Saturday 26 January 2013

[wanabidii] Helmet zinatusaidia sana kwa usalama wetu lakini vipi kuhusu maambukizi ya magonjwa ya ngozi?

Na. Lemmy Hipolite-Mo Blog.

Kofia ngumu za kusaidia kuokoa kichwa dhidi ya majanga mbalimbali iwe
ni katika maeneo ya ujenzi au katika vyombo vya usafiri ni muhimu sana
kwetu tunapokuwa katika mazingira hayo.

Tunaishukuru serikali kwa kutumia idara zake husika kuhimiza matumizi
ya kofia hizi hasa kwa madereva wa usafiri wa pikipiki maarufu kama
Bodaboda.

Kama inavyojulikana mtu ni afya na pia tunafahamu kuna baadhi ya
magonjwa ya kuambukiza kwa njia ya kugusana, kutumia kitu kimoja watu
wawili au zaidi na mengine kwa njia ya maji, hewa, mbu, kujamiiana na
kadhalika.

Hapa kwenye hili la kofia ngumu bado hainiingii akilini vizuri jinsi
gani twaweza kukwepa magonjwa ya ngozi na mba japo sio lazima tuyapate
wala hatuyaombei ila tunaangalia uhalisia wa matumizi ya kofia hizi.

Ndugu zangu wataalamu wa magonjwa ya ngozi na tiba hili likoje katika
uhalisia wake? Sichokonoi ila naomba kufahamu tu kwamba tuwe
tunazifua? Au hakuna neno? Mzingatie pia je zitakauka?.

Wadau sijasema msivae helmet la hasha nimeulizia tu ili woote tupate
fahamu.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment