Sunday 27 January 2013

Re: [wanabidii] SHULE ZA KATA NI MAKABURI YA KUZIKIA ELIMU YA WATOTO WA WALALAHOI!

Falsafa ya "Elimu Kwanza" ni kiini macho tu, nafikiri ni kutaka
kuwakumbusha watanzania kwamba akigombea wampime kwa mafanikio hayo.
Naomba kuwaambia kwamba Mzee Lowassa si muasisi wa shule za kata bali
yeye plan aliikuta tayari imeanza kutekelezwa. Alichofanya ni
kuiharakisha tu. Nikirudi kwenye mada kwamba Shule za kata ni makaburi
ya kuzikia elimu ya walalahoi. Kwa kiasi kikubwa ninamuunga mkono
ndugu Ryoba na kiasi kidogo simuungi mkono.

Kuanzisha shule za kata lilikuwa jambo jema kwa Tanzania na baadhi ya
vijana wameweza kupata elimu ya kuwawezesha kumudu maisha yao.
Kimsingi shule hizi zinatofautiana kati ya kata na kata kama ilivyo
kwamba mazingira ya kata zenyewe hayafanani. Kwa kiasi fulani
zimesaidia lakini yapo maeneo ambapo hazijasaidia. katika plani ni
jambo jema kwamba shule hizo zisingeanzishwa chini ya miembe inatakiwa
tuanze na majengo na baadaye kuongeza vingine ili ziitwe shule kama
alivyosema Ryoba.

Nijuavyo mimi zipo shule za kata ambazo tangu zimefunguliwa yapata
miaka kama nane iliyopita bado zina vyumba vya madarasa tu bila
majengo ya utawala wala maabara au majengo ya waalimu. Zina walimu
wachache sana ambao wamekata tamaa. Nikirudi kwenye msemo wa Ryoba
shule ikikaa miaka kama hiyo bila ya kuwa na maendeleo yoyote basi
itakuwa sahihi tukiita jina alilopendekeza Ryoba. Mtu anaweza kuamini
kwamba kwa vile hakuna kiongozi mkubwa ata mmoja mwenye mtoto katika
shule hizo ndiyo maana shule hizo haziendelezwi ipasavyo. Shule ili
iitwe shule lazima kuwepo na matukio ya ufundishaji na ujifunzaji
(palanned teaching and learning) uliopangiliwa kwa makusudi na walimu
waliosomea wakisaidiwa na vifaa vya kutumia(vitabu, maabara, chaki,
computer nk) with enabling environment. Kama wanafunzi wanakaa
darasani bila kuwa guided na watu waliosomea uwaalimu basi hizo si
shule bali inabidi ziitwe vijiwe kwa lugha ya mtaani. Majengo bila
watenda kazi na vitendea kazi hayatoshi kuitwa shule bali vijiwe.

Vijiwe vya namna hiyo vinaweza kuwa hatari kwa jamii maana
ukiwakusanya vijana lazima kuwe na shughuli ya kuwapa kama haipo
wanaamua kujipa wenyewe shughuli kama kujifunza kuvuta bhangi,
kujifunza wizi, kujifunza umalaya, kugombana na matendo mengine maovu.
Kwa namna hiyo zinakuwa shule lakini zisizofuata muhitasari uliopangwa
na hivyo kujivunza mambo yaliyo kinyume na matarajio. Inawezekana
baadhi ya matukio ya kuandamana na uvunjifu wa amani yakawa ndiyo
mafundisho wanayojifunza vijana wetu ndani shule zisizokuwa na vifaa
wala walimu wa kutosha. Wakati mwingine tukiporwa au kuona uvunjivu wa
amani mitaani kwetu tusilalamike hiyo ndo mitaala wanayojifundisha
vijana wetu kwenye baadhi ya shule zetu za kata zisizokuwa na sifa.
Tuelewe kwamba muda ni mali kuliko kuwakusanya vijana kwenye vikundi
(shule zisikuwa na kiwango) kwa muda wa miaka minne ni vyema
tukawaacha wakendelea kuishi vijijini kwao na kuutumia muda huo kwa
kazi nyingine zitakazowaletea manufaa mbeleni. TAFAKARI NA CHUKUA
HATUA

2013/1/26 <saidmdee@gmail.com>:
> Muasisi aka mzee lowasa alishaondolewa... He was the only guy who did know
> the meaning of SHULE ZA KATA... Nadhani kweli akisema elimu kwanza basi
> anamaanisha n anajua what to do...
> Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom
> ________________________________
> From: Gikaro Ryoba <rgikaro@yahoo.com>
> Sender: wanabidii@googlegroups.com
> Date: Sat, 26 Jan 2013 08:12:19 -0800 (PST)
> To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
> ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
> Subject: [wanabidii] SHULE ZA KATA NI MAKABURI YA KUZIKIA ELIMU YA WATOTO WA
> WALALAHOI!
>
> Mimi naomba niseme kwa sauti kubwa na bila kumung'unya maneno kwamba KWENYE
> KATA HAKUNA SHULE pale. Huwezi kuongelea SHULE mahali ambapo hakuna SHULE!
> Unajua shule ni nini? Shule inajumuisha madarasa (majengo), walimu,
> wanafunzi, vifaa vya kufundishia na kujifunzia, mazingira (surrounding), nk.
> Sasa niambie hizo mnazoziita shule za kata kama zinavyo vitu vyote
> nilivyovitaja hapo juu. Ni kama vile unapoweza kununua kitambaa, ukakiita
> nguo wakati bado hakijashonwa ili kufikia hadhi ya kuitwa nguo! Pale kwenye
> kata kuna majengo (sema magofu) ambamo vijana wanaomaliza (sio wanaofaulu)
> darasa la saba wanajazwa na kujipumzikia kwa kipindi cha miaka minne.
>
> Ndio maana 'wanafunzi' wengi (zaidi ya 90%) wanaohitimu kwenye 'shule' hizi
> hufaulu kwa kiwango cha daraja la nne (kwa alama 33 na kuendelea) au daraja
> la sifuri (zaidi ya alama 35). Serikali haikuwa na malengo ya kueleweka
> pindi wanaanzisha hizi 'shule' —lilikuwa ni wazo la kisiasa tu ili waendelee
> kupewa kura na kujikita madarakani. Kama hayo magofu ya kwenye kata ni SHULE
> ni kwa nini mafisadi hawasomeshi watoto wao huko? Mbona wao wanasomesha
> watoto wao kwenye 'international academies'? Kwa nini wasiwalete watoto wao
> nao 'wakosome' kwenye hizo shule? Hili ndiyo swali la kujiuliza. Huwezi
> kunipa sumu kwa kuniaminisha kwamba ni chakula wakati wewe na wanao hamli
> hiyo sumu.
>
> Katika kuonesha msisitizo kwamba shule za kata ni makaburi ya kuzikia elimu
> ya watoto wetu, Rais kikwete aliwahi kunena kwamba "watoto wanaosoma kwenye
> shule za kata watakuwa wakulima, wafugaji na wazazi wazuri pindi
> wakihitimu". Hii maana yake ni kwamba, hategemei kwamba kuna wanafunzi wa
> kutosha wanaoweza kupenya kutoka kwenye hizo shule wakaendelea na masomo ya
> juu zaidi ya hapo. Hata yeye alishasoma alama za nyakati akaona kwamba hizi
> shule hazina tija yoyote zaidi ya kuzalisha wakulima na wazaaji wazuri!
> Wanaume wakihitimu wataenda kwenye kilimo na wale wa kike wataenda kwenye
> kuolewa na kuzaa - na watakuwa walezi wazuri wa watoto kuwa wameishapata
> elementary knowledge juu ya reproductive health, child care and human
> nutrition. Hayo tu, basi! Hawasogei zaidi ya hapo.
>
> Pia naomba niseme kwamba 'mtu mwenye nusu elimu' ni mbaya kuliko yule
> asiyekuwa nayo kabisa. Msitegemee kwamba watoto wetu (kama wapo) watakaopata
> 'nusu elimu' kwamba itawafikisha popote. Na ndiyo maana hata Mh Rais
> aliliona hilo na kulisemea bila kumung'unya maneno. Ila kwa kuwa watanzania
> ni wagumu wa kuleewa na wepesi wa kusahau, itachukua muda kufahamu dhana
> hiyo ya Rais. Ni bora kumyima mtu elimu moja kwa moja kuliko kumpa nusu
> elimu.
>
> Serikali imechakachua ubora wa hizi shule hadi inakuwa vigumu kuchuja watoto
> wanaojua kusoma na kuandika. Kuma. Alama za ufaulu zilishushwa hadi 65 kwa
> 250 ili walau kupata watoto wa kujaza 'magofu ya kata' mnayoyaita shule. Hii
> ni aibu. Mtoto anayepata alama 65 kati ya 250 (wastani wa alama 65/5 = 13
> kwa 100) atachaguliwaje kujiunga na elimu ya sekondari?. Mtoto atapataje
> wastani wa alama 13/100 halafu achaguliwe kwenda sekonfdari 'kujaza nafasi'?
> Hawa si ndio wale wasojua kusoma na kuandika? Nakumbuka enzi zile za mwalimu
> Nyerere hakukuwa na ubabaishaji kama huu. Mtu ukienda sekondari unakuwa
> kichwa kweli.
>
> Kumbuka kwamba wananchi wanajitahidi sana kuchangia elimu lakini serikali
> haichangii chochote (hakuna walimu, vitabu, vifaa vya kufundishia, mazingira
> bora kwa wanafunzi, nk). Serikali inachojua ni kununua magari ya kifahari na
> vitu vingine vya anasa. Kila siku serikali wakitakiwa kuborsha elimu,
> wanadai hawana pesa. Pesa za anasa, kulipana posho na za kuficha uswisi
> zinatoka wapi? Halafu mtu anakuja kusimama mbele ya umma anatetea udhaifu wa
> serikali, Tumueleweje?
>
> Kazi ya wananchi wa kawaida ni kulipa kodi ambayo tungetegemea itumike
> kuboresha huduma za jamii. Badala ya kutumiwa kuboresha huduma za jamii
> (shule, elimu, maji, nk), zinatumiwa na mafisadi kujaza matumbo yao makubwa
> - ambayo hayajai kamwe!
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment