Saturday 29 December 2012

Re: [wanabidii] DR.SLAA TAMBUA MWOSHA HUOSHWA

Mr. Muhingo,

Upo sahihi, leo mtu atajiita kina la kiislam, kesho kikristo sana lakini wanasahau lugha ile ile na tabia kimaandishi haibadiliki whether ni vifupisho, tabia na misemo ni ileile ya mtu.
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.

From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sat, 29 Dec 2012 07:36:02 -0800 (PST)
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] DR.SLAA TAMBUA MWOSHA HUOSHWA

Si kazi ngumu sana kujua kuwa humu jamvini kuna watu wachache wanatumia majina mengi.
Wala sijatoka nje ya mada. Nimeijadili kwa njia hii.

--- On Fri, 12/28/12, Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com> wrote:

From: Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
Subject: [wanabidii] DR.SLAA TAMBUA MWOSHA HUOSHWA
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, December 28, 2012, 9:14 AM

UMEWADANGANYA watanzania vya kutosha, umewapandikiza chuki na
kuwafitinisha vya kutosha, haujaweza kuwashauri kufanya kazi zaidi ya
maandamano, umewaburuza vya kutosha ndani ya chama na umewagawa vya
kutosha sasa wamejitambua waachie chama chao waendelee.

Kwa wafuatiliaji wa siasa za hapa Tanzania wengi hata huku kwetu
Nyikani, tunajua kuwa katibu wa Chadema Taifa Dr, Wilbroad Slaa
amewapa vyeo kwa upendeleo waliokuwa ''wanamlamba'' miguu yeye pamoja
na mchumba wake Josephine Mshumbushi.

Padri Dr, Slaa mbali na hayo amevunja katiba ya Chadem vya kutosha,
amevuruga chaguzi za ndani ya Chadema vya kutosha, wanachama wengine
wameondoka kundini ikiwa ni pamoja na kushindwa kuendelea kukisaidia
chama hicho kwasababu yake na wengine wamekonda miili na akili,
wengine wameumizwa na vyombo vya dola kutokana ushawishi wa kutotii
sheria bila shuruti.

Tunakumbuka pale mkoani Mbeya mtu huyu huyu yaani Padre Dr. Slaa
aliposababisha mnyukano mkali mpaka leo kwa viongozi wa Chadema baada
tu ya kumalizika ziara yake Januari 13,2012 baada ya Dr. Slaa kuwapora
demokrasia wanaChadema mkoa wa Mbeya kwa kumvua madaraka aliyekuwa
katibu wa chama hicho mkoani humo Mwanasheria Eddo Mwamalala na
kumpachika cheo cha ushauri wa mkoa.

Kwa akili zake alifanya makusudi kwa kujua wazi kuwa hakuna wa kuhoji
maana anatumia mbinu ile ile ya kuwagawa kisha kuwatawala vizuri huku
baadhi akiwaahidi neema kwenye chama hicho.

Baada ya kumuondoa Mwamalala katika nafasi ya ukatibu wa mkoa,
akampachika Boid Mwabulanga kushika nafasi hiyo ambayo masikini mtu
huyo hajawahi kuiota wala kuiomba kwa mujibu wa katiba ya Chadema
kisha akapigiwa simu kuwa anaikubali au anaikataa nafasi hiyo jambo
ambalo lilimshitua sana Mwabulambo ambaye hawezi kushawishi vijana
kuandamana pasipo kuangalia maslahi ya wananchi kwanza.

Kutokana na hali hiyo Mwabulanga anaendelea kuishikilia nafasi hiyo
kwa ushahidi tu maana haivi chungu kimoja na baadhi ya viongozi
wenzake ambao wamejazwa fikra za kuendesha chama hicho chenye mvuto
kwa walio kata tamaa kwa mtindo wa sinema za vurugu.

Hakuishia hapo, kwa kujua kuwa Mbeya hakuna anayekijua vema chama
hicho na chama hicho sawa na mali ya watu fulani alifanya mamuzi ya
kumpachika cheo cha Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Mbeya Peter
Mwamboneke kana kwamba anataka kumvalisha viatu vikubwa alivyoviacha
mwanasheria Sambwee Shitambala ambavyo mpaka sasa nafasi hiyo hakuna
aliyeweza kuimudu.

Wanachama ambao walijitokeza kuwania nafasi hiyo ni pamoja na John
Mwambigija ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Mbeya Mjini na
rafiki mkubwa wa familia ya Dr.Slaa, Zabron Nzunda (Sabodo),
Mwanasheria Philipo Mwakilima(Crimax) na Mwanasheria John Ngeka.

Wengine walikuwa ni Joseph Mwachembe(China), George Mtasha, Herode
Jivava, Hugho Kimario, Aminika Mwihomeke na mwanadada pekee Sorwa Gea.

Katika uchaguzi huo rafiki wa Dr, Slaa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya
Mjini Joseph Mbilinyi, John Mwambigija, alionekana kuzidiwa na dalili
zilionesha kuwa asingeweza kushinda bali nyota ilikuwa ikiwaka kwa
Zabron Nzunda aliyekuwa akiungwa mkono na Eddo Mwamalala.

Uchaguzi huo ulikuwa ukitarajia kufanyika Juni 20 mwaka huu lakini
ukavurugwa na kuvurugika mpaka leo hapo ndipo inajidhihilisha kuwa
uzuri wa paka si rangi yake bali ujuzi wa kukamata Panya.


Katika kikao kilichoketi Januari 11, mwaka huu katika ukumbi wa hotel
ya Mount Livingstone Jijini Mbeya chini ya Dr, Slaa, mfuasi wake w
karibu kwa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chedema wilaya ya
Mbeya Mjini John Mwambigija alimtuhumu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya
Chunya George Mtasha kuwa ni mla rushwa na hiyo yote inaelezwa kuwa
alipata nguvu kutoka kwa ''Stering'' wao.

Baada ya mbegu hiyo ya kutaka kuwatimua wote ambao wanaonekana kuwa
kikwazo kwa kundi la Dr. Slaa, kilifanyika Kikao cha kumvua uongozi
Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Chunya Februari 10, mwaka huu wilayani
Chunya na kuongozwa na Mwenyekiti masalia wa chama hicho Peter
Mwamboneke.

Baada ya kugonga mwamba wilayani Chunya, ukapangwa mkakati mwingine
mfu wa kwenda kumuondoa Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Mbeya
Vijijini Eliah Kabholile kutokana na maelewano hasi na Dr. Slaa lakini
pia mkakati huo ukashindikana baada ya mtandao huu wa www.kalulunga.blogspot.com
kufichua siri hiyo.

Siwezi kunyamaza bila kusema haya kwa ulimwengu maana najua mahala pa
kumshitaki Dr. Slaa hata ndani ya chama hakuna maana wengi amewaweka
na kulazimisha wawe wanalipwa mishahara hivyo hawawezi kumfanya lolote
wala kumhoji lakini kwa nguvu ya kalamu na wanyonge asiowapenda ndani
ya Chadema anapaswa kusema yatosha.

Tena ana bahati kubwa Zitto Kabwe ni mvumilivu laiti kama angeamua
naye kuweka mkono wake kwa wanachadema wanaomkataa Dr, Slaa hakika
angekonda sana, lakini amshukuru Mungu kwa hilo.

Dr. Slaa amemtumia mchumba wake mara kadhaa kwenda mikoani huku
akipokelewa kama kiongozi wa Chadema Taifa wakati hatujui hata nafasi
yake ndani ya chama, bila aibu anapokelewa na wafuasi wake kwa kutumia
pesa na magari ya kuomba kwa wanachama kana kwamba chama kinamtuma!.

Kuna wanachama masalia wa Chadema ambao wanaona Dr, Slaa kusemwa kwa
uovu wake na viongozi wenzake ni kama dhambi na inawauma kwelikweli!!

Jibu lake ni kwamba hakuna kitu kibaya kama dhambi ya uongo na fitina
kwa mtu mzima na mara kadhaa Mungu anaamua kuuangusha ''uongozi''
hasi.

Dr, Slaa analijua hili kwa kina, na kabla sijamalizia tayari yeye
amekumbuka kuwa kabla hajamkana Mungu alisoma vema kuwa chanzo cha
wajenzi wa Mnara wa Babeli kutofautiana lugha kilikuwa ni dhambi na
mawazo hasi.

Nasema Dr, Slaa mwosha huoshwa kwasababu wale ambao aliwatendea kwa
hila wameamua kumlipa kwa hila baada ya kujitambua na nimkumbushe Dr,
Slaa kuwa katika Biblia tunaambiwa kuwa Elisha akamwambia Geazi kuwa
walio nyuma yetu ni wengi kuliko unaowaona hivyo umefika wakati wa
kupima hoja zao badala ya kutegemea wanachama masalia ambao
wanamshinikiza kubaki katika nafasi hiyo ili aendelee kulinda maslahi
yao.

Mwandishi wa makala haya anapatikana kwa simu 0754 440749
kalulunga2006@yahoo.com

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment