Sio kwamba natania , unajua serikali nayo inafanya biashara haiwezi kuwekeza sehemu tu bila kujua maslahi yake kwa siku zijazo na pia hali ya kusini haswa mtwara imekuwa tete kidogo kutokana na suala la usalama kumbuka ila vita ya kusini mwa afrika na hii choko choko ya mipaka inayoendelea kwa kipindi kirefu .
Tukitaka kuambiana ukweli mwengine watu watalia humu ndani .
2013/1/19 Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
Kwanza kwa sasa sidhani kama utapata ardhi Mtwara mjini. Yale maplot makubwa ya majumba ya zamani ya serikali, NHC etc kuna mahoteli. Ukanda wa bahari-mahoteli, peninsula za bahari ya Hindi Lindi hao customary owner waliopo huko na vibanda na vimnazi vyao naona watauza ardhi kwa mabilioni watu waweke mahoteli makubwa. Mtwara kumejaa wahindi, wachina, wasomali na kila jamii ya binadamu wanaotafuta kuwekeza. Mahelikopta ya huo utafiti wa mafuta na airwing yao ni tofauti na miaka ile. Utalii kuunganishwa na ule wa Kilwa Kisiwani-Mafia, Mikindani. Wale waliokando ya bahari Mikindani watanunuliwa watapata pesa za mtaji na wakitaka kuwa wabia. Mtwara-Lindi kuna maembe mengi anayonunua Bakhresa kwa sasa. Wakipanda mengi ya muda mfupi, kukazana na kilimo endelefu na ufuta na mtama unakuwa vizuri watauza value added crops. Bandari na daraja barabara kwenda Msumbiji na meli, lorries kwenda DSM hapo ni juhudi yao tu. Wakikazana na miradi ambayo ipo sasa kule ya Aga Khan, CONCERN, FAO, Janegoodal etc watafika mbali. Ila tu waache kukaa barazani kutwa longolongo. Bado hela za Mkuhumi. Wakianza uharibifu-watafukuza hawa wageni itakula kwao.
+255762544553/754763803Subject: [wanabidii] Re: MAANDAMANO MAKUBWA MTWARA - 19.01.2013To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, 19 January, 2013, 10:57Waachiwe waandamane ni haki yao ya msingi kuandamana na kusema mawazo
yao wako huru kabisa .
Uhuru wao unaishia pale wanapoanza ubinafsi wa kwanza hiki ni chetu
sio cha watanzania , watanzania wengine hawaruhusiwi kunufaika na hivi
na vile hiyo sio sahihi .
Lazima watambue maeneo ya kusini yanafaidika zaidi na mradi wa gesi na
mafuta kwa kipindi kirefu kijacho nitatoa mfano kidogo chini .
Bandari zao zitapanuliwa na kuwa kubwa kwa ajili ya biashara hii ya
mafuta na gesi , wataweza kuuza sio dsm tu maeneo mengine ya nchi na
nchi jirani haswa kusini mwa nchi kama Malawi , Zambia , msumbiji .
Kuna hoteli n huduma nyingine mbalimbali zitajengwa na zimeanza
kujengwa kutokana na sekta hii ya mafuta maeneo ya kusini kwa ajili ya
wafanyakazi na wadau wengine wa biashara maeneo hayo .
Vyuo vya ufindi na mashule yatajengwa kutokana na vipato vinavyotokana
na sekta hii kwa ajili ya kuandaa wafanyakazi wa sekta hii na nyingine
zinazofanana kwa kipindi kirefu .
Sasa wananchi wakianza maandamano sasa hivi na virugu wajue fursa
nyingi watapoteza , wawekezaji wanaotoa mitaji yao kwa ajili ya ujenzi
na miundombinu ya mafuta na mengine wanapenda kuhakikishiwa usalama
wao na wa mali zao kwanza ndio mengine yaendelee .
Waangalie wasije wakakosa vyote , wasipoangalia itakuwa kama north
mara na maeneo mengine ya migodi kwenye vurugu ambapo makampuni
yanaweka mageti makubwa walinzi na silaha wao utawaona kwenye ndege
kutoka na kuingia tu .
On Jan 19, 1:41 pm, Sylvanus Kessy <frke...@yahoo.com> wrote:
> Ndugu wanabidii
> Mzimu wa Gas unaendelea kuitafuna nchi, ukianzia huku Mtwara. Leo wananchi wamehamasishana Wilaya zote, za Lindi na Mtwara ili kupinga GAS ISITOKE Mtwara.
>
> Hakika Elimu na makubaliano yanahitajika. Viongozi wanaohusika watafute Hekima ya hali ya juu kutatua tatizo hili. Tukiendelea kusema ni wahuni watafanya mambo ya kihuni na tutapata hasara kubwa zaidi!
> sylvanus
--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

www.wejobs.blogspot.com Jobs in Africa
www.jobsunited.blogspot.com International Job Opportunities
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment