Monday 3 December 2012

[wanabidii] UTABIRI WANGU UMETIMIA - TANZANIA OYEEE!

 
Wanamichezo Watanzania,
 
Juzi niliweka dodoso kwamba TANZANIA BARA itaingia nusu fainali kwa kuitoa Rwanda.
Kweli imefanya hivyo kwa ushindi wa mabao 2-0.
 
Nilitabiri pia kuwa TANZANIA ZANZIBAR nayo itaitoa Burundi.
Kweli imefanya hivyo kwa kuichapa kwa penalti 6-5.
 
Utabiri wangu bado unaendelea kwamba timu hizi za Tanzania zitacheza zenyewe kwenye fainali siku ya Jumamosi baada ya mambo yafuatayo kutokea:
 
TANZANIA BARA itacheza na mshindi kati ya Kenya na Malawi na itamfunga bila huruma kupitia kwa John Boko.
 
TANZANIA ZANZIBAR itacheza na mshindi kati ya wenyeji Uganda na Ethiopia na itashinda kwa penalti tena.
 
Washabiki wa Yanga tunaomba muwaambie wachezaji wenu waongeze juhudi kwenye timu zetu; ndiyo pekee wanaolegea viwanjani.
 
Tunaomba TFF nao wafanye hima ili Mbwana Samatta aje dimbani; waache kuwadekeza wapuuzi wa Kongo.
 
 
Matinyi.

0 comments:

Post a Comment