Thursday 27 December 2012

Re: [wanabidii] Re: MTWARA WAFANYA MAANDAMANO YA KUPINGA GESI KUPELEKWA DAR

Ndugu Gabriel kwa sasa hilo haliwezekani ni vizuri viongozi wetu wakawaambie hawa wananchi ukweli , 

Kuna sababu kadhaa za kufanya hilo lishindikane kwa sasa .

Pamoja na hayo kuna fursa nyingine zinakuja na zipo kutokana na uvunaji wa gesi na mafuta maeneo hayo , hizi pia waambiwe wananchi na     jinsi wanavyoweza kushiriki na muhimu ni kupeleka watoto wao shule kusoma na kupata maarifa zaidi .

2012/12/27 Yachama Gabriel <yachama2012@gmail.com>
Hivi watu mnawaaminisha kuwa wana misitu yao? Kwani walipanda hata mti mmoja kama hawajaikuta tu na kuhamia huko wanajihalalisha. Mistu ni mali ya taifa kama walivyo wanyamapori wa selou na serengeti. Mtwara wanachotaka ni add-value hukohuko na baadae peleka mazao kuuza (umeme) kwa njia upendayo.
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Zantel Etisalat Tanzania.

From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
Date: Thu, 27 Dec 2012 16:11:05 +0000 (GMT)
Subject: Re: [wanabidii] Re: MTWARA WAFANYA MAANDAMANO YA KUPINGA GESI KUPELEKWA DAR

Ni kweli Gas ni tofauti lakini ni nishati kama maji. Jee, Mufindi, Pangani, Mtera wangeamua kubomoa mitambo/mfumo wa umeme, kukata milingoti umeme, transfoma umeme usifike DSM au maeneo mengine kwa vile unapita juu angani wao hawaupati si sawa tu na hao wa Mtwara?

Mitambo ya kuutawanya umeme wa Kihansi for example ipo bondeni wilaya ingine (Kilombero)-maji yanatoka wilaya ingine ambapo wanazuiwa kutumia misitu yao ili umeme upatikane.

Au mitambo ipo Ubungo ndio wire zigeuke zipelekwe kwa wengine unakotoka umeme-inapendeza? Hii ya Kihansi, ilileta shida kwa wananchi kuona wao wanatoa maji, yanapitishwa chini ya ardhi (Chura akaathirika kukosa mvuke asili) maji kuangukia mitambo huko bondeni (wilaya ingine-kilombero) ili kuweka nguvu ya kutoa umeme. Mtambo wa chini ardhini upo Kilombero ambako mafao ya barabara ya lami yamepelekwa huko. Sarakasi la mafao lilianza pia huko likatatuliwa nao kupata barabara ya lami hao watu wa Mapanda-Kibengu etc.

Lakini ujenzi mzima na pilika pilika zake kwao wao milimani na zahanati zao zilitumika, madawa kwisha mapema, athari za wageni kujaa na effect za HIV/AIDS maana  watafutao ajira hutoka mbali na kuzagaa vijijini kusiko makazi ya kutosha. Changu doa naye anahamia kutoka hata kenya, DSM na mikoa ya mbali kufuata wageni na wenyeji mafundi wa mitambo ya mradi huo. Vurugu, wizi mashambani na athari kibao. Haya yote yaja Mtwara wajiandae.

Gesiya Mtwara wanaweza wakatengeneza umeme ukaja Dar kama design ya mradi itakuwa hivyo. Ajira zitapatikana kama wenyeji watajituma na kufanya kazi kwa bidii na kwa uaminifu ama sivyo wageni toka mikoa mingine watajaa wao wakipenda umwinyi kazi ngumu hawataki.

Viwanda vya mtwara vikubwa na vidogo vikapata umeme bei nafuu. Ulaya (UK) gas inapita ktk bomba kama ifanyikavyo kwa maji inaingia moja kwa moja jikoni unapikia. Hapa kwetu unanunua kimtungi.

Kwa jinsi tulivyo wagumu kufundishika na kushika mawaidha ya usalama-gas ya kuja kwa bomba kama maji majumbani majumbani itatuua wengi mioto haitokwisha.

Kwa sasa Mtwara imejaa wageni wengi sana hao wa utafiti wa gas etc. Ndege zote hujaa sio kama zamani. Mabonde ya Kilimo Mtwara, Lindi, Rufiji ni potential kubwa kwa maendeleo. Bandari na visiwa vyake vya indian ocean kwa hotels na utalii mbali mbali kuunganisha na utalii wa Kilwa Kivinje, Kilwa Kisiwani kulikojaa Misikiti na makaburi ya Persians. Ikiunganishwa na Mafia na ZNZ (kama ZNZ watatutaka) ajira zitakuwepo. Ujenzi wa bandari na kilimo cha mazao mbali mbali. Ujenzi wa International Airport Mafia unaunganisha utalii wa Kilwa-hivyo Mtwara haipo mbali na uwanja wake unaboreshwa. 

Usishangae pamoja na resources zilizopo, mabonde mazuri ajabu, minazi iliyooteshwa na mwarabu kama mchicha au uyoga na maembe kibao, michungwa ile sweet  east african tall utaona kama tulivyoona wengine vya kushangaza saa moja ya asubuhii vijana wenye nguvu wanacheza pool table. Makumbi ya nazi yamejaa yanatoa materials za kutengeneza mazuria, vikapu, mapambo; minazi inatoa mbao nzuri za furniture za bei ghali; mtama unalimika na ufuta kichizi-tupo tupo barazani.

--- On Thu, 27/12/12, Yachama Gabriel <yachama2012@gmail.com> wrote:

From: Yachama Gabriel <yachama2012@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Re: MTWARA WAFANYA MAANDAMANO YA KUPINGA GESI KUPELEKWA DAR
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, 27 December, 2012, 13:40

Suala hapa naona ni kweli kwa kupeleka gesi Dar wao hawatapata kazi maana ufuaji umeme na mambo yyote yatafanyika Dar. Busara ingewatuma serikali wazalishie umeme hukohuko na viwanda vya plastiki navyo vijengwe huko ndio suluhisho la kuzalisha ajira Mtwara na kupunguza msongamano wa watu Dar. Umeme utakaozalishwa usafirishwe tu kwenda Dar, Dodoma, Iringa na Mbeya au Songea. Suala la mufindi kuzuia umeme kuletwa kwa watumiaji naona kidogo lipo tofauti na gesi.
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Zantel Etisalat Tanzania.

From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
Date: Thu, 27 Dec 2012 13:25:05 +0000 (GMT)
Subject: Re: [wanabidii] Re: MTWARA WAFANYA MAANDAMANO YA KUPINGA GESI KUPELEKWA DAR

Jee, wanavijiji wa Tarafa ya Mapanda Mufindi Mkoa wa Iringa nao wangekataa umeme wa Kihansi usifike Dar maana unatoka kwao wengine hawana hata na wamezuiwa kufanya shughuli zao katika catchment forest za huko ingekuwaje? Wakati huo huo walio wengi  wao hawana umeme au unapita juu angani katika kamba, lakini Chura wa Kihansi kapanda ndege kwenda USA na karudi baada ya miaka kadhaa analelewa kwa hela za mvuja jasho!!

Wale wa Mtera nao na wa Pangani River Basin wa mto Pangani kupeleka maji Hale Pangani 1 na Pangani 11 umeme unakuja Dar na miji mingine, wao kuvuaBwawa la maji la Pangani 11 utata. Wale wa Kidatu huko Kilombero vije? hata pantoni ya kuvuka mto tatizo lakini hawajaandamana kuzuia umeme wanaishi kwa mategemeo tutapata kesho pantoni keshokutwa!!. Mbunge wao kacharuka na tatizo hilo kila mtu kamshuhudia. Na wa Mtera huko Dodoma vipi? Jee na matatizo ya Bwawa la Nyumba ya Mungu kila siku msuguano kuhusu uvuvi kujipatia chakula visamaki vidogo utata kuvua na Ujenzi wa nyumba kando ya bwawa ili watu wavue jirani tata.

Kote huko umeme unasambazwa`miji mbali mbali ya Tanzania na wana mulikiwa Lindi na Mtwara kabla ya gas kugundulika. wangekosa umeme Ligula hospital ingekuwaje?

Zamani Mtwara ikitumia diseli na generator kutoa umeme. Hata nyama ikipelekwa kwa ndege kutoka DSM. Kwa sasa miradi mingi (FAO, CONCERN, Aga Khan, DADPs, Jane Goodal etc) imepeleka hela na kusaidia kilimo etc). jee, serikali iliwachukia si ikitoa mafao kwingine kupeleka huko? Na bandari inaboreshwa na barabara ya lami, madaraja hadi nchi jirani. Hela zote hizo zilizalishwa Mtwara-Lindi? Tuache ubinafsi.

Muhimu ni kuingia mikataba ya benefit sharing.  Vijiji kupitia kamati zao za mazingira, finance and planning waelekezwe upangaji mipango hiyo au kati ya ile ya O&OD ipi inaweza kuhisaniwa na hela zitokanazo na mauzo ya gas kuwafaidisha kwa ujumla na kwa mmoja mjoja wale needy-Yatima. Kuwa na ubinafsi hakufai. Mbona wamachinga wengi wamehamia DSM na kufaidika na biashara huko, umeme, maji ya mto Ruvu etc. Mbona huko Kilombero wananchi mabonde yao yamechukuliwa yanalimwa miwa na sukari inabwiwa nchi nzima wao wamekosa mabonde ya kulima ubwabwa waliozoea kula? wapo ktk mpambano na wafugaji ambapo mpunga wamegeuza majani ya kulishia mifugo? Kila mtanzania alipo popote pale anachangia maendeleo ya nchi hii kwa kuteseka.

Kwa sasa kusini (Lindi, Mtwara) kumejaa wapendao kuwekeza. Ardhi bwerere, mabonde mazuri lakini, kilimo cha mazao ya biashara kinahamasishwa na organizations mbali mbali (ufuta, mtama, mihogo dwarf, mbuzi na ng'ombe wa maziwa hybrid). Maembe na nazi kibao pia korosho. Sustainable farming na vikundi ya kusafirisha mazao to Dar-Msumbiji, Zimbabwe vitawakwamua badala ya kubweteka na kuona mtafaruku ndio solution.

Wachangamkie mipango na uwekezaji uliopo wafaidike. Diwani, Wabunge na viongozi wao, na watumishi wa sekta mbali mbali wahusike na bottom up planning na majadiliano na wawekezaji na mipango ya gas etc kuboresha na kufaidisha maisha ya waishio huko. wasije wakatoboa mabomba wakadhani wanaikomoa GVT-moto utawaka utawamaliza.
Dialogue na proper planning ya corporate responsibility and benefit sharing hiyo itasaidia sio vurugu na uharibifu.

--- On Thu, 27/12/12, Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:

From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
Subject: [wanabidii] Re: MTWARA WAFANYA MAANDAMANO YA KUPINGA GESI KUPELEKWA DAR
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, 27 December, 2012, 12:51

Wajadiliane maandamano hayasaidii kitu chochote , ingawa hili
tulishawahi kutabiri hata zile vurugu za mbagala hazikuwa dini ilikuwa
ni suala la gesi na mafuta .

On Dec 27, 3:46 pm, Ipyana Lwinga <ipyanalwi...@gmail.com> wrote:
> Maandamano yamefanyika leo Mtwara mjini kukataa Gas kupelekwa dar!
> Zaidi ingia kwenye link hii hapa chini'
>
> http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/374880-maandano-makubwa-mt...
>
> --
> Ipyana Lwinga
>
> Email:    ipyanalwi...@gmail.com
> Mob:     +255 757 065577
> Skype:   ipyana.plwinga
>
> "Mpende Jirani yako kama nafsi yako..."

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment