naomba kunukuu maneno ya mtu maarufu sana mitandaoni na kwenye uga wa
habari Mzee Mwanakijiji anasema
"Uongozi imara sio kutegeana, kunyemeleana na kufukuzana. Uongozi
imara ni kushirikiana".
PM7 ni jina lenye maana ya "PATRIOTIC MOVEMENT" yaani harakatiza
kizalendo kwa mujibu wa Ndugu Ben saanane ambaye alitumwa na kiongozi
wa juuwa chama kuja kulitekeleza kwa vijana walioenguliwa kwenye
uchaguzi wa BAVICHAmwaka 2011 na wanaoonekana kusigana na kiongozi
huyo kimawazo. PM7 ni wazoliliobuniwa na kiongozi mmoja wa juu wa
chama akishirikiana na Ben saanane wakinuia kutega mtego wa kuwanasa
vijana wanaoonekana wapo tofauti kimawazo nakiongozi huyo wa chama.
Kwa kuwa wazo hilo lilikuwahalina manufaa kwa chama, halikutekelezwa.
Kiongozi huyo bila kumung'unya maneno ameamua kuwatumia vijana hao
kuandaa kikao batili cha kamati tendaji ya John Heche ili awafukuze
vijana hao. Hii ni hatari sana kuona kiongozi wa chama unageuka simba
na kuanza kuwawinda watoto wake ili uwamalize kisiasa kwa sababu zako
binafsi.
MAAJABU KATIKAMEDANI ZA SIASA ZA BAVICHA MWAKA 2013
Ndugu waandishi wa habari,
1. Hii ni ajabu sana katika kikaocha kamati tendaji batili, Ambao
hatukuhojiwa ni watu wawili, mimi Juliana Shonzana kijana mmoja
anaitwa Exaud Mamuya. Lakini Mimi Juliana Shonza nimehukumiwa bila
hata kusikilizwa wala kupewa mashitaka na chombo chochote katika
chama. Wakati huo huo Exaud Mamuya hajahukumiwa kwa madai hakufika
kwenye kikao. Hii ni dhahiri huu ni mkakati wa kipuuzi ambao
unaendeshwa na watu wapuuzi tena kwa misingi ya kikabila na kikanda.
2. Muasisi mwenza wa PM7 na kibaraka wa kiongozi wa juu wa chama
aliyetumika kutoa shutuma chafu kwa Naibu Katibu Mkuu. Kijana
anayefahamika kwa jina la Ben Saanane ameachwa kwa madai yeye amekiri
mbele ya hiyo kamati tendaji kwamba ni kweli alinuia kumchafua Naibu
Katibu Mkuu wa chama na kukivuruga chama. Wakati tuhuma zake
zinafananana za Mchange na Mwampamba.
3. Mkakati wa John heche navibaraka wake umejikita kutukuza ukanda
ndani ya chama tena wa wazi wazi.Ukanda huu umejidhihirisha kwenye
kutoa hukumu batili za tuhuma kama ifuatavyo.
Vijana waliohukumiwa wote niwale wanaotokea Mbeya, Mbozi na Kibaha.
Wakati Vijana wa Kilimanjaro wameachwa kwa madai wao wametoa
ushirikiano.
Waliohukumiwa ni:
_Mtela Mwampamba-Mbozi, Mbeya
_Habib Mchange-Kibaha, Pwani
-Juliana Shonza-Mbozi, Mbeya
-Joseph Kasambala – Mbeya mjini (kasimamishwa)
- GWAKISA Mwakasendo –Rungwe, Mbeya (kasimamishwa)
Pamoja na wanachama watatu waliopo Mbeya mjini waliofukuzwa
uanachama.
Waliosamehewa ni:
_Ben saanane-Kilimanjaro
_Exaud Mamuya-Kilimanjaro.
Hii ni dhamira ya wazi kabisa kwamba CHADEMA sasa ni chama cha
kikanda, Viongozi wa CHADEMA wanatumika kutangaza ukanda kwa
watanzania.
Kwa maana hiyo wale wote wasio wa kaskazini ndani ya Chadema
tusitegemee kutendewa haki.
MAMBO NILIYOMSHAURI HECHE NA KUMUONYA:
Ndugu waandishi wa habari, Sisikama vijana tusigeuze siasa kuwa ajira
wala chombo cha kuendeshea maisha, ni moja ya vikwazo katika kukuza
demokrasia ya kweli, maana wengi wanaendekeza njaa na uhitaji wa
maisha yao ili kupindisha ukweli.
Moja ya maswali yangu kwa Mwenyekiti ni kitendo cha kubinafsisha gari
alilotoa Naibu Katibu Mkuu kwa ajili ya BAVICHA na badala yake
akalifisadi, akafanya mali yake binafsi na kumuweka Mdogo wake Chacha
Heche kuwa dereva wake, nimekuwa nikipinga matumizimabaya ya
rasilimali hiyo kwa manufaa binafsi, na badala yake gari hiyo
ifanyekazi iliyokusudiwa, huu ni msingi wa kuonyesha tofauti yetu na
wanaotumiarasilimali za serikali (Taifa) kwa manufaa binafsi nay a
familia zao.
Pia nilimshauri Mwenyekiti awe nakipato halali kama katiba ya chama
inavyosema Sura 10 MAADILI YA VIONGOZI ibara ya 10 kifungu cha (6)
kinasema Kiongozi anatarijiwa kujitosheleza yeye nafamilia yake kwa
mapato halali ili kutokuwa ombaomba kwani tabia hiyo itadhoofisha
uwezo wake wa kutoa uamuzi sahihi, ili kuwa mfano bora wauwajibikaji
kwa vijana, kama ambavyo Mwalimu Nyerere alivyosema kipimo cha Utuni
kufanya kazi, badala yake ametelekeza taaluma ya ualimu, aliyotumia
pesa za walipa kodi kwa kusoma na muda wote ni kupiga soga bila
uzalishaji na kujipatia kipato halali, na badala yake anategemea
mshahara usio halali kuishi, ni wazi Mwenyekiti ni cheo cha kisiasa na
hatakiwi kulipwa mshahara, wala kulipiwa nyumba kwa mujibu wa kanuni.
Badala yake majibu anafikiri ni kufanya njama na waliopindisha
taratibu hizo ili alipwe mshahara kwa maslahi yao ya kisiasa. Na
tumekuwa tukilipinga hilo kwani tunataka tuwe mfano wa utawala bora
kwa vitendo na si maneno peke yake.
MWISHO:
Ndugu waandishi wa habari,
Nipokwenye mchakato na wanasheria wangu kushughulikia swala la
kumpeleka mahakani Bwana John Heche na gazeti la Tanzania Daima toleo
namba 2958 kwa kuniita msaliti wa CHADEMA, natumiwa na CCM na kuwa
nina mahusiano (natumiwa) na Wassira tena bila kunihoji mimi Juliana
Shonza. Kwa maana hiyo wamenichafua na kunidhalilisha mbele ya umma wa
watanzania.
Pili naomba kuweka wazi kwambanatarajia kuomba ufafanuzi wa kikatiba
juu ya shutuma zilizotolewa kwenye vyombo vya habari dhidi yangu na
bwana Wegesa Suguta (John heche) ili aseme ni aminisho lipi la
kuthaminisha na kusakidikisha mtazamo wa maono yake ili bongo za
watanzania zijue ukweli. Mimi Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA natangaza
rasmi Mtela Mwampamba na Habib Mchange ni wanachama hai na halali wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Hivyo nawaomba waendelee na kazizao za ujenzi wa chama kwenye majimbo
yao na taifa kwa ujumla. Nawaomba wananchi na wanachama wote wa
CHADEMA waendelee kuwa na imani dhidi ya vijanahawa. Kama
mlivyomwamini Mwampamba na kumpa kura 32000 na kama mlivyo mwamini
Mchange na kumpa kura 10,400 kwenye uchaguzi wa Ubunge mwaka 2010.
Vivyo hivyo naowaombamuendelee kushirikiana nao kuhakikisha wanatimiza
adhima ya ukombozi mwaka2015.
Wenu katika ujenzi wa demokrasia makini
Juliana Daniel Shonza
M/Kiti BAVICHA-Tanzania Bara.
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment