Monday 31 December 2012

RE: [wanabidii] Heri ya mwaka mpya 2013.

Asante Magesa.
 
Mwaka huu uwe wa Watanzania kuacha kulalamika na kuanza kutenda.
 
Watanzania tunalalamikia kila kitu, siku hizi eti mpaka watu wanalalamikia ujenzi wa barabara kwamba hazina maana kwa watu maskini wakati enzi zile tulipokuwa hatuna barabara kila mtu alilalamika kwamba nchi hii huwezi kusafiri wala kusafirisha kitu. Ni kulalamika tu, asubuhi, mchana, jioni hadi usiku. Zanzibar hata mtu akikimbiwa na mkewe analalamikia Muungano, huku Bara hata mtu akifumaniwa na kianafunzi analalamikia mafisadi. Ni kulalamika tuuuuuuuu!
 
Sasa tufanye kazi kwa juhudi na maarifa na tuwe wabunifu; wenzetu wanakimbia, sisi bado tunabishania hata kuruka kichurachura tu. Inabidi tufanye zaiid ya kukimbia; turuke kwenye nyungo sasa, na wasioweza wapande fisi kama farasi na wengine watumie mamba majini kama ngarawa.
 
Tunaachwa na dunia, ebooh!
 
Matinyi.
 
> From: magesa@hotmail.com
> To: wanataaluma@googlegroups.com; wanabidii@googlegroups.com
> CC: mabadilikotanzania@googlegroups.com
> Date: Tue, 1 Jan 2013 00:31:21 +0000
> Subject: [wanabidii] Heri ya mwaka mpya 2013.
>
> Nawatakia wote heri ya mwaka mpya 2013.
>
> Tubadilike sasa ili tuweze kutimiza wajibu wetu vizuri.
>
> Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
>
> Magesa,P.
>
>
> Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> DELL LATITUDE D 620 & D30
>
> 80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
> DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
>
> TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
>
> CALL : 0786 806028
> Free Delivery in Dar es salaam
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

0 comments:

Post a Comment