Wednesday 5 December 2012

Re: [wanabidii] KAULI ya CHADEMA juu ya watumishi wa umma kutoa taarifa katika mikutano ya CCM

Jones,

Serikali ni ya ccm, hata upinzani watakapotawala uongozi wake utasimamia serikali yake. Mkataba wa wananchi kwa sasa ni kati yao na ccm, sio upinzani. Lakini pia usione kila kitu kinachoonekana hovyo kwa macho unahitaji mhandisi kukosoa! Kuna mambo na wizi mkubwa sana unaofanyika hususani kwenye ngazi ya halmashauri zetu waziwazi kwa kinga ya utendaji na utalaamu. Sidhani kujua daraja au jengo limejengwa kwa saruji kidogo unahitaji digrii!

Acheni checks and balance zifanyika kwa njia zozote! Watendaji mmezidi wizi na ufisadi na mnapoparanganya mambo mnasingizia serikali ya sisiemu! Wakomae nanyi labda mtapunguza wizi.
Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.

From: Jones Nyakwana <jonesn1478@yahoo.co.uk>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wed, 5 Dec 2012 08:32:15 +0000 (GMT)
To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] KAULI ya CHADEMA juu ya watumishi wa umma kutoa taarifa katika mikutano ya CCM

Hili jambo limenikera muda mrefu. Niliwahi kuhoji hapa mamlaka ya Nape kwenda UDOM kukagua na kutoa mashinikizo kwa uongozi wa chuo kuhusiana na ubora wa majengo ya chuo. Juzi nimemsikia mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita akitamka katika mkutano wa CCM huko Bukombe kuwa amelikataa bwawa la umwagiliaji ambalo lilikuwa linajengwa na mkandarasi chini ya usimamizi wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe. Hili nalo likanishangaza maana Mwenyekiti wa CCM wa mkoa si lazima awe muhandisi sasa sijui alishauriwa na nani na hata kama ameshauriwa, hayo mamlaka kapewa na nani....jibu lake naona ni kwasababu ni MBUMBUMBU wa taratibu za uendeshaji wa Serikali katika mfumo tuliopo.
 
Hawa watu wakiachwa waendelee na UMBUMBUMBU wao watawalazimisha walimu kurejesha maswali katika mitihani ya shule za misingi yaliyokuwa yakitutaka kutaja CCM imezaliwa lini, Makamu mwenyekiti wake wa taifa ni nani, katibu wa CCM wa taifa anaitwa nani n.k n.k.

From: Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, 5 December 2012, 9:54
Subject: [wanabidii] KAULI ya CHADEMA juu ya watumishi wa umma kutoa taarifa katika mikutano ya CCM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Kwa niaba ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) natoa mwito
kwa watumishi wa umma kote nchini kupuuza maagizo yaliyotolewa na
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu wake wa Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye ya kuwalazimisha kuhudhuria mikutano ya CCM na kutoa
taarifa za kiserikali kama yalivyotolewa katika baadhi redio na
televisheni tarehe 2 Disemba 2012 na kunukuliwa na magazeti mbalimbali
tarehe 3 Disemba 2012.

Pia namshauri Rais Jakaya Kikwete kwa mamlaka yake ya mkuu wa nchi na
kiongozi wa Serikali ambaye ndiye mwajiri wa watumishi wa umma wenye
kulipwa mishahara kwa kodi za wananchi wasio na vyama na ambao ni
wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa kukemea kauli kama hizo zilizo
kinyume na haki za kikatiba, misingi ya utawala bora, sheria na waraka
wa utumishi wa umma.

Aidha, CCM kutaka kujitwalia mamlaka ya Serikali kutoa maagizo kwa
watumishi wa umma badala ya vyombo vya usimamizi kwa niaba ya wananchi
kama bunge, baraza la mawaziri, mabaraza ya madiwani, kamati za
ushauri za wilaya, kamati za ushauri za mikoa, bodi za mashirika
mbalimbali na mamlaka nyingine ambapo wapo viongozi waliotokana na
chama hicho ni ishara ya udhaifu na uzembe wa viongozi wanaotokana na
chama hicho katika mikutano ya vyombo hivyo.

Maagizo hayo ya CCM yanazidi kuongeza sababu za wananchi kufanya
mabadiliko ya kweli kwa kuunga mkono CHADEMA ikiwa ndicho chama
mbadala chenye kuweza kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati
makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya taifa.

Maagizo haya ya CCM yanaashiria 'ulegelege' wa chama hicho na kuzidiwa
na vuguvugu la mabadiliko linaloongozwa na CHADEMA na madai ya
uwajibikaji toka kwa umma kwa kiwango cha kutaka kuirejesha nchi
katika maagizo yamfumo wa siasa wa chama kimoja ambapo kundi lote la
watumishi wa serikali na vyombo vyake walikuwa wakilazimishwa
kushiriki katika shughuli za CCM wakati ambapo kwa sasa watumishi hao
wengine ni wanachama wa CHADEMA na wapo ambao sio wanachama wa chama
chochote cha siasa.

Rais Kikwete aikumbushe CCM kuwa mapendekezo ya Tume ya Nyalali ya
mwaka 1991 na marekebisho ya Katiba ya mwaka 1992 kuingia katika mfumo
wa vyama vingi na marekebisho ya sheria yaliyofuata yameweka uhuru wa
watumishi wa umma katika kujiunga na vyama vya siasa (isipokuwa
watumishi wa kada maalum) na mipaka ya mahusiano kati ya kazi zao za
kiserikali na shughuli za vyama vya siasa kikiwemo chama
kinachotawala.

Naitaka CCM izingatie kuwa utumishi wa umma katika nchi yetu
unaongozwa na Sheria ya Utumishi Serikalini namba 16 ya mwaka 1989 na
Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma Toleo la 1994 pamoja na
marekebisho yake. Kifungu cha 4(1) cha Sheria hiyo kinampa mamlaka
Mkuu wa Utumishi wa Umma, ambaye ni Katibu Mkuu kiongozi kutoa waraka
kuhusu taratibu mbalimbali za utumishi wa umma.

Chini ya Mamlaka hayo, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Martem Y.C.
Lumbanga tarehe 26 Juni, 2000 alitoa Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa
Umma na. 1 wa mwaka 2000 wenye kumb. Na. SHC/C.180/2/113 uliohusu
maadili ya Watumishi wa Umma katika mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Waraka huo unawataka watumishi wa umma kutekeleza wajibu wao wa
utumishi bila kufanya upendeleo wala ubaguzi wa chama chochote cha
siasa. Waraka huo unawakataza watumishi wa umma kuzungumza na kutoa
taarifa kwenye mikutano ya vyama vya siasa na haujatoa ruhusa kwa
watumishi hao kuzungumza katika mikutano ya CCM pekee; hivyo maagizo
yaliyotolewa na chama hicho ni kinyume maagizo ya Serikali
inayoongozwa na chama hicho hicho.

Ikiwa Rais Kikwete atahalalisha maagizo hayo haramu ya CCM, watumishi
wa umma watawajibika pia kuitwa na kutoa taarifa kwenye mikutano ya
CHADEMA na vyama vingine vya upinzani nchini.


Imetolewa na:

John Mnyika (Mb)

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi

04/12/2012

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

DELL LATITUDE D 620 & D30

80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,2 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .

TSHS : 380,000 , 1 YEAR WARRANTY

CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.




0 comments:

Post a Comment