Saturday, 19 January 2013

Re: [wanabidii] TUJADILI UCHUMI

Tukubali tusikubali kuongoza nchi yenye madeni kama Tanzania hata mie kesho nikiingia madarakani kwa ukosefu wa umakini unaweza kuwa kama hawa jamaa. Unaingia benki kuu unakuta kweupeeeee, halafu serikali ya mapinduzi kule hawajalipa mshahara mwezi wa 3 kila kitu kinatoka serikali kuu. Jamaa wa IMF wanakupigia simu na kukuambia mr. Prezo kuna hela tulizisimamisha hapa kupisha uchaguzi tuko tayari kuzitoa ila kufuatana na research iliyofanyika nchi ya ulimwengu wa tatu kama yako kule amerika kusini it is our best interest kuona hiyo hela tunakupatia na wewe unaitumia kama tunavyotegemea uitumie. Hapa haijalishi kama mazingira ilikofanyika research hiyo yanaendana na nchi yetu au la hela inatolewa na wahuni kibao kama wataalam wanakuja,  hatujakaa sawa 75% imebaki kwa wahuni kule kule.

Hii kiini macho cha upuuzi wa mkukuta na mkurabita havikusaidia watanzania. Lakini cha kujiuliza kweli kila kitu cha uchumi ni lazima tupangiwe na watu wa nchi za nje? Wachumi wetu sidhani kama ni wabaya lakini matusi ya maraisi wetu kwa wasomi wa kitanzania nashawishika kuamini kuwa hata uandika karatasi nzuri yenye rangi za kuvutia zitaishia kwenye heavy cabinets nyuma ya waziri( mwanasiasa ) fulani amabe unaambiwa kila siku watu wa wilayani kwake wanampigia simu hali si nzuri uchaguzi ujao, GUESS WAT? kampenyezo kahela kakijitokeza hatakaacha.

Nchi inakuwaje na njaa wakati kuna mahala tunazalisha kupita kiasi? mwekezaji wa ndani hujengewi mazingira mazuri ya kutoa ushindani kwa mwekezaji kutoka nje kisa hujakaa kutoa 10% lakini atakuja muhuni toka Lebanon ati ananunua aridhi kwa ajili ya kulima kwenye bonde la rufiji hata kama hana capital baadae unasikia kumbe aridhi yenyewe iko na kiwese cha kufa mtu. Wananchi wanahamishwa pale miaka 15 hakuna kinachoendelea unajiuliza hawa wahuni toka jangwani nao wanakuja wekeza kwenye kilimo je hakuna watanzania ambao wangefanya vyema kuliko hao?

Wanaofanya mandundu haya tunawafahamu na dhambi zao zinajulikana ila wamejijengea empire kuubwa mno kiasi kwamba kuibomoa ni kazi matokeo nchi imejaa wachuuuzi na kila mtu anafanya deal kwa lugha nyepesi " bongo ya mishe mishe" na mfumo wa kodi ndo kichefu chefu kama kuendesha daladala kicheche

2013/1/19 Kamala J Lutatinisibwa <jlkamala@gmail.com>
MJL, una point ila sijui kama itasound maana tulishaachana na mambo kama hayo, tumelewa sifa za WB na IMF. gesi ya mtwara tunaipeleka dar kwenye viwanda vikubwa na maduka ya wawekezaji na sio kendeleza mtwara kwanza kwa kuipatia umeme wa uhakika na nishati za kupikia na kuwawezesha wanamtwara kwanza kuwa na uhakika wa uzalishaji na kuanzisha viwanda vidogovidogo vya mazao yao kwa kutumia umeme au gesi.

kuna barrier (belia) moja ya ushuru wa mazao bukoba vijijini wameweka Tangazo (nikiweza nitalipiga picha) kwamba mwisho wa kusafiirisha mazao ni saa 12 jioni. maana yake huruhusiwi kufanya kazi masaa 24, uchumi huo!

mtu unasafiri na basi kutokea mwanza kwenda Dar, mnalazimishwa kuingia kila stend ya wilaya ili mkalipe 1000 ya ushuru.. vijistende mshenzi hivi vingine viko mbali na barabara kuu na vingine barabara zake ni mbovu kama kile cha igunga, nzega, kwa kutaja vichache wakati basi halina mshukaji hapo, hmana jinsi ya kuokoa muda kwa kufanya malipo mbadala mpaka kutupotezea muda huu?

mizani ya kupima mabas je? kwanini isiwe pande zote mbili za barabara ili kuokoa muda kama ile ya kibaha? kuna gari la mafuta liliwahi kuungulia kenye foleni ya mizani!

ttukiongelea uchumi sisi ni kutafuta wawekezaji wa nje ili waje kuchukua mali huku sisi tukiambulia uvibarua tu. mkulima analima mazao yake then anapangiwa soko na bei kama vile zao la kahawa, mahindi yanawaozea wakulima kisa? serikali haitaki wayaxport badala ya kuwawezesha walime mengi zaidi na kuuza zaidi na kupata chakula cha ziada. nchi zote zilizotuzunguka hazina chakula cha kutosha wala ardhi ya kulima chakula hicho, sisi tunayo ardhi na maji

wapi kuna mradi wa maana wa umwagiliaji ili tusitegemee mvua katika kilimo? then tunalilia ajira kwa vijana! na mvua kutokunyesha  kama matatizo!
sasa jamaa wanataka tupunguze idadi wa udahiri kwenye vyuo vikuu kwa kuwa eti waasomi wengi ajira kidogo, kwa nini kwa mfanyo tusiwekeze kwenye kusomesha madaktari weengi then wakaenda kufanya kazi nje ya nchi na kuleta  fedha za kigeni?

miradi isiyokosa pesa huwa ni ile ya ununuzi wa magari ya kifahali kwa viongozi woote wa juu, ku-import fenicha, kununua masuti bila shaka, kutalii kwa viongozi,, kununua mabomu na lisasi za kutumiminia walalamikaji. hatuna legacy wala nini yaani ni bora liende tu. tukisifiwa na watawala wa dunia na wakadai kumpenda raisi wetu tunajiona watoto wazuuuuuri kinoma  ni hayo tu kwa sasa.



2013/1/19 mutabaazi lugaziya <mjlugaziya@mail.com>

Ndugu zangu,

Tangu tume"shauriwa" kuruhusu uchumi huria na kuachia ushindani, yaani biashara iwe ya ushindani(japo sisi hatukuwa na cha kushindanisha), ndipo viwanda vyetu vikabidi kufa.

Kufa kwa viwanda kukapukutisha ajira kwa watanzania walio wengi. Kukosekana kwa ajira kukaenda sambamba na kupanda kwa gharama zote kutokana na serikali "kushauriwa" tena kuondoa ruzuku, nk.

Tangu "tushauriwe" hivyo, kila uchao tunasifiwa kuwa uchumi unakua. Ukuaji wa uchumi wetu umejikita kwenye uzalishaji gani endelevu? Madini na miradi mingi ya wawekezaji inategemea rasilimali zinazoisha(diminishing resources). Dhahabu na almasi vikiisha, tutakwenda wapi, na haya madeni tunayolimbikiza kila siku, yatalipwa na nini?

Mbona nchi zilizoendelea, hujulikana pia kama nchi zenye viwanda? Vya kwetu viko wapi, na tunaedeleaje kama taarifa zetu zote za kukua kwa uchumi hazizungumzii non-perishable activities kama hizo za viwanda? HIvi hakuna shida hapa? Wachumi watusaidie

Naomba kuwasilisha wajameni!

MJL

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 



--
kamala J Lutatinisibwa

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment