Saturday 19 January 2013

Re: [wanabidii] Natamani kuwa mwanasiasa

Victor kama kweli unataka kuwatumikia wananchi ziko njia nyingi sana, lazima utakuwa umejiona unakipaji cha uongozi au watu wamekuona hivyo unahisi ni muda wa kuangaza nyota yako hiyo uliojaliwa. Mie ningeshauri anza katika level ndogo katika mazingira yaliokuzunguka fanya mambo badiliso mtitazamo ya watu wako. Wafunguo macho waone kuanyomambo mengi wanaweza fanya si kutegemea serikali kwa kila kitu. Mfano kiunadhambi gani kujenga nyumba nzuri za walimu kwa shule za kata kunakoweza shawishi walimu wanaopangwa kazi huko kwenu wabaki na kuwafundisha watoto wenu badala ya wanavyokimbia vituo vyao vya kazi sababu ya kukosa hata mahala pa kulala.

Waonyeshe wananchi wako raslimali zao na jinsi wanavyoweza kuzitumia kuendeleza familia zao. Peleka mabadiliko ya elimu, kuwa chanzo cha usuruishi wa migogoro mbali mbali huo uwakilishi utakuja wenyewe and that is how u can build ur legacy


2013/1/17 Victor Mwita <victormwita@gmail.com>

Ndugu wadau
Kwa muda mrefu nimetamani kuwa mwanasiasa nikiwa na lengo la kuwawakilisha wananchi wenzangu mjengoni na katika fursa mbalimbali ndani na nje ya nchi. Ni kweli kwamba huko nilikozaliwa kuna matatizo ya msingi ambayo kwa miaka mingi hayajawahi kutatuliwa. Tatizo kubwa ni siasa na vyama vyake katika nchi hii. Ili kutumiza azma yako inabidi ku-sacrifice sana muda, rasilimali (fedha) na utu wako kwa chama chako but hayo yote hayakuhakikishii kuendelea kubaki katika chama. Wakati wa kutafuta ticket ya chama ili uwe mgombea wa nafasi yoyote kuna mizengwe kibao!! Kubwa mno ni hii tabia ya watanzania kutaka uwape kitu kwanza ili ukawawakilishe!
Kwenye vyama nako kumejaa watu wa kila aina. Mwanzoni nilidhani vijana wanaoingia katika siasa wako serious kutaka kuleta maendeleo katika nchi hii, kumbe wanatafuta ajira na fedha. Ndio maana wananunulika na wanasiasa wazee na kuishia kujaribu kuharibu sifa za vyama vyao.
Mambo haya yananifanya nianze kupata wasi wasi na mustakabali wa siasa za nchi yetu. Najiuliza maswali kadhaa yasiyo na majibu. Kubwa zaidi ni hili na wananchi kuhitaji kitu kidogo kutoka kwa wagombea kabla ya kuwachagua. Je waliochaghuliwa watakuwa wanawawakilisha hao wapiga kura waliohongwa au wanaenda kutimiza matakwa yao? Labda ndio maana wawakilishi wetu wakishafika mjengoni wanafanya kila wawezalo kujiongezea posho na mishahara mikubwa ili kupata mitaji wa kwenda tena kununua kura next elections. Tumeona wawakilishi huko Kenya walijiandalia pension ya nguvu. Na ninaamini hata hapa kwetu hilo linakuja.
Vijana amkeni msimamie hatma ya nchi yetu. Kumbukeni the country is bigger than the individual. Msitumike kuvuruga vyama vyenu kwa faida yetu sisi ambao miaka yetu inaelekea mwisho lakini bado tuna uroho wa madaraka. Fikiria iweje wewe kijana mzee akupe vijisenti kidogo ili akutumie kuharibu carrier yako yote katika siasa?! Just say no and stay focused.
Bado najiuliza kama niingie katika siasa za huko kwetu na niingie kwa style gani
--
Victor Caleb Mwita
P.O. Box 9152
Dar Es Salaam

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment