Sunday 27 January 2013

Re: [wanabidii] Huu ni unafiki ama...?

Katika historia ya nchi yetu au nchi za wenzetu utakuta semi na mambo
mengi yaliyohifadhiwa na yanaendelea kuwa na maana hadi leo hii.
Wananchi na wasomi duniani kote wanaendelea kuyanukuu kwa mfano mwl.
JK Nyerere aliwahi kusema kumsomesha mtanzania elimu ya juu halafu
akakimbilia nje ni sawa na wanakijiji wenye njaa kutoa akiba yao ya
chakula na kumpa mtu aende kijiji kingine kuwatafutia chakula halafu
apotelee huko bila kurudi. Alimuita mtu huyo kuwa ni mtu mbaya sana
(betrayer). Rais Kenedy wa Marekani akiwahutubia wamarekani alisema "
my fellow Americans, ask not what your country can do for you, ask
what you can do for your country na mifano mingine mingi toka viongozi
mbalimbali duniani.

Kwa viongozi tulio nao katika nchi yetu nashindwa kuona kama yupo
anayeweza kutuachia msemo au maneno ya busara yatakayodumu vizazi ata
viwili. Hii ina maana tuna ombwe la uongozi, kwamba wengi wanaoingia
kwenye uongozi hawana vipaji vya uongozi bali ni wajasiliamali.
Kwa upande mwingine kama mtu anataka kutoa mfano wa viongozi waliowahi
kutoa semi za ajabu na za kuwahudhi wananchi unaweza kuzipata Tanzania
kwa wingi mfano Mh. Basil Mramba alisema kama nyasi watu watakula
lakini ndege ya rais lazima inunuliwe. Mh. John Pombe Magufuli alisema
kama wananchi wa Kigamboni hawataki kulipa nauli ya Sh.200/= basi
wapige mbizi. Mh. mwingine alipoulizwa kwa nini Tanzania ina
rasilimali nyingi na ni maskini akasema ata yeye anashangaa kwa nini
hali iko hivyo na wengine wengi siwezi kuwataja nikawamaliza.

Hatumshangai waziri na wenzake waliosema kwamba Katiba yetu inakidhi
haja na hivyo hakuna haja ya kubadilisha. Lakini viongozi hao hao leo
wakiulizwa wanatoa mapendekezo lukuki. Viongozi hawa hawana msimamo
wala mwelekeo, shida yao ni kupata mlo wa siku hiyo kwa kusema
chochote wanachofikiri kitamfurahisha boss wao. Hawajitegemei katika
kuwaza, kuna kundi au watu wanaowaza kwa niaba yao. Wanaishi kama
roboti, wanacholishwa ndo wanachokitema bila ata ya kukimungunywa.

Hivi ukijiuliza swali ni kweli maneno hayo walikuwa wanayachambua kwa
akili zao au ndo hivyo zilikuwa ni redio kaseti zikibonyezwa zinalia
mziki uliorekodiwa? Katiba ni ile ile leo mawazo mapya wanayatoa wapi
kama miaka miwili iliyopita hawakuwa nayo? Binafsi naona ata hilo jina
la wanafiki halitoshi labda tuwatafutie jina lingine. Na ata
wakimaliza muda wao wa uongozi hakuna kubwa lolote la kujifunza kutoka
kwao.

2013/1/27 abel makubi <makubi55@gmail.com>:
> Hawa ndo viongozi wetu. Jibu ni unafiki tu
>
>
> 2013/1/27 Mgaywa GMD Magafu <gmdmagafu@gmail.com>
>>
>> Wanabidii,
>>
>> Kuna kitu kimekuwa kikinisumbua moyoni. Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi
>> kuhusu viongozi wetu (waliopo madarakani na wastaafu) na Katika mpya. Kabla
>> Rais hajakubali kuundwa kwa Katiba mpya kila aliyekuwa anaulizwa (ukitoa
>> upande wa vyama vya upinzani) alikuwa anajibu: "Katiba iliyopo inakidhi
>> mahitaji ya sasa - hakuna haja ya katiba mpya". Leo wanapoonana na Tume ya
>> Waryoba ya Katiba, wale wale waliosema Katiba ya sasa inakidhi mahitaji ya
>> sasa, wanatoa mawazo mengi sana mapya yenye kuikosoa Katiba yetu ya sasa.
>> Je, huu si unafiki? Kama si unafiki ni nini? Ama ndio kwenda na wakati?
>>
>> Magafu
>>
>> NB: Nasubiri hususani maoni ya Mh Kombani (kama bado hayajayatoa). Bila
>> shaka ataendelea kusema: "inakidhi mahitjai ya sasa - hakuna haja ya katiba
>> mpya".
>>
>> --
>> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
>> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
>> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment