Saturday 29 December 2012

Re: [wanabidii] FreeMan Mbowe : Dr Slaa Mgombea Urais CHADEMA 2015


Hebu oneni alichokiongea Mbowe Karatu kilivyogeuzwa makusudi na watu


Mbowe: Sigombei urais

•  Asema atasimamia kupata mgombea bora kuingia Ikulu 2015
na Mwandishi wetu

 


HATIMAYE Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amevunja ukimya na kuweka bayana kuwa hatagombea urais katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Kwa kauli hiyo, Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upunzani Bungeni, amefuta rasmi minong'ono ya muda mrefu kwamba anakusudia kuwania tena urais baada ya kufanya hivyo mwaka 2005.

Akizungumza na wananchi wa Karatu kwenye Uwanja wa mpira wa Karatu baada ya kumaliza kikao chake na viongozi wa Karatu, Mbowe alisema kwa sasa amejielekeza kupanga na kutekeleza mikakati kuhakikisha CHADEMA inaingia Ikulu mwaka 2015 na kuhakikisha anasimamia kupata viongozi bora wa kupeperusha bendera ya chama hicho kikuu cha upinzani.

Mbali na kusimamia upatikanaji wa mgombea bora wa urais, Mbowe alisema pia kazi yake kubwa itakuwa kuhakikisha anasimamia upatikanaji wa wagombea bora wa nafasi zote za uongozi kuanzia ngazi ya serikali za vijiji, vitongoji, madiwani, wabunge na urais.

"Kuna taarifa za upotoshaji zinaenezwa kuwa mimi na Dk. Slaa tuna ugomvi wa kuwania urais. Jambo hili sio kweli hata kidogo, mimi sitawania urais mwaka 2015 na Dk. Slaa nafanya naye kazi kwa kuheshimiana na maelewano ya hali ya juu kwani tumekuwa wote kwa muda mrefu sasa," alisema Mbowe.

Alitamba kuwa CHADEMA itaingia Ikulu mwaka 2015 na itachukua majimbo mengi ya uchaguzi na kutolea mfano wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwamba kati ya majimbo 22 yaliyopo, chama hicho kina uhakika wa kushinda 15.

Kuhusu mgogoro wa Karatu uliokipasua chama hicho katika makundi, Mbowe alisema umemalizika baada ya kikao chake na viongozi hao kwa siku mbili.

Katika kuonesha kwamba viongozi hao wamemaliza tofauti zao, Mbowe aliwapandisha jukwaani viongozi wote na kushikana mikono kama ishara ya kutakiana amani.

Mwaka 2000, Mbowe alikuwa Mbunge wa Hai, lakini ilipofika mwaka 2005, chama kilimwomba kuwania urais, hivyo aliacha kuwania ubunge licha ya wananchi wa Hai kumtaka asiache.

Hata hivyo alishindwa na Rais Jakaya Kikwete. Ilipofika mwaka 2010, Mbowe aliwania ubunge wakati Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa akijitosa kuwania urais, akichuana na Rais Kikwete.

Dk. Slaa alitoa upinzani mkali kwa Rais Kikwete na kusababisha aibuke na ushindi mdogo wa asilimia 60.

Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka 2010, Mbowe amekuwa akitajwa na duru za siasa nje na ndani ya CHADEMA kwamba anakusudia kuwania tena urais mwaka 2015.

Mbowe amekuwa akitajwa sambamba na Dk. Slaa na Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe kwamba wanasuguana kutaka urais kupitia CHADEMA.

Wapo waliokwenda mbali wakihusisha migogoro ya chini kwa chini inayoendelea ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani, kwamba inatokana na makundi ya vigogo hao watatu kuutaka urais kwa udi na uvumba.

Hata hivyo, Zitto pekee ndiye ambaye tayari ameshaelezea nia yake ya kutaka kuwania urais kama chama chake kitampa ridhaa, na amekuwa balozi mzuri wa kupigia debe katiba ibadilishwe ili umri wa kuwania urais upungue kutoka miaka 45 ya sasa hadi 30.



Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

From: Bmkinga <bmkinga@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 30 Dec 2012 08:20:05 +0300
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] FreeMan Mbowe : Dr Slaa Mgombea Urais CHADEMA 2015

Siyo Lipumba tu hata JK aligombea mara ya kwanza akadondoshwa na Mkapa, mara ya pili ndipo aliposhinda.

CHADEMA kama mahasimu wakuu wa CCM hawawezi wakashauriwa na CCM na bado likawa ni jambo jema. Kama CCMA hawataki mtu fulani katika CHADEMA agombee ujue huyo wasiyemtaka ndiye anayefaa. Kama CHADEMA wakateua mgombea, kisha wakasifiwa na CCM kuwa wamefanya uteuzi mzuri, ni lazima CHADEMA warudi na kutafakari mpya maana ni lazima uteuzi huo utakuwa wa kuinufaisha CCM.

Kama CCM haitaki kabisa Dr Slaa agombee, basi huyo ndiye atakayetakiwa kusimamishwa na CHADEMA kugombea. Kama ni uteuzi mbaya kwa nini watu wa CCM kama akina YONA na akina KIGWANGALA iwaumize sana? Si ingekuwa faraja kwao maana chama chao CCM kitapita kiurahisi?

Bart


Sent from Samsung Mobile



gm26may@gmail.com wrote:



Dr Slaa amegombea mara moja tu mnadai anatakiwa apumzike

Vipi kuhusu Pr Lipumba aliyegombea mara zote tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza mnamshaurije?


Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

-----Original Message-----
From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sat, 29 Dec 2012 16:16:54
To: Wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] FreeMan Mbowe : Dr Slaa Mgombea Urais CHADEMA 2015

Katika Mkutano Mmoja huko Karatu mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe
amemtangaza Dr W P Slaa kama mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA mwaka
2015 .

Mimi Binafsi nashangaa ni Utaratibu gani umetumika kumpitisha Dr Slaa
kama mgombea urais wa CHADEMA , Najua huwa kuna vikao na michanganuo
kadhaa wa kadhaa kwa hapa sijui imekuwaje .

Ndugu Tumaini Makene tunaomba utujuze au Mhe Mbowe alikuwa Anapima
upepo tu ?

Kwa maoni yangu ningependa kumwona Dr Slaa akupumzika amwachie nafasi
hiyo mwingine yeye mpaka sasa ameifanyia chadema na taifa hili mengi
akiwa mshauri itakuwa hatua nzuri zaidi asiwe kinganganizi kama
akikubalia basi apishe utaratibu wa kidemokrasia ufanyike ili kumpata
mgombea .

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


0 comments:

Post a Comment