Tuesday 15 January 2013

Re: [wanabidii] MAONI YA SAED KUBENEA KUHUSU KATIBA MPYA

Hivi katiba haitamki uwepo wa haki ya elimu na afya? mimi nadhani tuisome upya, navyojua mimi unaporidhia maazimio muhimu ya kimataifa, sheria zako inabidi uziboreshe ziendane na kile kinachotajwa na maazimio hayo! Kwa hiyo elimu ni haki ya kila mtu, japokuwa kwa kutoijua haki hiyo watu hatuidai na vivyo hivyo kupatiwa huduma ya afya ya msingi ni lazima na hata sera ya afya inayotumika hivi sasa imetamka hivyo! na ndivyo ilivyo pia katika katiba!

2013/1/15 Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
Nani anataka nini katika katiba mpya?


Haya ni maoni yaliyowasilishwa na Saed Kubenea wa MwanaHALISI; gazeti
lililofungiwa na serikali kwa muda usiojulikana tangu 30 Julai 2012.

JUZI (10 Januari 2013) wenye vyombo vya habari na asasi nyingine za
habari waliwasilisha kwa Tume ya Katiba Mpya, mapendekezo ya asasi zao
na hata kuongeza maoni binafsi kama mwenyekiti wa mkutano wa Katiba,
Prof. Mwesiga Baregu alivyoruhusu.


Saed Kubenea, Mkurugenzi Mtendaji wa Hali Halisi Publishers Limited
(HHPL), wachapishaji wa magazeti ya MwanaHALISI na MISETO,
aliwasilisha maoni yake. Ndimara Tegambwage ameyasoma na kuyafanya
moja ya mambo muhimu aliyoona yenye thamani. Anatushirikisha:

Mapendekezo: Katiba Mpya (Na Saed Kubenea)

1. Kuhusu vyombo vya Habari

KATIBA itamke kuwa vyombo vya kutunga sheria (Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania; Baraza la Wawakilishi, Bunge la Tanganyika au
Bunge la Shirikisho; na vyovyote vile vitakavyokuwepo) visitunge:

a) Sheria inayopingana (inayokinzana), inayokwaza au kuingilia uhuru
wa kuwa na maoni (kufikiri)
b) Sheria inayopingana, inayokwaza au kuingilia uhuru wa kujieleza
(kutoa kauli)
c) Sheria inayopingana, inayokwaza au kuingilia uhuru wa habari
(kupata habari zozote zinazohusu jamii zilizoko mikononi mwa serikali)
d) Sheria inayopingana, inayokwaza au kuingilia uhuru wa vyombo vya
habari (kazi za utafutaji, ukusanyaji na usambazaji wa habari
inayofanywa na waandishi wa habari na watangazaji)
e) Sheria inayopingana, inayokwaza au kuingilia uhuru wa kujumuika kwa
amani (mikutano/maandamano ambavyo kihalisi ni njia za wanajamii
kuwasiliana au kupeleka ujumbe kwa wahusika)

2. Kuhusu Mamlaka ya DPP

Katiba itamke kuwa:

a) Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ateuliwe na chombo huru cha uteuzi
(siyo rais wa nchi) na athibitishwe na Bunge
b) DPP awajibike kwa Bunge (Chombo cha kutunga sheria)

3. Mapendekezo Mengine

1. Katiba itamke kuwa ARDHI ni mali ya Watanzania. Isiwekwe chini ya
rais bali iwe chini ya wananchi wa Tanzania. Serikali itakuwa tu na
mamlaka ya kutwaa ardhi kwa ajili ya manufaa ya umma ambayo
yameainishwa kama vile ujenzi wa miundombinu, utunzaji wa mazingira na
uboreshaji makazi. Serikali isiwe na uwezo wa kutwaa ardhi kwa ajili
ya uwekezaji wa mtu binafsi au kampuni kama inavyoelezwa sasa na
Sheria ya Ardhi ya Mwaka 1999.

2. Katiba itamke kuwa kila kijiji kitakuwa na serikali ya kijiji
ambayo itaongoza kijiji hicho pamoja na uwezo wa kutunga sheria ndogo
na kuzipitisha chini ya usimamizi wa mkutano mkuu wa kijiji. Serikali
za vijiji ndizo zitakuwa na mamlaka ya kusimamia na kulinda haki za
wananchi juu ya umiliki wao wa ardhi ya kijiji na kupanga mipango ya
matumizi ya ardhi. Zitakuwa na uwezo wa kutoza kodi na kuendesha
miradi ya maendeleo vijijini.

3. Katiba itamke kuwa rasilimali za madini, mafuta, gesi na maliasili,
ni mali ya Watanzania na ni lazima zitumike na kuvunwa kwa manufaa ya
Watanzania. Serikali haitasaini mikataba bila kibali cha bunge; bali
itakuwa na uwezo wa kutoa leseni za utumiwaji wake. Utoaji huo wa
leseni lazima pia uwe wa wazi na ambao utaidhinishwa na Bunge.

4. Katiba itamke kwamba migogoro yote ya uwekezaji sharti isuluhishwe
kwa mujibu wa sheria za Tanzania na Mahakama za Tanzania. Hili ni
takwa la Kanuni ya makubaliano ya Calvo na vilevile Azimio Na. 1803 la
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la Mwaka 1962 na Azimio Na. 3281 la
1974 la Baraza hilo juu ya Haki na Wajibu wa Mataifa juu ya Maliasili.

5. Katiba itamke kuwa rais atachaguliwa kwa kupigiwa kura na kupata
zaidi ya asilimia 50 ya kura za watu wanaotakiwa kupiga kura. Yeye na
serikali yake ni lazima awajibike kwa bunge na kila uteuzi anaofanya
kwa nafasi za juu za uongozi, sharti uidhinishwe na bunge baada ya
Bunge kuhojiana nao.
6. Katiba itamke kuwa Bunge lina madaraka na haki ya kumfuta kazi rais
kwa kutowajibika au kwa kutumia madaraka yake vibaya.

7. Katiba itamke kuwa rais hatakuwa na haki au uwezo wa kulivunja
bunge kwa sababu yoyote ile.

8. Katiba itamke kuwa rais hatakuwa na kinga dhidi ya mashitaka yoyote
yale akiwa madarakani na baada ya kutoka madarakani. Mtu yeyote
anaweza kufungua kesi dhidi yake binafsi au ofisi yake.

9. Katiba itamke kuwa uteuzi wa majaji wa mahakama kuu na mahakama ya
rufaa ufanywe na chombo huru (badala ya rais) na ufuate umahiri na
uelewa wa sheria pamoja na uadilifu wa kimaadili na kisheria.

10. Katiba itamke kuwa mhimili wa Mahakama, ukiongozwa na Jaji Mkuu,
ndio usimamie na kuwasilisha bajeti yake bungeni (badala ya serikali
kama ilivyo sasa).

11. Katiba itamke kuwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na viongozi
wengine wakuu wa tume, wateuliwe na chombo huru cha uteuzi baada ya
wanaotaka nafasi hiyo kuomba na kufanyiwa usaili. Aidha, maamuzi ya
tume, kwa nafasi yoyote ile ya wagombea, yaweze kupingwa na mtu yeyote
mahakamani.

12. Katiba itamke kuwa kukosa uadilifu au kutumia madaraka vibaya,
kama itakavyothibitishwa na chombo husika, ni kosa la jinai.

13. Katiba itamke kuwa wote wanaojipatia utajiri kwa kuhujumu uchumi
au watu wanaojitajirisha kwa kutumia madaraka yao ya umma, lazima
washitakiwe kwa kosa la uhaini na mali zao zote, ikiwa ni pamoja na
zile za walionufaika kutokana na kosa hilo, zitaifishwe.

14. Cheo cha Makamu wa Rais kiondolewe. Kibaki cha Waziri Mkuu.

15. Katiba itamke kuwa wakuu wa mikoa, wilaya (kama ni lazima
kuendelea kuwa nao) wapatikane kwa kupigiwa akura ili w3aweze
kuwajibika vema katika maeneo yao. Mameya wa miji na majiji nao
wachaguliwe na wananchi moja kwa moja badala ya kuchaguliwa na
madiwani.

16. Katiba itamke haki ya kuishi katika mazingira safi na salama
lazima.

17. Katiba itamke kuwapo haki ya kufungua kesi za kutetea katiba, haki
za binadamu na utawala wa sheria bila gharama zozote zile.

18. Katiba itamke kuwa elimu na afya ni haki kwa Watanzania wote.

19. Katiba itamke haki ya starehe.


Mwisho.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment