Saturday 29 December 2012

[wanabidii] VYAKULA VYA GMO MADUKANI KWETU

Ndugu zangu


Nilikuwa natafuta vyakula Fulani Fulani vya watoto na moja ya kitu nilichokuwa naangalia kwenye kila bidhaa ni kama vyakula hivyo vina nembo zenye kuonyesha kama ni GMO au la , Nilipata bidhaa kama 3 hivi zilizokuwa na chapa inayosema NON GMO kwa zile bidhaa zinazotoka nje ya nchi haswa Ulaya Na Marekani .


Bidhaa hizi nimezikuta katika duka la shoprite mlimani city ,hii imekuwa ishara nzuri maana tumejadili mara kadhaa kuhusu bidhaa kuwekwa nembo kama ni GMO au la hii nimeiona kwa mara ya kwanza hapo Shoprite .


Hili sio Tangazo la biashara ila ni kuleta mjadala huu mpana zaidi kuhusu bidhaa zinazotokana na GMO haswa vyakula ambavyo inasemekana vipo nchini na watu wanatumia na tumekuwa tukisikia au kusoma kuhusu madhara ya bidhaa hizi sehemu mbalimbali duniani .


Kama una ushuhuda wowote kuhusu GMO kwa kanda ya afrika mashariki au popote ulipo tunaweza kutupa kutumia mtiririko wa mjadala huu au tuma kwenda wanabidii@googlegroups.com kama wewe sio mwanachama wa Wanabidii na wengine wataweza kusoma mchango wako .


Karibu tuendelee kujadiliana huku tukijenga nchi zetu .


Unaweza kusoma au kujifunza zaidi kuhusu GMO kwa kutembelea 


http://www.raiamwema.co.tz/chembe-hai-za-ng%E2%80%99ombe-nge-zachanganywa-kutengeneza-ng%E2%80%99ombe-mpya


http://en.wikipedia.org/wiki/Genetically_modified_organism


http://www.whfoods.com/genpage.php?tname=george&dbid=207



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment