Saturday 29 December 2012

[wanabidii] Fw: [Mabadiliko] Wamakonde wakitaka gesi yao na wao warudishe pesa za Katani na Kahawa - Prof Muhongo



Wanamabadiliko,
Nafikiri Waziri ametoa hoja nyepesi kutaka kuzima hoja ya watu wa Mtwara.

Waziri akumbuke kua tatizo la watu kutofaidika na raslimari zinazopatikana katika maeneo yao nikubwa sana Tanzania. Hebu jamani fikiria kwa Tanzania haki ya mtu kutumia ardhi inaishia kwenye surface soil (crop cultivation only). Hii inakuja kweli?? Nafikiri kunahaja yakua na tafsiri pana ya haki zinazo ambatana na ardhi ambayo mtu amekua akitumia kwa miaka mingi. Ikiwezekana to borrow definition ya James kua 'Land include much more than just physical soil or substance. It include for instance, building, and any other thing attached permanent to the soil or permanently fastened to anything which is attached to the soil (James 1971)

Kwa Tanzania nitofauti, vitu vyote vilivyochini ya ardhi ni mali ya serikali na mtu aliekua akitumia hiyo ardhi hana haki navyo. Kwahiyo vito vya thamani vikigundulika chini ya ardhi yake mtuhuyo anaondoshwa nakua-compensated kidogo tu na kubadili hao wanaoitwa 'WAWEKEZAJI' badala ya 'WAPORAJI' . Rasilimali hizi zingetumika vema ingekua rahisi sana kwa serikali kujustify, tatizo hilo halijawezekana kwa Tanzania.

Mahali pengine watu wameondoshwa kwanguvu na kuuwawa hovyo, kumbukeni ya Bulyankulu. Chaajabu hao wawekezaji wanaondoka nautajiri mkubwa na watu wa maeneo hayo kubakia masikini 'ndugu zangu tujaribu kuwa fare hata kidogo hivi wewe unaona nihalali wageni watajirikie kwenye ardhi uliokua ukilima, kukusanya kuni, kuchungia mifugo yako huku wewe ukibakia masikini?? Hiyo haikubaliki hata kidogo.

Mahala pengine watu wanaishia kupigwa tena kwa risasi, kuitwa wavamizi kwenye ardhi yao wenyewe, na mbaya zaidi rasilimali zao mhimu kama maji zikiharibiwa na heavy metals nk. Huo ujinga mpaka lini? Niwakati wa Serikali kuangalia kwa upya hizi sera za uwekezaji ambazo kwa sehemu kubwa hazizingatii utu wa mzawa. Hii haiwezi kukubalika.

Utajiri wa vito uliogundulika mahala pengine ungetumika vema TZ, watu wa mtwara wangekua na shule nzuri, hospital nzuri, human resource yakutosha, barabara, maji safi nk. Waziri angeibuka nahoja kua hayayote mnayoyaona Mtwara hayajatokana na Koroshwa tu bali pia na samaki wa Mwanza, Tumbaku ya Tabora, Almasi za Mwadui, Tanzanite ya Merarani, Utalii wa Serengeti nk. ingekua na maana sana. Nahakuna ambae angekua na chembe ya shaka juu ya hoja ya Waziri. But poverty in Southern regions and Tanzania in genral are widespread. Haya mambo mpaka lini jamani??? Nafikiri tuungane na watu wa mtwara kubadilisha sera. Issue ya UZAWA nibora sana ikitumika vema.
Alexander




From: Lemburis Kivuyo <lembu.kivuyo@gmail.com>
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Sent: Saturday, December 29, 2012 2:35 PM
Subject: [Mabadiliko] Wamakonde wakitaka gesi yao na wao warudishe pesa za Katani na Kahawa - Prof Muhongo

Nimeikuta hii katika gazeti la Mwanachi 29 Desemba  2012 nikaona itasaidia kujadili kwa kina zaidi kuhusu madai ya WanaMtwara kudai Gesi yao

Profesa Muhongo alidai kuwa kuna wakati nchi ilitegemea sana Katani katika kuendesha nchi, hivyo Mtwara nayo ilifaidika na mapato hayo ya katani. Kuna kipindi pia nchi iliendeshwa kwa Kahawa, na Mtwara nayo ilifaidika kwa mapato ya Kahawa. Sasa gesi imegundulika kwao wanataka wafaidi wenyewe. Alidai warudishe hizo pesa kwanza za Katani na Kahawa. Hata hivyo alidai kuwa mkuu wa kaya atatolea ufafanuzi katika salamu zake za kufunga mwaka tarehe 31 Dec 2012


Real Change for Real Development,  

Lemburis Kivuyo
+255654650100/078 7665050/0755646470
Website: www.kivuyo.com,  Skype: lekivuyo, Facebook: http://facebook.com/lemburis.kivuyo, Titter: http://twitter.com/lembu1, Linkedin: http://tz.linkedin.com/in/lembukivuyo, Google+: gplus.to/lembukivuyo
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group, send email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
 
 




0 comments:

Post a Comment