Nikubaliane nawewe kuwa kuna kudharauliana kwingi kati yetu waTz. Utaona hata hapa jukwaani watu walivyo wepesi kudadavua uwezo wa mtu hata pale fani ya huyo mtu mchangiaji ni "innocent" kabisa. Hii ni sifa kubwa ya ujinga wetu, tunaangalia nani kasema badala ya nini kimeongelewa!
Tunafika hadi kudharau watu performers bila msemaji kutoa au kujielewa kuwa huenda yeye ndiye mjinga au mhurumiwa wa umbumbumbu kwenye fani husika. Imefikia hadi an undergrad anadharau a graduate kwenye fani yake au chuo alichosoma au mfumo alioutumia kupata elimu. Waelevu wa kielimu hawajiingizi kwenye mabishano kama hayo kwavile kila mtu aliyepata elimu na kupita hithibati, anayo elimu aliyoipata na kwa maeneo mengine anayebisha huenda akawa mwanafunzi wa huyo anayedharaulika!
KEMS, point ambayo nimeieleza hapo awali ni ya uhusishwaji wa fani tofauti tofauti kwenye miradi yetu; unakuta wizara moja ambayo ina wataalamu wa sekta fulani kuona wanajitosheleza kwenye miradi bila kuhusisha sekta au utaalaam toka sekta nyingine. Ndipo nikasema huenda sekta za uchumi na biashara hazijahusishwa na wasimamizi wa mradi wa gesi kwenye kupata muafaka wa mradi unaohusisha sekta tofauti.
Mfano utayarishaji wa wananchi wa Mtwara ungefanyika mapema na wakaelewa faida na hasara ya mradi kwenye nyanja zote. Wataalam wa jamii na maendeleo vijijini nao wangehusika na hata taasisi za kiraia kwenye utayarishaji wa wananchi.
Makosa haya yanafanyika kila siku, hata kwenye ujenzi wa barabara, hawahusishi sekta nyingine ukiacha EIA, kitu kinachoangalia mazingira zaidi ya other socioeconomic au socio-political impact ya miradi.
Hapa ndipo upweke wa uelewa wa wataalam wetu unapoanza kuonekana kwa hali zote na sijui hili la kujiamini sana kwa fani moja na kupuuza fani nyingine linatoka wapi! Lakini ndicho kinachojitokeza mwisho wa siku kutoonekana uzuri wa mradi kwa jamii moja au zote.
Tatizo jingine ni kutanguliza mbele sana fedha! Unakuta mradi uliosanifiwa miaka 10 iliyopita ukakwama kwa ukosefu wa fedha, ghafla unaanzishwa baada ya fedha kupatikana bila kupitiwa upya kujua kama bado unahitajika na kwa kiwango kipi mahitajio ya vipengele vya mradi vinatakiwa kubadilishwa au la. Hapa utaona mdudu rushwa au ufisadi unatawala maamuzi ya leo na kudharau umuhimu wa mapitio ya mradi. Hii inaonekana kuathiri miradi mingi mipya iliyotekelezwa kwa misingi hii.
Huenda kuna siku tutabadilika baada ya makosa makubwa na madhara makubwa kama ilivyo mtwara kwa sasa kutokea!
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
From: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Date: Sun, 27 Jan 2013 05:11:10 +0000 (GMT)
To: tony_uk45@yahoo.co.uk<tony_uk45@yahoo.co.uk>; wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Subject: Re: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam
Tony PT
Nashukuru kwa maoni yako. Ninavyoelewa mimi CHINA wanataka kusaidia sana katika nchi za kiafrica kwa vile wanataka kuliteka soko hivi kwa miaka ijayo. Lakini huenda mkakati wao wanamanufaa nao pia. Kwamba utakapofika wakati basi kuwe na mahitaji makubwa ya wao kwa kuwa ndio wanakuwa wanajua walichokifanya katika miradi husika.
Chukulia kwa mfano uwanja wa taifa, kwa mtizamo wangu kama mtanzania wa kawaida viti vilivyowekwa havikuwa vya kiwango kile walivyoweka katika viwanja vya kwao. Hapa nafikiri walitaka (na wameweza) kutengeneza soko la baadaye. Na ukiangalia sana utaona kwamba ili nchi nyingine ziweze kutoa viti vya kurekebisha pale ni lazima kuwe na uzalishaji mpya kwa vile vipimo kidogo vinapishana na standard zinzokubalika.
Huko china kuna kazi pia zinazofanyika lakini zinafail. Ninayo mifano ya madaraja na barabara yaliyoanguka au kubomoka baada tu ya kujengwa. bahati yao ni kuwa kila wanapojenga wanatunza kumbukumbu kiasi kwamba kabla ya kuchukua hatua kufuatilia tatizo lilikuwa wapi. Ikitokea kwamba kilichosanifiwa ni tofauti na kilichojengwa basi hatua huchukuliwa.
Sina hakika sana na adhabu ya kifo ambayo mara zote imekuwa ikitamkwa hapa. kwa hiyo sina uwezo wa kuijadili. Ninachofahamu ni kuwa hatua zinachukuliwa ikiwa ni pamoja na kifungo ambacho wengine wanakuja huku kwetu ni wataalamu lakini wako katika vifungo na kutmika kufanya kazi. Huenda ni uataratibu mzuri lakini sijui kama forced labour inaweza kuwa na productivity nzuri, hili nal;o linahitaji mjadala wake.
Nije kwa mradi wa GAS Mtwara, kwa taarifa nilizo nazo mimi wahisani walitaka ije DSM kwa vile kwao ni biashara ya ajira kwa watu wao na Tanzania ingepewa fedha nyingi pamoja na kuwa haina riba kubwa lakini itakuwa imeongeza kiwango cha madeni kwa nchi husika kwa hiyo hapo baadaye ingewezekana kuwa na uhakika wa kuwekeza katika maeneo nyeti. Lingine ambalo sina uhakika nalo sana ni kuwa katika sehemu ambazo bomba lingepitia kuna uwezekano wa madini ya URANIUM na mengine kama Corbat nk hasa sehemu za Lindi na jirani na bonde la Rufiji. Huenda katika kuchimba na kuchukua madini hayo gharama yao ingerudi na hivyo kazi hiyo ingefanyika kwa hasara.
Hoja ya uzembe kwa wasomi wetu wetu mara nyingi mimi siiafiki sana. Unajua Tony, tunao wasomi wazuri sana. Na mara nyingi wamekuwa watumishi wazuri sana huko wanakokuwa wameajiriwa. Inakuwaje sasa wanapokuja hapa usomi wao haueleweki wala hauwasaidii wananchi wenzao?
Chukulia mfano Prof. Muhongo. Niliwahi kuhudhuria presentation yake kuhusu ujenzi wa Chuo Kikuu pale Musoma. Hoja ya Mkoa ilikuwa kujenga Chuo Kikuu cha Waalimu lakini akaja na wazo la kujenga chuo kikuu cha Bio - Science. Wote tuliokuwepo tulimkubali sana jinsi alivyokuwa anajenga hoja yake. wakati huo alikuwa SA katika Tume ya Science ambayo kama sikosei ndiko alikokuwa hadi uteuzi wake kama Mbunge na Waziri.
Huenda tatizo lipo jingine ambalo inabidi tutafute kwa nini wasomi wetu hawakubaliki nyumbani. Tukijua hili na kulifanyia kazi tunaweza kujenga heshima yao na kujiamini kiasi kwamba tutakuwa tayari kuwasikiliza na wao kutusikiliza. Ilivyo kwa sasa kuna uadui mkubwa kati ya wasomi na wananchi wa kawaida. Siku zote wananchi wanadhani wasomi wanawadanganya na wasomi anaona kwamba wananchi hawaelewi. Tukiweka sawa hapo naamini tutakwenda.
kazi ya msingi ninayoiona hapa ni kuweka sawa kwanza uwanja wa maelewano kati ya wananchi na viongozi wao kisha mjadala uendelee wa jinsi ya kufanya. Timu ya wataalamu ikae iangalie nini cha kufanya halafu kuwekwe mazingira ya kukaa pamoja kila upande ukitoa hoja na kupata majibu kisha utakelezaji ukianza kila mtu ashiriki upande wake.
Njia hii inatumiwa sana na Wajapani. japani hata mtu pale anapotaka kubadilisha matumizi ya eneo lake au hata serikali hushirikisha wananchi. Matangazo hutolewa, michoro huandaliwa na kuwekwa hadharani na kwenye mitandao yao. wananchi wanatoa maoni yao na majibu yanatolewa kisha kunakuwa na siku ya kukutana pamoja na kujadiliana kwa pamoja. watumishi wa eneo hilo hupewa ruhusa kuhudhuria na kutoa michango yao. Huenda hawa wako katika kiwango cha juu cha ushirikishaji wa jamiii, lakini bado tunaweza kuanzia mahali.
Samahani kwa maelezo mafupi kiasi hiki.
K.E.M.S.
From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>
To: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Sent: Saturday, 26 January 2013, 8:22
Subject: Re: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam
To: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Sent: Saturday, 26 January 2013, 8:22
Subject: Re: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam
Ezekiel,Mikopo ya kichina haina shinikizo kama ya nchi za magharibi; wanachojali sana sana ni maslahi yao. Huo mkopo ni maombi ya Tanzania kwa kushauriwa na wataalam ambao au hawajaiva au nao kwa maslahi yao. Ukumbuke mara nyingi nchi yetu huletewa wataamu wengi wao ni toka 2nd world, sio premium! Nawaheshimu sana Ethiopia ambao kwa miradi yao mingi wataalam ni wao na akikosea mtu na kuitia hasara serikali anapotelea kuzimu! Wanakuwa very careful na they always score best. Injinia aliyejenga uwanja wa ndege wa Addis nasikia alipotea baada ya uwanja kufunguliwa na ukawa unavuja sana ikinyesha mvua! Hapa njaa, rushwa na kutoelewa mambo kunatuponza sana!
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
From: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Date: Sat, 26 Jan 2013 15:37:50 +0000 (GMT)
To: tony_uk45@yahoo.co.uk<tony_uk45@yahoo.co.uk>
Subject: Re: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam
Tony Nakusihi usikatee tamaa, nchi hii ni yetu wote.lazima tuisaidie kwa.kadri tuwezavyo. Sijui kama kuna mtu anaweza kutusaidia kuangalia gharama za kujenga mitambo ya kuzaalisha umeme Mtwara na gharama.za.kuusafirisha na kuunganisha na Grid ya taifa hapa DSM halafu ilinganishwe na gharama ya kuleta hiiyo.Gas kwa maana ya mabomba. Kwa uamuzi wa.kiserikali nadhani kama uamuzi ulikuwa tayari huko.nyuma nafikiri Ngeeleja asingeweza kuubadilisha ukizingatia kuwa mara nyingi tumekuwa tunasukumwa kufanya mambo yetu ya.kiuchumi kwa.matakkwa ya.wawekezaji.au wahisani. Usije ukakuta kwamba kwa.kuwa.fedha yenyewe ni ya mkopo basi masharti yake yalikuwa haya yaanayotiletea msuguano kama wananchi kwa upande mmoja na Serikali kwa upande mwingine. Maamuzi.ya.wahisani mara zote.yamekuwa.na.athari kubwa katika chumi za nchi nyingi zinzoendelea, mfano rahisi tu ni hapa kwetu tulipoambiwa kuuza nyumba zote za.Serikali na kuacha hakuna utaratibu maalumu.wa.watumishi.wapya.wanapohaamia inuwaje. Serikali imekuwa inaingia hasara kubwa kihifadhi watu hasa mawaziri katika hoteli kubwa kwa kipindi kirefu. Jambo pia liloingia naaufisadi yake. Nina hakika hata kama tukiridhia kkama taifa kujenga mfumo wa.uzalishajii umeme hapo Mtwara ili kuvutia wawekezaji kama si matakwa ya wakubwa itakuwaa kaama barabara ya kwenda huko ilivyokwama kukamilika kwa kuwa kwao siyo Priority. Naogopa isije tumia fedha nyingi lakini mtambo usifanye kazi kwa muda mrefu ikawa kama maamuzi ya kuhaamia Dodoma yalivyo. Sina hakika na hoja yako ya kutojituma. Kwa.nini nasema.hivyo. Ni kwamba inategemea mwingine anakuanggalia vipi. Mimi naweza kujituma.sana kulima bangi kwa kuwa nikiiuza nitapata fedha za.kikidhi mahitaji yangu lakini mwingine ataona unafanya mzaha na kejeri kwaupande mwingine. Au niseme kwamba yawezekana tukawaona wale.kwamba hawakujituma kwa vile.kwa.sasa tunao mtizamo mmwingine. Hojja ya kuzalisha umeme Mwanza nakimbuka ilipoibuka hoja hiyo Serikali ilisema kwamba itatumia njia ya reli. Na.wakati huo reli ilikuwa inaaminika na.mazingira ya kufanyia kazi hayakuwa kama yalivyo leo. Kiwango cha uwajibikaji kinachodaiwa na wananchi kwa viongozi wao kkiko juu sana. Pia wakati huo ilidsiwa kwamba Mwanza kulikuwa na mitambo ya kuanzia kazi ya uzalishaji wa umeme na tatu lengo ilikuwa kuwa na.uwezo.wa kuuza umeme wetu kwa nchi zinzopakana na ziwa hili ikiwemo Rwanda na Burundi. Msisitizo.wa hoja yangu hapa.ni kwamba huenda kulikuwaa.na msukumo kutoka njekwa hiyo uwezo.wetu wa kufikiri na kuamua ukafungwa kapuni na kusubiri mwenye kutoa ndio afanye na maamuzi.ninj kifanyike. Nafikiri mwafaka utapatikana kwa kuangaalia upya mpango wetu kwa.sasa una manufaa gani kuendelea kuleta Gas DSM au kujenga mtambo wa umeme hapo Mtwara na kufikiria kuiiuzia hata Msumbiji. Mwishho wa yote lazima tubakie kama nchi moja Tony ambapo.watoto..wetu.na wajukuu watapata nafasi ya kuishi kwa.amani na ffuraha na kufaidi mali za nchi yao kwa umoja na mshikamano kama Tanzania. Sent from Yahoo! Mail on Android |
From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>;
To: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>;
Subject: Re: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam
Sent: Sat, Jan 26, 2013 2:00:27 PM
To: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>;
Subject: Re: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam
Sent: Sat, Jan 26, 2013 2:00:27 PM
Ezekiel, Upo sahihi kabisa, lakini kupuuzia kuko kwingi maana ushauri wa kujenga generation Mtwara ulitolewa siku nyingi pia. Wakashauriwa kuwa generation ya umeme mtwara utafaidisha liganga na baada ya generation ya Mchuchuma (from coal) ungeongeza density ya power kwenye grid. Hawajasikia, na aliyeanza kubadili mambo ni Mramba alipokuwa viwanda. Akina Ngereja nao hawakujiongeza na kubadili maamuzi ya awali kulingana na hali ya sasa. Mkusanyiko wa makosa ya maamuzi ya kisaidiwa na makosa ya kutojituma yametufikisha hapa leo! Kwa hili siwezi kusamehe, maana hata maamuzi ya kujenga 100mW huko mwanza yalipingwa kwani supply ya heavy oil italeta madhara ya barabara na uzalishaji wa umeme wa aghali sana kutokana na overhead cost nyingi. Walishauriwa waimarishe uzalishaji umeme Songosongo na Mchuchuma na pia njia ya kusafirisha umeme kupitia Tabora, Shy, Mwz na Mara. Sikio la kufa halisikii dawa! Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network. From: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk> Date: Sat, 26 Jan 2013 13:21:02 +0000 (GMT) To: tony_uk45@yahoo.co.uk<tony_uk45@yahoo.co.uk> Subject: Re: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam
From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>; To: <wanabidii@googlegroups.com>; Subject: Re: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam Sent: Sat, Jan 26, 2013 12:12:54 PM
|
0 comments:
Post a Comment