Wednesday 5 December 2012

RE: [wanabidii] NI ZAIDI YA UKATILI

Safi kabisa dada Hilda na Hongera sana kwa kuongezea picha zingine ili watu wote turaghbike zaidi, tujifikirishe, tafakuri tujipatie, tufanye utambuzi, tupime na tuchukue hatua. Ilikwisha andikwa katika historia kwamba yafanyikayo mafichoni ni lazima yaletwe peupe ili watu wapone. Watu lazima waelimeshwe kwa nguvu ili mabadiliko yaweze kupatikana. Ndiyo maana Mjerumani alitufundisha kwa viboko. Hawa watu wakeketao wanawake inatakiwa watembelee maeneo ya ‘Uganda beach’ ya nchini Uganda na ‘Kunyaza ‘ ya huko Rwanda ili waweze kujua madhara ya ukeketaji. “Mficha uchi hazai” na pia “Mficha donda ndugu kifo kitamuumbua” lazima tujifunze kwa nyenzo yenye nguvu, picha chokozi.

From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On Behalf Of Hildegarda Kiwasila
Sent: Tuesday, December 04, 2012 6:26 PM
To: wanabidii@googlegroups.com
Cc: wlac@wlac.or.tz; wildaf_tanzania@yahoo.com; tpfnet2007@yahoo.com; info@wat.or.tz; akaruwes@futuresgroup.com; lhrc@humanrights.or.tz; stella.mwambeja@yahoo.com; emajani@engenderhealth.org; haitz@helpagetz.org; tawla_tawla@yahoo.co.uk; mewataa@yahoo.com; envirocare@bol.co.tz; envirocare_2000@yahoo.com; wrdp@udsm.ac.tz; fabia_shundi@yahoo.com; sherrykassim@yahoo.com; kivamwo@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] NI ZAIDI YA UKATILI

Wadau wa Utokomezaji wa Ukatili wa kijinsia- kwa maoni yangu hakuna kuficha kitu hapa.Demetria Kalogosho ametufundisha kitu muhimu kwa kutuwekea picha sisi watu wazima tuone watoto wetu watakavyoteswa wakati mwingine bila ya ridhaa yetu. Ndygu anaweza akakuibia akamkeketa kwa kukuona wewe eti unajifanya msomi au umeokoka huzingatii mila. Ninaona kuficha ukweli kama aonavyo Nd Kailima Kombwey si sawa. Heshinda iwepo lakini tujadiliane na tuonyeshane ukweli. Ama sivyo hatutoweza kuelimisha jamii na sisi wenyewe kujua kinachoendelea nchini ambavyo ni kinyume cha haki za binadamu.

Tena hii picha ni ya mtoto mdogo. Watu wamejitoa ktk TV wakionyesha matende ya kutisha pamoja na kutitoa ktk gazeti akionyesha hydrocele lilivyomzidi ili apate msaada. Hii ni toto/sio ya maana kwa hizo.

Wapo watu wazima wanaokamatwa ukweni na kukeketwa kwa nguvu au anaviziwa wakati wa kujifungua nurse anapewa kaposho au akizalia kwa mkunga wa jadi mpango unafanywa. Wakati wa civil war uganda yupo mama alisimuliwa alivyokatwa kisha akabakwa kwa kuchangiwa, akatumbukizwa kwenye mto wenye mamba bahati akaweza kusota na kutoka, akatembea kilometa kadhaa. Hizi aibu za kutazama na kuongelea yanayotokea ktk mila na destruri zetu ndizo zinazofanya baadhi ya maovu yaendelee.

Vita vya congo, imetoka radioni na ktk TV wanaume wakilalamika kutendewa uchafu ktk vita lakini hawapati msaada wa ushauri na matibabu kwa kutokana na mila zetu na vizuizi vyake. Wanahitaji msaada na matibabu ya kuzuia na kutibu maambukizo lakini wanashindwa pa kuanzia aseme-nimebakwa (mwanaume amekabwa na wanaume). Inawanyima watu jinsi ya kupata misaada tunapoona kuficha ndio tija. Haipendezi.

 Kwani hata viongozi wa Siasa huogopa kwenda katika makabila yao kwenye majimbo yao walikochaguliwa (kwa wale waliochaguliwa kwao) kuongea na watu wao na wazee wa mila masuala ya kutokomeza mila potofu na tabia mbaya zinazoleta madhara. Hadi leo hii kabila linaweza likasimama na kusema-tutakeketa na tuna wasichana elfu 5 wa kufanya hivyo tuone wa kufanya kitu!!
Yanini tuwe na wanasiasa, wanasheria, makanisa, misikiti na viongozi wa dini maeneo hayo? Kwa nini tuwe na police, JWTZ na mahakama, wanaharakati, SOSPA, katiba na mahakama? Raia atawale na kusema yupo above wote hawa na tumtezame akikeketa? Tuyaongee, tuongee nao na taifa na vijana wao ambao pamoja na vyombo vya serikali na wanasiasa wa eneo hilo ni wengi kuliko hao wazee wachache.

Kuna la kujibu hapa. Tuyaongee, tuonyeshe ili kujenga ufahamu wa matatizo ili tusaidiane kuyatatua.  Ndio hivi kwa kutokuyaongea na kuonyesha wengi hudhania Matende na mabusha ni ugonjwa tu wa pwani unaotokana na nazi na madafu. Kumbe ni ugonjwa unaotokana na uchafu wa mazingira na joto na kuwepo mbu wa kusambaza vimelea.

Climate change inaleta mabadiliko na joto na ukame unazagaa, uchafu wa mazingira na uwepo wa kinyesi cha mifugo na vyoo vya shimo vitapeleka tende na hydrocele (busha) hadi juu Iringa na Kilimanjaro. si wanakuja DSM kuleta bidhaa na kufanya biashara, mabus yanakuja na yanarudi huko na mbu culex na vimelea vyake tunawapelekea culex wa milimani kwenye joto wanavibeba na kuvisambaza. Tuwaonyeshe picha ya tende na hilo lingine waone-maana hatuoni tunaona vimetuna ndani ya nguo unadhania ni dafu hilo. Kumbe ni kitu ambacho nawe unacho kinaweza kuharibika hivyo. Kuona kunasaidia kumbukumbu na ufahamu kwa asilimia 80%. Tukificha pseudo science ya kusingizia visababishi vya uongo kwa maradhi itaendelea.

Zipo video za wasichana na wavulana wakitahiriwa na zinatumika hapa nchini ktk kufundishia mangariba. Mimi ni mmojawapo niliyezitumia tuliagiza kutoka nje na kupata baadhi kutoka Wizara ya Maendeleo Secretariat ya kutokomeza Ukeketaji. Video hizo za Kenya, Somali, Uganda, ethiopia za wasichana na wavulana zilifunua watu akili na Ngariba au wakeketaji walishindwa kuangalia. Waliona ni ukatili ulioje hawajui kama nao huumiza na kuathiri watu kama walichokuwa wakiangalia.

Wapo wasichana waliotahiriwa lakini hawajui kama wametahiriwa kwani wamekua wakubwa wamejikuta hivyo walidhania ndio inavyokuwa hivyo. Baadhi imewaathiri kindoa baada ya kuolewa mume hamtaki anarudisha mke kwa wazazi kwani alichokiona hakubaliani nacho.

Wapo wanaopata madhara ya Fistula kutokana na FGC/FGM na akiwa na Fistula mume anamuacha maana(Ashakum)  msamba umeunganika na vagina kinyesi kinapitia mbele (ukeni) au anavuja mikojo mfululizo kibofu kimeunganika na vagina mikojo inatoka mfululizo kupitia mbele na hauna kizuizi kama hicho kinyesi. CCBRT imekuja imewafanyia akina mama na dada hawa wenye Fistula miujiza na kuwarudishia utu wao. Kijijini wanawaona watu hawa wenye fistula lakini wanasema-wamelogwa na watu kushikana uchawi. Mke mdoko kumshuku mkubwa etc. Kumbe ni Female Genital Cutting (FGC) kama kisababishi kimojawapo na kwa sehemu kubwa pia.

Tuwaonyeshe na tuonyeshe aina mbali mbali za makato (see mojawapo attached na ntaongeza kuwaonyesha nina vitabu vyake nivisake nibandike zaidi).

Tulionyesha Video tarafa ya Mikumi kwa makundi mbali mbali, tukajadiliana FGM.FGC na madhara yake. Tulipotembeza vipeperushi vya maelezo ya Fistula baada ya mafunzo hayo  tulipata wanawake wengi wenye Fistula (VVF na RVF) bila ya kutegemea tukawasafirisha kwenda CCBRT. Kama si mafunzo ya kuonyesha picha na video za FGM na madhara yake-na vipeperushi vya fistula tulivyopata Women Dignity Project na ikatuunganisha CCBRT tusingepata hao wagonjwa wa fistula ambao walikuwa ni wasichana wanaopendeza umri mdogo. Waliowengi wanaachwa na waume zao kutokana na hali zao za kinyesi na mikojo. Inataka moyo kuwasafirisha, kukaa nao kwako ili kesho umpeleke CCBRT au kama clinic imejaa ghafla umeambiwa asubiri a day or two. Bado hao ambao makato yamefanya ametunga usaha mbele, amefishwa kuogopa gvt, anaoza anaharibikiwa.

Tukubali kuzijadili na kuzionyesha na kuzitokomeza zile mbaya zenye madhara. Tusione aibu maana leo mwingine kesho ni mwanao au dadako, mjukuu wako anapata madhara haya ya kuepukika. Kupanua uke watoto wadogo (mwemba) na kuingilia visichana vidogo sexually (esoto) kama mila, kuoza vichanga etc vyote tuviongee na madhara yake na picha tusizifumbie macho. Heshima ya Mila na uafrika wetu viwepo inategemea unaangalia na nani-mtandao huu ni wa watu wazima. Yet utakuta vijijini watu wazima wanaangalia picha za matusi na watoto wadogo ktk vibanda vya nyazi kwenye video za kulipa. Pia kuna vibanda kwenye machimbo vya shutashuta (chapu chapu) tumejipanga foleni na vyangudoa na watoto wanatuona. Mitaani kila baada ya nyumba tatu kuna bar na watu wanakwenda haja hovyo watoto wanawaona. Ama wakati mwingine tu nduma kuwili.

Ikitokea ajali ya gari watu wapo hovyo kundi kubwa utaliona la watoto linaangalia, watu wamekatika vichwa n.k bado hizo dansi za matusi ya nguoni tunazoziona daima ktk TV watoto wanaangalia mama zao na baba, kaka zao wanavyocheza kwa kupekecha maeneo ya utupu. Tunashindwa kutokomeza haya ya wazi (utandawazi kama excuse). Kufundishana humu sisi watu wazima sio kosa hata. Ieleweke tunafunguka.

--- On Mon, 3/12/12, Vincent Mhangwa <vmhangwa@gmail.com> wrote:

From: Vincent Mhangwa <vmhangwa@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] NI ZAIDI YA UKATILI
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, 3 December, 2012, 8:02

Ni ukatili usiokubalika. Ni vizuri kwamba picha inatupa hisis ya jambo lenyewe na kuguswa sana. Lakini pia ni nudhalilishaji kwa watoto kuonesha picha kama hii. Napendekeza iondolewe kwenye mtandao.

Vin

On Mon, Dec 3, 2012 at 10:47 AM, kailima kombwey <kailima.kombwey@googlemail.com> wrote:

Kwa hiyo hata picha ya kichwa cha mtu kilichochinjwa na kutenganishwa au watu wanaopigwa picha wakiwa wanazini nazo ziwekwe hapa ili watu wajifunze? Hujuwi Desturi za Mwafrika Mtanzania? Unadhani picha hizo kuwa hadharani kutasaidia? Suala la kusaidia ni kuelimisha kwa kadri inavyowezekana na vyombo vinavyosimamia sheria kutumiza wajibu wao kwa wote wanaofanya haya na siyo kuweka picha hizi hapa. Tudhani ni ndugu yako wa kike utajisikiaje?

On Dec 3, 2012 10:21 AM, "Lutgard Kagaruki" <lutgardk@yahoo.com> wrote:

Nadhani si vibaya; hata ambao hatujawahi kuona tushuhudie. Kuficha hakusaidii.  Hata hivyo desturi zetu zipi?? Hii ni kwa ajiri ya kuwasaidia hata wengine. Mwili wangu umesisimka kwa woga na uchungu!! LKK

From: kailima kombwey <kailima.kombwey@googlemail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Cc: sophiawambura@yahoo.com; eneeso@pathfind.org; nathanielissa@ymail.com; tawla2000@yahoo.com; icnictz@gmail.com; envirocare_2000@yahoo.com; chesociety@yahoo.com; piastellah@yahoo.co.uk; info@hdt.or.tz; katri@kiwohede.org; markwambura@yahoo.com; mghambagrace@cdftz.org; envirocare@bol.co.tz; fchilimo@pactworld.org; netwo2002@yahoo.com; mewataa@yahoo.com; msangilaura@hotmail.com; Zumuni2008@yahoo.com; childrenwidows@yahoo.co.in; stella.mwambenja@yahoo.com; tomkiwala@yahoo.com; peacetanzania@yahoo.com; tahurifo1@yahoo.com; wofatatz@yahoo.com; adolfkissima@yahoo.com; fawetz@posta.co.tz; shivyawata@yahoo.com; mosesgasana@yahoo.com; Jansgar2002@yahoo.com; lrmbise@ywcatanzania.or.tz; MBetron@engenderhealth.org; elipunda@yahoo.co.uk; mwajey2003@yahoo.co.uk; berthaney@yahoo.com; mhinablandina@yahoo.com; mcharolydia@yahoo.co.uk; fnzema@hotmail.com; wlac@wlac.or.tz; info@tcib.or.tz; holmstrom@unfpa.org; lucy.merere@dfa.ie; eliza@yahoo.com; wildaf_tanzania@yahoo.com; tpfnet2007@yahoo.com; info@wat.or.tz; lucy.chamwi@yahoo.com; siltanmziray@yahoo.com; m.mshana@yahoo.com; laseha@gmail.com; murio@mst.org.tz; mawazochanya@gmail.com; children_widows@yahoo.com; judieus@yahoo.com; akaruwes@futuresgroup.com; merykessi@gmail.com; gearoid.loibhead@concern.net; mpungulez@yahoo.com; tawla_tawla@yahoo.co.uk; janethkeha@yahoo.com; mpangulez@yahoo.com; neemaduma@yahoo.com; deus.kibamba@tgnp.org; lhrc@humanrights.or.tz; gmtenga@unicef.org; khamar.kashoro@co.care.org; haitz@helpagetz.org; edacha2002@yahoo.com; gmunuo@yahoo.com; drkatanta@yahoo.com; b.ench@yahoo.com; ksimwanza@engenderhealth.org; floramasue@yahoo.com; merykessi@yahoo.com; stella.mwambeja@yahoo.com; fmakoye@yahoo.com; emajani@engenderhealth.org; lrmbise@ymcatanzania.or.tz
Sent: Monday, December 3, 2012 10:03 AM
Subject: Re: [wanabidii] NI ZAIDI YA UKATILI

Sidhani kama ilikuwa busara na kwa desturi zetu kuweka picha hii hapa.

Tuwe tunatumia busara walau kwa 23%  kabla ya ku uproad picha

On Dec 3, 2012 9:56 AM, "Demetria Kalogosho" <demetria.kalogosho@tgnp.org> wrote:

JAMANI WADAU WA GBV JIONEE UKATILI HUU

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment