Saturday 29 December 2012

[wanabidii] Re: FreeMan Mbowe : Dr Slaa Mgombea Urais CHADEMA 2015

Hivi Mbowe kama mwanachama wa Chadema akipendelea kumuona Dkt Slaa kama mgombea anayefaa kupepea bendera ya chama hicho hapo 2015 ndio inamaanisha AMEMPITISHA KUWA MGOMBEA?

Ni vema kutumia busara ya kuielewa habari kabla ya kuhitimisha mambo jumla jumla.

Halafu, Dkt Slaa kama mwana-Chadema ana kila haki ya kugombea urais kama ilivyo kwa Zitto Kabwe aliyekwisha tangaza nia yake ya kuutaka urais 2015. Pengine busara kidogo tu zingeweza kukufahamisha kuwa mafanikio waliyopata Chadema katika uchaguzi uliopita ambapo Dkt Slaa alikuwa mgembea yanaweza kuongezeka pindi akipitishwa kugombea tena mwaka 2015.

By the way, kama kuna wanasiasa wanaopaswa kupumzika kugombea ni Maalim Seif na mwenzie Lipumba ambao wameshagombea mara kadhaa na kuambulia patupu.

Neglecting your opinion, nadhani Chadema wanatambua fika kuwa mwanasiasa pekee anayeweza kuwaingiza Ikulu ni Dkt Slaa. Pamoja na hujuma mbalimbali zinazofanywa dhidi yake ameendelea kuwa mwana-Chadema maarufu kuliko wote,arguably, na kwa kila anayefuatilia vema siasa za Tanzania ataafikiana nami kuwa ndio tegemeo pekee kwa chama hicho kuingia Ikulu come 2015
On Sunday, 30 December 2012 00:16:54 UTC, Yona F Maro wrote:
Katika Mkutano Mmoja huko Karatu mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe
amemtangaza Dr W P Slaa kama mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA mwaka
2015 .

Mimi Binafsi nashangaa ni Utaratibu gani umetumika kumpitisha Dr Slaa
kama mgombea urais wa CHADEMA , Najua huwa kuna vikao na michanganuo
kadhaa wa kadhaa kwa hapa sijui imekuwaje .

Ndugu Tumaini Makene tunaomba utujuze au Mhe Mbowe alikuwa Anapima
upepo tu ?

Kwa maoni yangu ningependa kumwona Dr Slaa akupumzika amwachie nafasi
hiyo mwingine yeye mpaka sasa ameifanyia chadema na taifa hili mengi
akiwa mshauri itakuwa hatua nzuri zaidi asiwe kinganganizi kama
akikubalia basi apishe utaratibu wa kidemokrasia ufanyike ili kumpata
mgombea .

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment