Saturday, 26 January 2013

Re: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam

Tony PT
 
Nashukuru kwa maoni yako. Ninavyoelewa mimi CHINA wanataka kusaidia sana katika nchi za kiafrica kwa vile wanataka kuliteka soko hivi kwa miaka ijayo. Lakini huenda mkakati wao wanamanufaa nao pia. Kwamba utakapofika wakati basi kuwe na mahitaji makubwa ya wao kwa kuwa ndio wanakuwa wanajua walichokifanya katika miradi husika.
 
Chukulia kwa mfano uwanja wa taifa, kwa mtizamo wangu kama mtanzania wa kawaida viti vilivyowekwa havikuwa vya kiwango kile walivyoweka katika viwanja vya kwao. Hapa nafikiri walitaka (na wameweza) kutengeneza soko la baadaye. Na ukiangalia sana utaona kwamba ili nchi nyingine ziweze kutoa viti vya kurekebisha pale ni lazima kuwe na uzalishaji mpya kwa vile vipimo kidogo vinapishana na standard zinzokubalika.
 
Huko china kuna kazi pia zinazofanyika lakini zinafail. Ninayo mifano ya madaraja na barabara yaliyoanguka au kubomoka baada tu ya kujengwa. bahati yao ni kuwa kila wanapojenga wanatunza kumbukumbu kiasi kwamba kabla ya kuchukua hatua kufuatilia tatizo lilikuwa wapi. Ikitokea kwamba kilichosanifiwa ni tofauti na kilichojengwa basi hatua huchukuliwa.
 
Sina hakika sana na adhabu ya kifo ambayo mara zote imekuwa ikitamkwa hapa. kwa hiyo sina uwezo wa kuijadili. Ninachofahamu ni kuwa hatua zinachukuliwa ikiwa ni pamoja na kifungo ambacho wengine wanakuja huku kwetu ni wataalamu lakini wako katika vifungo na kutmika kufanya kazi. Huenda ni uataratibu mzuri lakini sijui kama forced labour inaweza kuwa na productivity nzuri, hili nal;o linahitaji mjadala wake.
 
Nije kwa mradi wa GAS Mtwara, kwa taarifa nilizo nazo mimi wahisani walitaka ije DSM kwa vile kwao ni biashara ya ajira kwa watu wao na Tanzania ingepewa fedha nyingi pamoja na kuwa haina riba kubwa lakini itakuwa imeongeza kiwango cha madeni kwa nchi husika kwa hiyo hapo baadaye ingewezekana kuwa na uhakika wa kuwekeza katika maeneo nyeti. Lingine ambalo sina uhakika nalo sana ni kuwa katika sehemu ambazo bomba lingepitia kuna uwezekano wa madini ya URANIUM na mengine kama Corbat nk hasa sehemu za Lindi na jirani na bonde la Rufiji. Huenda katika kuchimba na kuchukua madini hayo gharama yao ingerudi na hivyo kazi hiyo ingefanyika kwa hasara.
 
Hoja ya uzembe kwa wasomi wetu wetu mara nyingi mimi siiafiki sana. Unajua Tony, tunao wasomi wazuri sana. Na mara nyingi wamekuwa watumishi wazuri sana huko wanakokuwa wameajiriwa. Inakuwaje sasa wanapokuja hapa usomi wao haueleweki wala hauwasaidii wananchi wenzao?
 
Chukulia mfano Prof. Muhongo. Niliwahi kuhudhuria presentation yake kuhusu ujenzi wa Chuo Kikuu pale Musoma. Hoja ya Mkoa ilikuwa kujenga Chuo Kikuu cha Waalimu lakini akaja na wazo la kujenga chuo kikuu cha  Bio - Science. Wote tuliokuwepo tulimkubali sana jinsi alivyokuwa anajenga hoja yake. wakati huo alikuwa SA katika Tume ya Science ambayo kama sikosei ndiko alikokuwa hadi uteuzi wake kama Mbunge na Waziri.
 
Huenda tatizo lipo jingine ambalo inabidi tutafute kwa nini wasomi wetu hawakubaliki nyumbani. Tukijua hili na kulifanyia kazi tunaweza kujenga heshima yao na kujiamini kiasi kwamba tutakuwa tayari kuwasikiliza na wao kutusikiliza. Ilivyo kwa sasa kuna uadui mkubwa kati ya wasomi na wananchi wa kawaida. Siku zote wananchi wanadhani wasomi wanawadanganya na wasomi anaona kwamba wananchi hawaelewi. Tukiweka sawa hapo naamini tutakwenda.
 
kazi ya msingi ninayoiona hapa ni kuweka sawa kwanza uwanja wa maelewano kati ya wananchi na viongozi wao kisha mjadala uendelee wa jinsi ya kufanya. Timu ya wataalamu ikae iangalie nini cha kufanya halafu kuwekwe mazingira ya kukaa pamoja kila upande ukitoa hoja na kupata majibu kisha utakelezaji ukianza kila mtu ashiriki upande wake.
 
Njia hii inatumiwa sana na Wajapani. japani hata mtu pale anapotaka kubadilisha matumizi ya eneo lake au hata serikali hushirikisha wananchi. Matangazo hutolewa, michoro huandaliwa na kuwekwa hadharani na kwenye mitandao yao. wananchi wanatoa maoni yao na majibu yanatolewa kisha kunakuwa na siku ya kukutana pamoja na kujadiliana kwa pamoja. watumishi wa eneo hilo hupewa ruhusa kuhudhuria na kutoa michango yao. Huenda hawa wako katika kiwango cha juu cha ushirikishaji wa jamiii, lakini bado tunaweza kuanzia mahali.
 
Samahani kwa maelezo mafupi kiasi hiki.
 
K.E.M.S.
From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>
To: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Sent: Saturday, 26 January 2013, 8:22
Subject: Re: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam
Ezekiel,Mikopo ya kichina haina shinikizo kama ya nchi za magharibi; wanachojali sana sana ni maslahi yao. Huo mkopo ni maombi ya Tanzania kwa kushauriwa na wataalam ambao au hawajaiva au nao kwa maslahi yao. Ukumbuke mara nyingi nchi yetu huletewa wataamu wengi wao ni toka 2nd world, sio premium! Nawaheshimu sana Ethiopia ambao kwa miradi yao mingi wataalam ni wao na akikosea mtu na kuitia hasara serikali anapotelea kuzimu! Wanakuwa very careful na they always score best. Injinia aliyejenga uwanja wa ndege wa Addis nasikia alipotea baada ya uwanja kufunguliwa na ukawa unavuja sana ikinyesha mvua! Hapa njaa, rushwa na kutoelewa mambo kunatuponza sana!
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
From: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Date: Sat, 26 Jan 2013 15:37:50 +0000 (GMT)
To: tony_uk45@yahoo.co.uk<tony_uk45@yahoo.co.uk>
Subject: Re: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam

Tony
Nakusihi usikatee tamaa, nchi hii ni yetu wote.lazima tuisaidie kwa.kadri tuwezavyo. Sijui kama kuna mtu anaweza kutusaidia kuangalia gharama za kujenga mitambo ya kuzaalisha umeme Mtwara na gharama.za.kuusafirisha na kuunganisha na Grid ya taifa hapa DSM halafu ilinganishwe na gharama ya kuleta hiiyo.Gas kwa maana ya mabomba.
Kwa uamuzi wa.kiserikali nadhani kama uamuzi ulikuwa tayari huko.nyuma nafikiri Ngeeleja asingeweza kuubadilisha ukizingatia kuwa mara nyingi tumekuwa tunasukumwa kufanya mambo yetu ya.kiuchumi kwa.matakkwa ya.wawekezaji.au wahisani.
Usije ukakuta kwamba kwa.kuwa.fedha yenyewe ni ya mkopo basi masharti yake yalikuwa haya yaanayotiletea msuguano kama wananchi kwa upande mmoja na Serikali kwa upande mwingine.
Maamuzi.ya.wahisani mara zote.yamekuwa.na.athari kubwa katika chumi za nchi nyingi zinzoendelea, mfano rahisi tu ni hapa kwetu tulipoambiwa kuuza nyumba zote za.Serikali na kuacha hakuna utaratibu maalumu.wa.watumishi.wapya.wanapohaamia inuwaje. Serikali imekuwa inaingia hasara kubwa kihifadhi watu hasa mawaziri katika hoteli kubwa kwa kipindi kirefu. Jambo pia liloingia naaufisadi yake.
Nina hakika hata kama tukiridhia kkama taifa kujenga mfumo wa.uzalishajii umeme hapo Mtwara ili kuvutia wawekezaji kama si matakwa ya wakubwa itakuwaa kaama barabara ya kwenda huko ilivyokwama kukamilika kwa kuwa kwao siyo Priority. Naogopa isije tumia fedha nyingi lakini mtambo usifanye kazi kwa muda mrefu ikawa kama maamuzi ya kuhaamia Dodoma yalivyo.
Sina hakika na hoja yako ya kutojituma. Kwa.nini nasema.hivyo. Ni kwamba inategemea mwingine anakuanggalia vipi. Mimi naweza kujituma.sana kulima bangi kwa kuwa nikiiuza nitapata fedha za.kikidhi mahitaji yangu lakini mwingine ataona unafanya mzaha na kejeri kwaupande mwingine. Au niseme kwamba yawezekana tukawaona wale.kwamba hawakujituma kwa vile.kwa.sasa tunao mtizamo mmwingine.
Hojja ya kuzalisha umeme Mwanza nakimbuka ilipoibuka hoja hiyo Serikali ilisema kwamba itatumia njia ya reli. Na.wakati huo reli ilikuwa inaaminika na.mazingira ya kufanyia kazi hayakuwa kama yalivyo leo. Kiwango cha uwajibikaji kinachodaiwa na wananchi kwa viongozi wao kkiko juu sana.
Pia wakati huo ilidsiwa kwamba Mwanza kulikuwa na mitambo ya kuanzia kazi ya uzalishaji wa umeme na tatu lengo ilikuwa kuwa na.uwezo.wa kuuza umeme wetu kwa nchi zinzopakana na ziwa hili ikiwemo Rwanda na Burundi.
Msisitizo.wa hoja yangu hapa.ni kwamba huenda kulikuwaa.na msukumo kutoka njekwa hiyo uwezo.wetu wa kufikiri na kuamua ukafungwa kapuni na kusubiri mwenye kutoa ndio afanye na maamuzi.ninj kifanyike.
Nafikiri mwafaka utapatikana kwa kuangaalia upya mpango wetu kwa.sasa una manufaa gani kuendelea kuleta Gas DSM au kujenga mtambo wa umeme hapo Mtwara na kufikiria kuiiuzia hata Msumbiji.
Mwishho wa yote lazima tubakie kama nchi moja Tony ambapo.watoto..wetu.na wajukuu watapata nafasi ya kuishi kwa.amani na ffuraha na kufaidi mali za nchi yao kwa umoja na mshikamano kama Tanzania.
Sent from Yahoo! Mail on Android
From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>;
To: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>;
Subject: Re: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam
Sent: Sat, Jan 26, 2013 2:00:27 PM
Ezekiel,

Upo sahihi kabisa, lakini kupuuzia kuko kwingi maana ushauri wa kujenga generation Mtwara ulitolewa siku nyingi pia. Wakashauriwa kuwa generation ya umeme mtwara utafaidisha liganga na baada ya generation ya Mchuchuma (from coal) ungeongeza density ya power kwenye grid. Hawajasikia, na aliyeanza kubadili mambo ni Mramba alipokuwa viwanda. Akina Ngereja nao hawakujiongeza na kubadili maamuzi ya awali kulingana na hali ya sasa.

Mkusanyiko wa makosa ya maamuzi ya kisaidiwa na makosa ya kutojituma yametufikisha hapa leo! Kwa hili siwezi kusamehe, maana hata maamuzi ya kujenga 100mW huko mwanza yalipingwa kwani supply ya heavy oil italeta madhara ya barabara na uzalishaji wa umeme wa aghali sana kutokana na overhead cost nyingi. Walishauriwa waimarishe uzalishaji umeme Songosongo na Mchuchuma na pia njia ya kusafirisha umeme kupitia Tabora, Shy, Mwz na Mara.

Sikio la kufa halisikii dawa!
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
From: ezekiel kunyaranyara <ekunyaranyara@yahoo.co.uk>
Date: Sat, 26 Jan 2013 13:21:02 +0000 (GMT)
To: tony_uk45@yahoo.co.uk<tony_uk45@yahoo.co.uk>
Subject: Re: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam
Eng Haamisi hata mimi nakubaliana.na nadharia ya.mwalimu wako.lakini.niende mbali zaidi kwa kusema.kuwa hata ukienda huko ulya bado elimu watakayokupa ni ile itakayokufanya ufanye maamuzzi kma wwnavyotaka wao..
Hoja nyingine ni kwamba uamuzzi wa kupeleka Gas DSM ulifanyika.siku nyingi kidogo huko nyuma. Economics dynamics zina nadharia inayosema the best solution today it might be the worst solution or decision today.
Kwa.mtizamo wangu hili ndilo linaloweza kuwa limetokea. Waliokuwepo lazima.wasiamame na kueleza msingi wa uamuzi wao wa wakati huo. Tatizo li akuja pale hata wanaoelezwa hawataki kusikilizaa bali kuleta vurugu tu. Ni vigumu kusikiliza hata uwepo wa mawazo mapya iwapo hata unayemsikiliza yeye hana muda wa kukusikilizaa ili aone ni nini ulichtazamia kufanya.
Ccost benefit analysis inayofanyika sasa haiwezi kutoa majibu mazuri ya kufavor hali ya wakati huo. Kumbukeni wakati huo hatukujua mambo mengi kuhusu Gas na mafuta.
Mimi.nashauri kwamba wananchi hebu nao wakubali kuusikiliza upande wa pili, vinginevyo tunakokwenda.siyo kwenyewe. Itafikia kila mtu adai vitu vinavyopatikana kwao virudi kwao. Ikifika hapo hatutakuwa na Tanzania bali kitu kingine tu.
Sent from Yahoo! Mail on Android
From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>;
To: <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam
Sent: Sat, Jan 26, 2013 12:12:54 PM
Abdallah,

Mimi nakubaliana na huyo mwalimu wako. Hapa tumejaza watu waliosoma mechanically tu, hawana uwezo wa kuchanganya uelewa wa kiuchumi na uhandisi katika misingi ya kibiashara.

Niliposikia maandamano ya kwanza Mtwara mimi nilihoji kama maamuzi ya kutumia dolla billion 2 kuwepa bomba la gesi Dar kama ulikuwa uamuzi jadidi; sikupata jibu na watu wakakimbilia kujibu kisiasa zaidi ya kiuchumi na kibiashara. Kwa fedha hizo tungweza kujenga mtambo wa gesi wa kutoa megawati 1200 huko huko na kuweza kujenga transmission line ya Km 1000 kupeleka umeme kwenye gridi na kuongeza uwezo wa gridi kuwa Kv 660 ili iweze kuhimili umeme huo.

Wahandisi wa umeme tu na nyenzo (power/energy) yaonekana ndio waliotoa wazo la kusafirisha gesi na kusahau kuangalia options nyingine kwavile utaalamu wa kibiashara na uchumi sio major ya wizara hiyo na nina shaka kama wizara za uchumi na biashara kama zilihusishwa.

Gesi inayoletwa kwa sasa kutoka Songosongo, inatosha kukidhi matumizi ya viwanda vya saruji, na vinginevyo na pia vinu vya umeme vilivyo hapa Dar ambavyo vingebaki kama standby kwa grid balancing purpose.

Tunaleta gesi, na bado tutabidi kujenga vinu tena kutumia hiyo gesi efficiently! Operating cost ya kutunza mitambo ya kusukuma gesi toka Mtwara na gharama za kuendesha mitambo ya umeme hapa Dar ni karibu ya mara 1.4 ikilinganishwa na shughuli hiyo kufanyika Mtwara. Ukikokotoa gharama hizi na kutengeneza cost/benefit analysis ya mradi kuleta gesi Dar utaona ujinga mkubwa uliofanyika.

Ukiacha hilo la CBA, social benefits nazo ni kubwa kwa watu wa kusini kwa nyanja mfano:
Viwanda vya kutengeneza plastics (granules) vingewekwa Mtwara, navyo gharama ya kuviendesha ingekuwa chini ikilinganishwa na Dar. Ujenzi wa makazi ya wafanyakazi wa viwanda ungefanyika mtwara na kunufaisha wananchi wa huko. Pia ajira nyingi ukiacha ya high class cadre nayo ingenufaisha wakaazi wa mtwara.

Inakisiwa kuwa maamuzi ya kuchukua gesi mtwara na kuileta Dar itaingizia taifa hasara kwenye nyanja ya viwanda na kutokidhi ushindani wa kimataifa kwa bidhaa zitakazozalishwa Dar badala ya Mtwara!

Abdallah, point ya mkufunzi wako ni halisi na ujinga wetu leo utatugombanisha na pia gharama kubwa ya kulilinda bomba itakuwa kubwa kwa maamuzi ya kipumbavu kabisa. Eti tuna watalaam, mie wanatuingiza mkenge kwa fikra njiwa zinazolitia taifa hasara. Kheri ya Nyerere aliyetuona hatuna utalaam akazuia uchimbaji wa raslimali zake hadi taifa likue.


------Original Message------
From: Abdalah Hamis
Sender: wanabidii@googlegroups.com
To: Wanabidii
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Incompetence Responsible for Faulty Decision to Transport Mtwara Natural Gas for Power Generation in Dar es Salaam
Sent: Jan 26, 2013 14:37

Dr A. Massawe/massaweantipas@hotmail.com/

I remember my Head of Department at the foreign university I did my
engineering studies saying that from his teaching experiences in
helping engineering curriculum developments abroad, found out that the
education taught in most African institutions is only meant to create
doers rather than both business makers and doers.

And it is very true, very little of the engineering or business design
science is taught nowadays in our local institutions of higher
learning and almost all the local experts are equipped with in
business or engineering design is the know how to use western
developed computer designing programs in feeding in the inputs and
retrieving the outputs mechanically-like robots.

As a consequence, in the absence of western made computer program (s),
our local experts completely fail to advice our decision makers
properly on easily understood business/engineering design problems
such as the one involving choice of option for the location of Mtwara
Natural Gas based power generation plants from the two options given:
Dar es Salaam or Mtwara.

I consider the disputed Government choice to build a pipeline for
transporting the natural gas from Mtwara for Power generation in Dar
es Salaam a faulty one because:

Dar es Salaam and its nearby surroundings could be having a lot more
of its own natural gas than Mtwara has (1);

Producing power in Mtwara and building up a new power grid to
distribute in Mtwara, Lindi, Pwani and Dar es Salaam regions would
have empowered all coastal rural and urban centers from Mtwara to Dar
es Salaam with a reliable supply of power which is connectable or
easily connectable to the national grid to enhance its reliability and
its stimulation of investing for economic growth within the whole
urban and rural coastal corridor from Mtwara to Dar es Salaam (2);

Our priority industrial development focus now should have been Mtwara
which neighbours the very rich developing Mozambique and nearer to
landlocked countries like Malawi, Zimbabwe and Zambia than Dar is to
these countries, especially aimed to grasp a significant share of the
market for manufactured goods consumption in Mozambique and in the
other nearby landlocked countries of Malawi, Zimbabwe and Zambia. If
we don't do it this way, Mozambique will and become the main supplier
of manufactured goods in our southern regions and in the other nearby
landlocked countries mentioned here (3).

Similarly, relative to Dar es Salaam, the Tanzanian towns of Tanga,
Arusha and Moshi should have also been given priority industrial
development focus aimed to conquer markets in the neighbouring Kenya
and to reverse the trend in which it is Nairobi and Mombasa exporting
almost all East African manufactured goods consumed in Tanzania,
especially in the Northern part of our country.

Was very surprised to hear a Honourable decision maker publicly
arguing that the choice to use the Mtwara natural gas for power
generation in Dar es Salaam instead of Mtwara was correct because this
power generation won't have much to offer in the form of jobs to the
people of Mtwara because it doesn't employ many, not knowing that most
important of what Mtwara would have benefited from having the power
generated in Mtwara was the reliable availability of cheap power which
stimulates investing for economic growth in our southern regions.
Again the same Honourable decision maker argued that decision was
correct because natural gas transportation via pipeline is cheaper
than power transmission via grid (yes, the cost of power
transportation via grid is almost twice the cost of natural gas
transportation via pipeline), not knowing that main determinant of
option choice in this case and in
any other similar business are the total profit returns from the two
project options during their whole life spans. The same Honourable
decision maker concluded public argument by saying that the choice of
Dar es Salaam was correct because choice of Mtwara would have resulted
into
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


0 comments:

Post a Comment