Saturday 19 January 2013

Re: [wanabidii] TUJADILI UCHUMI

Ndugu senkondo

Jioulize kwa nini wabunge hao wameamua kuajiri watu wa nje kwa ajili ya kuendesha biashara zao na sio watanzania ? hapo ujue kuna tatizo miongoni mwa watanzania wenyewe , wajiangalie waone wapi wanakosea ili waweze kupata fursa mbalimbali zinazotokea sio kuendelea kulalamika tu kila kukicha .

Pili hii boom ya raia wa Asia kuvamia ajira haliko tanzania tu , hata mataifa mengi ya afrika yana boom hili , hata huko kanda ya arabia kuna boom la hawa jamaaa , tujiangalie tuna matatizo chungu nzima .

2013/1/19 <esenkondo@yahoo.com>
Ndugu zangu tunapozungumzz kuhusu ajira kwa wazlendo tuangalie pia ajira za viwanda vilivyotaifisjswa idadi ya wahindi ma wafilipino ni wengi kwenye viwanda vya Morogoro acha miti inayoteketea viwandani hapo. Nani akemee hili? Viwanda hivyo ni vya wabunge fulani wa Tanzania

----------
Sent via Nokia Email

------Original message------
From: Kamala J Lutatinisibwa <jlkamala@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, January 19, 2013 12:05:07 PM GMT+0300
Subject: Re: [wanabidii] TUJADILI UCHUMI

MJL, una point ila sijui kama itasound maana tulishaachana na mambo kama
hayo, tumelewa sifa za WB na IMF. gesi ya mtwara tunaipeleka dar kwenye
viwanda vikubwa na maduka ya wawekezaji na sio kendeleza mtwara kwanza kwa
kuipatia umeme wa uhakika na nishati za kupikia na kuwawezesha wanamtwara
kwanza kuwa na uhakika wa uzalishaji na kuanzisha viwanda vidogovidogo vya
mazao yao kwa kutumia umeme au gesi.

kuna barrier (belia) moja ya ushuru wa mazao bukoba vijijini wameweka
Tangazo (nikiweza nitalipiga picha) kwamba mwisho wa kusafiirisha mazao ni
saa 12 jioni. maana yake huruhusiwi kufanya kazi masaa 24, uchumi huo!

mtu unasafiri na basi kutokea mwanza kwenda Dar, mnalazimishwa kuingia kila
stend ya wilaya ili mkalipe 1000 ya ushuru.. vijistende mshenzi hivi
vingine viko mbali na barabara kuu na vingine barabara zake ni mbovu kama
kile cha igunga, nzega, kwa kutaja vichache wakati basi halina mshukaji
hapo, hmana jinsi ya kuokoa muda kwa kufanya malipo mbadala mpaka
kutupotezea muda huu?

mizani ya kupima mabas je? kwanini isiwe pande zote mbili za barabara ili
kuokoa muda kama ile ya kibaha? kuna gari la mafuta liliwahi kuungulia
kenye foleni ya mizani!

ttukiongelea uchumi sisi ni kutafuta wawekezaji wa nje ili waje kuchukua
mali huku sisi tukiambulia uvibarua tu. mkulima analima mazao yake then
anapangiwa soko na bei kama vile zao la kahawa, mahindi yanawaozea wakulima
kisa? serikali haitaki wayaxport badala ya kuwawezesha walime mengi zaidi
na kuuza zaidi na kupata chakula cha ziada. nchi zote zilizotuzunguka
hazina chakula cha kutosha wala ardhi ya kulima chakula hicho, sisi tunayo
ardhi na maji

wapi kuna mradi wa maana wa umwagiliaji ili tusitegemee mvua katika kilimo?
then tunalilia ajira kwa vijana! na mvua kutokunyesha  kama matatizo!
sasa jamaa wanataka tupunguze idadi wa udahiri kwenye vyuo vikuu kwa kuwa
eti waasomi wengi ajira kidogo, kwa nini kwa mfanyo tusiwekeze kwenye
kusomesha madaktari weengi then wakaenda kufanya kazi nje ya nchi na
kuleta  fedha za kigeni?

miradi isiyokosa pesa huwa ni ile ya ununuzi wa magari ya kifahali kwa
viongozi woote wa juu, ku-import fenicha, kununua masuti bila shaka,
kutalii kwa viongozi,, kununua mabomu na lisasi za kutumiminia
walalamikaji. hatuna legacy wala nini yaani ni bora liende tu. tukisifiwa
na watawala wa dunia na wakadai kumpenda raisi wetu tunajiona watoto
wazuuuuuri kinoma  ni hayo tu kwa sasa.



2013/1/19 mutabaazi lugaziya <mjlugaziya@mail.com>

>
> Ndugu zangu,
>
> Tangu tume"shauriwa" kuruhusu uchumi huria na kuachia ushindani, yaani
> biashara iwe ya ushindani(japo sisi hatukuwa na cha kushindanisha), ndipo
> viwanda vyetu vikabidi kufa.
>
> Kufa kwa viwanda kukapukutisha ajira kwa watanzania walio wengi.
> Kukosekana kwa ajira kukaenda sambamba na kupanda kwa gharama zote kutokana
> na serikali "kushauriwa" tena kuondoa ruzuku, nk.
>
> Tangu "tushauriwe" hivyo, kila uchao tunasifiwa kuwa uchumi unakua. Ukuaji
> wa uchumi wetu umejikita kwenye uzalishaji gani endelevu? Madini na miradi
> mingi ya wawekezaji inategemea rasilimali zinazoisha(diminishing
> resources). Dhahabu na almasi vikiisha, tutakwenda wapi, na haya madeni
> tunayolimbikiza kila siku, yatalipwa na nini?
>
> Mbona nchi zilizoendelea, hujulikana pia kama nchi zenye viwanda? Vya
> kwetu viko wapi, na tunaedeleaje kama taarifa zetu zote za kukua kwa uchumi
> hazizungumzii non-perishable activities kama hizo za viwanda? HIvi hakuna
> shida hapa? Wachumi watusaidie
>
> Naomba kuwasilisha wajameni!
>
> MJL
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>



--
kamala J Lutatinisibwa

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.





--
www.wejobs.blogspot.com Jobs in Africa
www.jobsunited.blogspot.com International Job Opportunities

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment